Watoto wanaonyonya maziwa ya mama wafikia asilimia 64

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,024
1,616
Takwimu za watoto wanaonyonyeshwa maziwa ya mama pekee imeongezeka kutoka asilimia 58 ya mwaka 2018 hadi kufikia asilimia 64 mwaka 2022.

Pamoja na hilo takwimu za watoto wanaonyonyeshwa ndani ya saa moja baada ya kuzaliwa zimeongezeka kutoka asilimia 53.5 mwaka 2018 hadi kufikia asilimia 70 mwaka 2022.

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Afya, Dk Godwin Mollel wakati akizindua maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji ambayo yalianza kuadhimishwa nchini mwaka 1993

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Dk Mollel amesema kuongezeka kwa takwimu hizo ni mafanikio ya elimu inayoendelea kutolewa katika jamii ikiwemo maadhimisho ya wiki hiyo yanayofanyika kila mwaka.

Pamoja na mafanikio hayo amesema utekelezaji na ufuatiliaji wa haki za uzazi kwa wanawake hapa nchini unakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uelewa duni wa baadhi ya waajiri, wafanyakazi na jamii kuhusu jambo hili.

“Changamoto nyingine ni ukiukwaji wa haki za uzazi za wanawake wanaofanya kazi katika baadhi ya sekta rasmi na sekta zisizo rasmi. Hii inatokana na kukosekana kwa mazingira wezeshi katika mifumo ya kijamii ya kuwasidia wanawake waweze kuwanyonyesha watoto wao ipasavyo.

“Nachukuwa fursa hii kuendelea kuhimiza waajiri katika sekta rasmi na zisizo rasmi na jamii kwa ujumla kuwasaidia wanawake waweze kunyonyesha watoto wao huku wakiendelea kufanya kazi,” amesema Dk Mollel.

Akizungumzia hilo mwakilishi wa Tume ya Usuluhisi (CMA) iliyo chini ya ofisi ya Waziri Mkuu, Yohana Masawe amewataka wanawake walio katika maeneo ya kazi na kukutana na vikwazo vya kuzuia unyonyeshaji kupeleka malalamiko yao.

“Kama unakutana na changamoto ya aina hii mwajiri anakuzuia muda wako wa kunyonyesha, lete malalamiko

yako tutayshughulikia milango iko wazi ila watu hawajitokezi kuleta malalamiko hayo,” amesema Yohana.

Source; Mwananchi
 
Back
Top Bottom