Watu 600 hawana makazi Mwanza

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
Kandoro%2812%29.jpg

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Abbas Kandoro.



[FONT=ArialMT, sans-serif]Familia zaidi ya 120 zenye takribani watu 600 hazina makazi kutokana madhara ya mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali iliyonyesha usiku wa kuamkia juzi mkoani Mwanza.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Watu hao wakitaabika, majina ya watu wanne kati ya watano waliofariki kutokana na mafuriko yaliyosabaishwa na mvua hizo yametajwa.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Waliofariki wametajwa kuwa ni Martha Samwel (25) na Yunis Peter (25) ambao ni wakazi wa Kisesa wilayani Magu, Wankuru Kilali (65) mkazi wa Kiseke na Mashauri Masasila (60), mkazi wa Buswelu jijini hapa. Mmoja bado hajafahamika.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Mkazi mwingine, Philemon William (25) alijeruhiwa na kulazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Mwanza ya Sekou Toure baada ya kuangukiwa na nyumba.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Nonosius Komba, alisema waathirika wa maafa hayo wamehifadhiwa katika shule za sekondari, msingi na kwenye maghala.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Akifafanua kufuatia mvua hiyo iliyoleta maafa makubwa, Kamanda Komba alisema katika eneo la Kisesa wilayani Magu nyumba 21 zilibomoka, wakati katika kijiji cha Ihushi nyumba 119 zilibomoka. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Alitaja vijiji vilivyoathirika na idadi ya nyumba zilizobomka kwenye mabano kuwa ni Sese (30), Matale (36), Buswelu (2) na Kiseke (1).[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Komba alisema kufuatia maafa hayo, tathmini itaendelea kufanyika kubaini ukubwa wa tatizo pamoja na madhara yaliyopatikana kutokana na mvua hiyo na kwamba taarifa zaidi zitatolewa.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Kamanda Komba alisema marehemu wote waliangukiwa na kuta za nyumba wanazoishi wakati mafuriko hayo yalipotokea.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Wakati huo huo serikali ya Mkoa wa Mwanza imeanza kuwasaidia watu walioathirika na mafuriko ambao wapo kwenye majengo ya shule kwa kuwahudumia kwa chakula na kuwatafutia maturubai kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za muda.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Abbas Kandoro, alisema watu hao kwa sasa wamehifadhiwa katika Shule ya Sekondari ya Ihushi kwenye jengo la utawala pamoja na nyumba ya mwalimu, lengo likiwa ni kutoathiri wanafunzi wanaoendelea na masomo.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Kandoro alisema kuwa barabara iliyokuwa imefungwa ya kuelekea Igombe kutokana na daraja lake kukatika kutokana na mafuriko hayo, imefunguliwa na mabasi yameruhusiwa kuanza kupita.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Kwa mujibu wa Kandoro, hatua hiyo imewezesha huduma ya usafiri kurejea katika hali ya kawaida wakati ukarabati ukiendelea.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Aidha, Kandoro amewataka wakazi wa mabondeni kuachana na ubishi na kukubali maelekezo yanayotolewa na viongozi.[/FONT]
“[FONT=ArialMT, sans-serif]Unajua ndio natoka huko sasa hivi, kama kijiji cha Ihushi walioathirika wengi ni wakazi wa mabondeni na walikwishaelezwa muda mrefu kuwa wahame kutokana na kuwepo kwa tishio la mvua za El-nino, lakini waliendelea kukaidi maelezo ya viongozi,” alisema Kandoro. [/FONT]



CHANZO: NIPASHE
 
Back
Top Bottom