Watoto wa wakubwa hawasemwi vibaya kwanini Januari Makamba tu?

juma30

Senior Member
Jun 25, 2022
149
421
Kuna maneno yanasemwa sana humu JF kwamba watu wanamuonea wivu Januari Makamba ndio maana wanamkosoa juu ya utendaji wake wa kazi ni kwa sababu tu ametoka kwenye familia bora ya uongozi

Watoto wa Mwalimu JK Nyerere kina Makongoro Nyerere RC wa Manyara mbona hawana kesi na umma na hawasemwi kwa lolote

Kwanini Hussein Ali Mwinyi- Rais wa Zanzibar hajawahi kusemwa kwa ubaya wowote licha ya kuwa Mtoto wa Rais Mstaafu wa Zanzibar na baadaye Rais wa JMT na tunaona mageuzi anayoyafanya Zanzibar.

Watoto wa Benjamini Mkapa ambaye nadhani mmoja ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi kama sikosei mbona licha ya Baba yake kuwa Rais wa JMT hasemwi kwa lolote

Watoto wa Mstaafu Rais Jakaya Kikwete, Ridhiwani Kikwete mbona yeye anaonekana ni mtu mwenye kuongelewa vizuri na watu sio mtu wa kujikweza na hata majukumu haya mapya aliyopewa ya Naibu Waziri wa Ardhi anaonekana ameanza vizuri na hakuna anayelalamikia utendaji wake.

Watoto wa Dk. John Pombe Joseph Magufuli ndio hawakusika kabisa enzi baba yao akiwa Rais wanaonekana siku ya mazishi ya Baba yao

Hii dhana kwamba Januari Makamba anaonewa wivu kwa sababu ni mtoto wa Mkubwa sasa yeye ambaye Baba yake aliishia kwenye Katibu Mkuu wa CCM na hao ambao baba zao wameishia kwenye Urais kabisa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nani wazazi wao walikuwa watu wakubwa kwenye nchi hii.

Alafu tunaletewa maneno kwamba Januari amelelewa vizuri na Mzee Mkapa na Kikwete sasa yeye atakuwa amepata malezi bora zaidi ya akina Ridhiwani au Nicholas?

Swali la kujiuliza kwanini Jakaya Kikwete hakuwahi kumpa Uwaziri kamili kama alimuamini uwezo wake kwanini aliishia kumpa Unaibu Waziri tu tena wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mei Mwaka 2012 akahudumu kwa miaka mitatu tu kufikia 2015 mwisho wa utawala wa JK.

Tutatafakari kwa pamoja kama kuna mahali nimekosea mnaweza kunisahihisha.
 
January aacha tabia za kuharibu halafu anasingizia watu kumchukia

hajawahi kuwa mtendaji mzuri kwenye kila eneo la kiuongozi alilopitia.
 
January ana potential kubwa kuliko watoto wengine wote wa wakubwa. January ni threat kwa wasakavyeo wote unaowajua wewe.

In short mti wenye matunda ndiyo unapigwa mawe. But watake wasitake January ndiye the next president.
 
Nadhani ungeweka wazi Potentiality yake kwanza katika utendaji kazi wa shughuli za Umma na matokeo anayozalisha kabla ya kulaumu hao unaowaita wasaka vyeo
 
Hqjawahi kutenda kazi kinyume na maelekezo ya mteuzi wake. The guy is so smart ktk kazi zake. Unasemaje juu ya hilo?
 
Ni kweli kina Hussein Mwinyi Rais wa SMZ sijawahi kumsikia akitajwa kwa ubaya wowote hata huyu Ridhiwani nadhani tumpe muda maana kazi za Serikali ndio ameanza juzi sidhani kama ana doa lolote kwenye u Naibu Waziri wake wa Ardhi.
 
Kuna maneno yanasemwa sana humu JF kwamba watu wanamuonea wivu Januari Makamba ndio maana wanamkosoa juu ya utendaji wake wa kazi ni kwa sababu tu ametoka kwenye familia bora ya uongozi

Watoto wa Mwalimu JK Nyerere kina Makongoro Nyerere RC wa Manyara mbona hawana kesi na umma na hawasemwi kwa lolote

Kwanini Hussein Ali Mwinyi- Rais wa Zanzibar hajawahi kusemwa kwa ubaya wowote licha ya kuwa Mtoto wa Rais Mstaafu wa Zanzibar na baadaye Rais wa JMT na tunaona mageuzi anayoyafanya Zanzibar.

Watoto wa Benjamini Mkapa ambaye nadhani mmoja ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi kama sikosei mbona licha ya Baba yake kuwa Rais wa JMT hasemwi kwa lolote

Watoto wa Mstaafu Rais Jakaya Kikwete, Ridhiwani Kikwete mbona yeye anaonekana ni mtu mwenye kuongelewa vizuri na watu sio mtu wa kujikweza na hata majukumu haya mapya aliyopewa ya Naibu Waziri wa Ardhi anaonekana ameanza vizuri na hakuna anayelalamikia utendaji wake.

Watoto wa Dk. John Pombe Joseph Magufuli ndio hawakusika kabisa enzi baba yao akiwa Rais wanaonekana siku ya mazishi ya Baba yao

Hii dhana kwamba Januari Makamba anaonewa wivu kwa sababu ni mtoto wa Mkubwa sasa yeye ambaye Baba yake aliishia kwenye Katibu Mkuu wa CCM na hao ambao baba zao wameishia kwenye Urais kabisa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nani wazazi wao walikuwa watu wakubwa kwenye nchi hii.

Alafu tunaletewa maneno kwamba Januari amelelewa vizuri na Mzee Mkapa na Kikwete sasa yeye atakuwa amepata malezi bora zaidi ya akina Ridhiwani au Nicholas?

Swali la kujiuliza kwanini Jakaya Kikwete hakuwahi kumpa Uwaziri kamili kama alimuamini uwezo wake kwanini aliishia kumpa Unaibu Waziri tu tena wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mei Mwaka 2012 akahudumu kwa miaka mitatu tu kufikia 2015 mwisho wa utawala wa JK.

Tutatafakari kwa pamoja kama kuna mahali nimekosea mnaweza kunisahihisha.
KWANI Januari ni Mtoto wa Mkubwa yupi?
 
kusemwa vibaya si kigezo pekee cha kuhitimisha kuwa wewe ni mbaya ni sawa na kusemwa vizuri sio kigezo pekee cha kusema Wewe ni mzuri

Kama Hayati Dr John Magufuli pamoja na yote mema aliyofanya bado alikuwa anasemwa vibaya na baadhi ya watu
 
Timu Mwigulu mkisikia jina LA January mnatamani kujiharishia. Hivi kwanini mmeanza kampeni mapema hivi???
 
Sitaki kuwa biased wala siko personal
Ngoja niandike ninachokijua
Ramadhani kingai our new DCI na January Makamba ni mtu na kaka yake
Kingai kakulia kwenye household ya mzee Makamba mzee wa kisambaa mizaa mingi ila akao mama wa kihaya toka kyaka a very strict woman.
Connect dots
 
Mtoa mada acha kujificha kwenye mkaranga, hata huyo Ridhiwani Kikwete mnamsema mno......ni hv tu karibuni angalau kimepita kimya na nguvu zimemuelekea huyu makamba!
Halafu mashambulizi dhidi ya makamba yamezidi kipindi alichofanya ziara kanda ya ziwa,
 
Back
Top Bottom