Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,502
- 9,280
Wanawake wanakumbana na viwango vya umasikini vya juu kuliko Wanaume, na pengo la kijinsia katika Umasikini linatarajiwa kuendelea hadi katikati ya karne.
Takwimu za Kimataifa kutoka UN Women zinaonesha, asilimia 10.3 ya Wanawake Duniani wanaishi katika Umasikini wa kutisha kuliko Wanaume.
Takwimu kutoka Nchi 48 zinazoendelea zinaonesha Dola zaidi ya bilioni 360 zinahitajika kila mwaka ili kufikia Usawa wa Kijinsia pamoja na kumaliza Umasikini na njaa.
Maendeleo kuelekea kumaliza Umasikini yanahitaji kuwa mara 26 zaidi ili kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG's) ifikapo 2030.
Aidha, Mgogoro wa sasa wa Chakula na Nishati unawaathiri Wanawake kwa kiasi kikubwa, sababu pengo la Kijinsia la Kimataifa katika Ukosefu wa Chakula lilikuwa asilimia 2.4 Mwaka 2022.
Mabadiliko ya hali ya Hewa na Upotevu wa Bioanuai una athari kubwa kwa Wanawake na Wasichana, haswa wanaotegemea Rasilimali asilia kwa Chakula, Maji, na Nishati. Wanawake na Wasichana milioni 158.3 wanaweza kuingia katika Umasikini ifikapo Mwaka 2050.