Watendaji Dawati la Jinsia ‘kupewa mbinu mpya’ Dodoma

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,462
Watendaji wa Dawati la Jinsia na Watoto kutoka Tanzania Bara na Zanzibar wapo Jijini Dodoma lengo likiwa ni kuwapa mafunzo nambinu za kukabiliana na vitendo vya ukatili vinavyofanywa na baadhi ya watu wenye ulewa mdogo na imani potofu.
2114be7e-41ae-4622-9095-708b8d09143a.jpeg

Msemaji wa Jeshi la Polisi, Kamishna Msaidizi wa Polisi SACP David Misime

Taarifa hiyo imetolewa Jijini Dodoma na Msemaji wa Jeshi la Polisi, Kamishna Msaidizi wa Polisi, SACP David Misime ambapo amebainisha kuwa Kikao hicho kinatarajiwa kufunguliwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini kikiambatana na watendaji zaidi ya 300 ambao watashiriki kikao hicho.

Ameongeza kuwa mafunzo hayo yanaenda sambamba na Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia ambapo watendaji wanatarajia kufanya kikao kazi Jijini Dodoma kuanzia Disemba 8 hadi Disemba 17, 2023 kwa lengo la kuweka mikakati na kujifunza mbinu mbalimbali za kukabiliana na vitendo hivyo.

mbali na kufanya kikao hicho watendaji wa dawati watafanyatathmini ya utekelezaji wa majukumu ya Dawati kwa kipindi cha mwaka mmoja, Pia kutakuwepo na mafunzo ya siku mbili yatakayotolewa na wadau mbalimbali na namna bora ya kutekeleza majukumu yao ikiwemo kutoa huduma bora na zenye ufanisi zaidi” Alisema SACP Misime.

Pia Msemaji wa Jeshi hilo amebainsha kuwa pamoja na mafunzo hayo kwa watendaji hao watapita katika mitaa mbalimbali ya Jiji la Dodoma kutoa elimu kwa Wananchi lengo ikiwa ni kujenga uelewa wa athari za vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa jamii.
 
Back
Top Bottom