Hakuna cha kupoteza yani ni kuharibu tu sababu wangu mimi niliye na mamlaka hapiti mfumo huo. Hali ndio inafanya watoto wenu wapitie magumu hayo.Mtoto kasoma mika saba, likizo anakua na tuition, amemaliza la saba, anakaa wiki tatu anarudi kambini tena kwa jina la pre-form one, wazazi watakaa na watoto wao muda gani? Hivi huko kwa wenzetu nako ni mchaka mchaka hivi hivi?
Litawezekana vipi wakat watu wamemalza shule na wameondokaMada nzuri ila umekosea kuiwasirisha,title wambie mods waiediti,kiufupi eti serikali inataka watoto waanze kusoma tena wale waliomaliza darasa la saba
Ujumbe tulitumiwa walimu huu hapa
Wakuu wa Shule, tumepokea maelekezo toka kwa Katibu Tawala wa Mkoa kuwa tunatakiwa kuanza English Orientation Course tarehe 02.10.2023 kwa wanafunzi wote waliomaliza darasa la Saba 2023.
Haya ni maelekezo, kwahiyo Kila mmoja aandae mazingira ya kuwaweka wanafunzi hao.
Labda ninachoweza kupokea toka kwenu ni ushauri wa namna gani tufanye na tuanze muda gani.
Najua mko safarini lakini hebu tulijadili hili Ili niwape maelekezo ma AEK.
Wao nilishaambia kuhusu kuwaeleza Walimu Wakuu Maxence Melo tusaidie kuiweka vizuri heading ili wizara ya elimu ipige marufuku hili jambo kwani linawanyima watoto muda wa kupumuzia
Shule Kama st Francis's ya mbeya haina haya mambo na matokeo Yao ni safi kabisa.Ninachojua wenzetu huu ujinga hawana, sio nani alileta haya mambo. Mtoto hajapumzika hata kidogo anapelekwa pre form one, then shule zinafunguliwa, sijui nani anatuletea huu ujinga...na sisi tunaubeba kama ulivyo.
Sasa hivi kuna ile ya kumuanzisha mtoto class one akiwa 4-5yrs, mambo yamekuwa mengi sana.