Watoza ushuru wa parking Mwanza kero tupu!

SirBonge

JF-Expert Member
Jul 18, 2010
378
435
Naamini kwamba system ya kulipia Parking iliwekwa ili kuongeza mapato ya jiji na pia kufanya mpangilio mzuri wa kuegesha magari kusiwe na kero barabarani!
Jijini Mwanza hawa jamaa wanaotoza ushuru kwa kweli ni kero kubwa sana kwa sababu, wanafanya kazi kama MAROBOTI...kwanza sehemu nyingi hazina alama za kuonyesha kwamba unaruhusiwa kupaki au lah! hivyo watu wanatumia uzoefu, kwa hiyo wale wageni wanapata shida sana kujua na kwa bahati mbaya sana, wanakuvizia, wakiona unahangaika wanajificha na ukitoa mguu tu wanakufungia mnyororo-kutoka tena ni lazima ulipe faini ya tsh 50,000/-
Sehemu zingine mfano pale maeneo ya CBE, kuna parking lakini hakuna alama inayoonyesha kwamba unatakiwa upaki kimshazari au kiurefu, ukipaki kiurefu badala ya kimshazari, mambo ni yale yale tena! Na mbaya zaidi wakishakufungia gari yako, hakuna sehemu yoyote unayoweza kulalamika na kupatiwa haki...wanasema ni lazima ulipe kwanza halafu uandike barua kwa mkurugenzi wa jiji kulalamika...hii ni KOMEDI!
Nadhani hawa jamaa wanalipwa kutokana na magari ambayo wanayafunga kwa siku hivyo wanafanya juu chini wapate vichwa!

USHAURI;-Uongozi wwa jiji uboreshe alama za kuelekeza ni wapi kwenye parking na wapi hakuna, na gari lipakiwe vipi.
-Kama hilo haliwezekani basi kila mahali akae mtu anayemwelekeza dereva apaki vipi, sio kujificha mkiona dereva anakosea.
-Mfanye kazi kama binadamu wenye akili, sio kufunga tu minyororo hata kama mmekosea hamkai mkasikiliza maoni ya watu
wengine
 
Ni kweli hawa jamaa wanavizia hasa siku zinazokaribia sikukuu! Au jiji linahitaji hela za sherehe! Mimi walifunga gari yangu tarehe 7/8 wakalamba 30,000/. Jiji liweke alama sehemu ambazo haziruhusiwi na alama ya kuonyesha gari inapaki vipi? TUMECHOKA WIZI WENU!
 
Back
Top Bottom