Watoto wengi wa kitanzania hawana future.

Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
15,570
19,447
Tanzania ni nchi ambayo watoto wake wengi hawana future kabisa; wala hawafundishiwa kuwa binadamu wengi wa leo hawaishi kwenye mapango au chini ya miti.

attachment.php

Standard Three pupils of Chinyarira Primary School in Nanyumbu District, Mtwara Region, while away the time outside their classroom, as captured by our correspondent yesterday. (Photo:Correspondent Happy Severine)

Hiyo ndiyo halisi ya watoto wengi wa kitanzania. Ni wale wachache tu ambao wazazi wao walifaidika, kama Kikwete na Lowassa, kutokana na uongozi wa Nyerere wakapata elimu nzuri ya bure ndio leo wanaofaidi elimu nzuri katika shule za binafsi!!!
View attachment 27287
 
Hao watoto wanafuraha bwerere. Hebu waangalie walivyo strike mapozi. Utasemaje hawana mustakabali wa maisha yao haupo?

Mimi naona wako poa kabisa.
 
Tukisema miaka hamsini ya uhuru bila maendeleo viongozi wanajibu hatuna macho,pua,wala ubongo wa kufikiri, sasa miaka hamsini ya uhuru kama kuna watu wanasomea kwenye kilindio cha shamba la mpunga unategemea nini? si watakuja kuwa manamba tu hapo baadaye watoto hao? kwa kuwa elimu wanayopata hapo ni duni kama darasa lao, na walimu wao pia ni duni kwa kuwa hawatakuwa na mori wa kufundisha kutokana na mazingira duni wanayoishi.
 
Alexander the Great alipomaliza ku-conquer dunia yote, alikaa mlimamni na kuangalia himaya yake. Alilia sana na kwa dhati kutoka moyoni. Alipoulizwa analia nini, akasema "there is no more lands to conquer".

Sasa sisi, sorry - I mean viongozi wetu, wanapojiandaa kusheherekea miaka 50 ya uhuru wao, tunasimama juu ya mlima na kuangalia himaya yetu. Tunalia kwa uchungu wa dhati tunapoona ni FAILURES kila mahali. Elimi ni kituko, Miji inajikulia yenyewe, Makampuni ya umma ni mapango ya ufujaji, Uchumi ni shagala bagala, Nchi imekuwa omba omba mpaka tunatia kinyaa

Lakini cha kusikitisha kuliko vyote ni kwamba watoto wetu hawana future. Mtoto anamaliza Std 7 hajui kusoma, Form six hajui kuwa Jua liko katikati ya Solar system na dunia inalizunguka kwa siku 365. Kijana anamaliza degree yake ya Masters hawezi kutunga sentense moja ya kiingereza iliyonyooka. Na ma-PhD wetu wanashindana kuelekea Loliondo kwa Babu awapatie tiba ya kimuujiza.

Tanzania inaweza kabisa ikawa ni nchi yenye IQ ndogo kuliko zote ulimwenguni.
 
You have said it all mdau! Thank you!
 
Hio ndo TZ zaidi ya uijuavyo, future wataijuaje wakati wazazi wao wametekwa kiuchumi na majuha.
 
Alexander the Great alipomaliza ku-conquer dunia yote, alikaa mlimamni na kuangalia himaya yake. Alilia sana na kwa dhati kutoka moyoni. Alipoulizwa analia nini, akasema "there is no more lands to conquer".

Sasa sisi, sorry - I mean viongozi wetu, wanapojiandaa kusheherekea miaka 50 ya uhuru wao, tunasimama juu ya mlima na kuangalia himaya yetu. Tunalia kwa uchungu wa dhati tunapoona ni FAILURES kila mahali. Elimi ni kituko, Miji inajikulia yenyewe, Makampuni ya umma ni mapango ya ufujaji, Uchumi ni shagala bagala, Nchi imekuwa omba omba mpaka tunatia kinyaa

Lakini cha kusikitisha kuliko vyote ni kwamba watoto wetu hawana future. Mtoto anamaliza Std 7 hajui kusoma, Form six hajui kuwa Jua liko katikati ya Solar system na dunia inalizunguka kwa siku 365. Kijana anamaliza degree yake ya Masters hawezi kutunga sentense moja ya kiingereza iliyonyooka. Na ma-PhD wetu wanashindana kuelekea Loliondo kwa Babu awapatie tiba ya kimuujiza.

Tanzania inaweza kabisa ikawa ni nchi yenye IQ ndogo kuliko zote ulimwenguni.

UKIINGIA JF HATA KAMA UTAKASIRIKA..UTA-SMILE NA BAADAYE UTACHEKA...Thanks mdau...
 
Unatakiwa kufafanua nini maana ya future unayoitaka. Babu zetu hawakuwa na madarasa lakini waliishi, wewe na wengine mmesoma chini ya miti na sasa mmemaliza vyuo na mna hiyo future so usirukie jambo na kurusha humu.
 
Pia wewe Una IQ ndogo?
Nini Sababu ya yote hayo??
Nini unashauri??
Nini unadhani kifanyike?

My Take is most of us we tend to Blame when we see failures, and we tend not to associate with Failures,

Be real, this is your country, what is your contribution in your country!,
Perion.
 
Chakushangaza, Nanyumbu lilikuwa ni jimbo la Uchaguzi la Kigogo fulani hapa nchini kwa miaka kadhaa!!
 
Alexander the Great alipomaliza ku-conquer dunia yote, alikaa mlimamni na kuangalia himaya yake. Alilia sana na kwa dhati kutoka moyoni. Alipoulizwa analia nini, akasema "there is no more lands to conquer".

Sasa sisi, sorry - I mean viongozi wetu, wanapojiandaa kusheherekea miaka 50 ya uhuru wao, tunasimama juu ya mlima na kuangalia himaya yetu. Tunalia kwa uchungu wa dhati tunapoona ni FAILURES kila mahali. Elimi ni kituko, Miji inajikulia yenyewe, Makampuni ya umma ni mapango ya ufujaji, Uchumi ni shagala bagala, Nchi imekuwa omba omba mpaka tunatia kinyaa

Lakini cha kusikitisha kuliko vyote ni kwamba watoto wetu hawana future. Mtoto anamaliza Std 7 hajui kusoma, Form six hajui kuwa Jua liko katikati ya Solar system na dunia inalizunguka kwa siku 365. Kijana anamaliza degree yake ya Masters hawezi kutunga sentense moja ya kiingereza iliyonyooka. Na ma-PhD wetu wanashindana kuelekea Loliondo kwa Babu awapatie tiba ya kimuujiza.

Tanzania inaweza kabisa ikawa ni nchi yenye IQ ndogo kuliko zote ulimwenguni.

nakugongea thanks yangu ya 8 toka 2007! umeongea point mkuu
 
Unaweza kuitafasiri future kwa maana mbalimbali, binafsi kwa kuitafasiri picha, vijana wanafurahia na wana penda maisha yao. Umenikumbusha sinema zetu ambapo huwa wanadhani mhusika aliyeanza kama maskini huonesha kafanikiwa akihitimishwa yupo ndani ya hekalu na jacuz.

Future yao ipo hapo walipo
 
Future wanayo lakini siyo nzuri.

Uko sahihi, lakini future ambayo si nzuri ni kama siyo future

Unatakiwa kufafanua nini maana ya future unayoitaka. Babu zetu hawakuwa na madarasa lakini waliishi, wewe na wengine mmesoma chini ya miti na sasa mmemaliza vyuo na mna hiyo future so usirukie jambo na kurusha humu.

Dunia inakwenda na wakati. Mazingira waliyoshi watu wa zamani ni tofauti na mazingira wanayoishi vijana wa kizazi cha leo. Zamani mtu akimaliza darasa la nne anakuwa anaheshimika kuwa ana elimu nzuri, leo hii hata shahada ya chuo inaonkena haitoshi. Huwezi kutosheka na mazingira wanayoosomea watoto hawa kwa kuilinganisha na mazingiria waliyoshi watu wa zamani. Ni Mtazamo finyi sana unaofanywa na viongozi wetu unaonedelea kuwaacha watanzania katika maisha duni kama yale waliyoshi mika ya 40.

sema watanzania wengi hawana furuture we unafuture????

Ni kweli watanzania wengi hawana future nzuri. SDiwezi kudanyana kuwa sina future kwa vile sasa ninaishi katika future yangu nikila bonasi ya maisha kutokana na elimu nzuri iliyotolewa bure na Nyerere.
Unaweza kuitafasiri future kwa maana mbalimbali, binafsi kwa kuitafasiri picha, vijana wanafurahia na wana penda maisha yao. Umenikumbusha sinema zetu ambapo huwa wanadhani mhusika aliyeanza kama maskini huonesha kafanikiwa akihitimishwa yupo ndani ya hekalu na jacuz.

Future yao ipo hapo walipo

Vijana hao kufurahia mazingira hayo ni kwa sababu hawana matazamo mpana wa maisha. Ukosefu wa mtazamo ndio unaowaacha wakiwa hawana future. Walinganishe watoto hao na watoto wa umri wao katika nchi kama China au Singapore ili ujue dunia iinaionaje future. Nyerere alifundisha kuwa "We must run while they walk." sisi tunasimama kabisa na kuchekelea wakati wenzetu wanakimbia. Tutakuta wameshachukua future yote.
 
Unatakiwa kufafanua nini maana ya future unayoitaka. Babu zetu hawakuwa na madarasa lakini waliishi, wewe na wengine mmesoma chini ya miti na sasa mmemaliza vyuo na mna hiyo future so usirukie jambo na kurusha humu.

Babu zetu walikuwa hawana darasa lakini watoto wao (mababa zetu) walipata elimu bora, kwa hiyo baba zetu walikuwa na future. Hebu angalia wazee wetu walioenda shule halafu linganisha na hizi product za siku hizi ujiulize, "hivi nimeelewa mada inayozungumzwa au nimekurupuka".

Ni kwamba inabidi kila kizazi kipya kipate elimu bora kuliko kizazi kinachoondoka. Kama mnafanya kazi kwa umakini hili huwa linawezekana kwani mnajenga tu kutoka pale mlipofika jana. Bahati mbaya sisi tunaboronga, badala ya kuendeleza tulipofika, tunabomoa. Kila waziri wa elimu anakuja na experiment yake.

Dawa;

1. Shule zote zilizotaifishwa zirudishiwe wenyewe. Tambaza, Zanaki, Kisutu, Azania... Rudisha
2. Lugha ya kufundishia iwe English from Std One
3. Punguza mashangingi na posho za viongozi, Ongeza mishahara ya walimu
4. Leta standard ya elimu inayokubalika kimataifa, e.g. Cambridge O Level, A Level

Back
Top Bottom