Vyamavingi
JF-Expert Member
- Oct 3, 2014
- 5,745
- 5,446
Mimi ni miongoni mwa watumiaji wa gesi ya Taifa Gas kwa ajili ya matumizi ya nyumbani. Wiki 4 zilizopita nilienda dukani kununua gesi [kubadilisha mtungi]. Wakati nauinua nikasikia kimiminika [gesi] ikicheza ndani kwa ombwe kubwa.
Kwa kuwa mwenye duka anao mzani [nilimshauri hivyo kufuatia agizo la serikali kuwa wauzaji wa gesib lazima waweke mizani ili wateja wahakiki ujazo] ilibidi niupime pale pale. Huwezi kuamini, kulikuwa na upungufu wa gm 950, yaani karibu kilo nzima! Akanipa mtungi mwingine, nao ukawa umepungua pia! Mtungi wa tatu ndio ukawa sawa.
Wiki iliyopita gesi ikawa imeisha, kwa kuwa sikuwa na pesa ya kutosha ikabidi nichukue mtungi mdogo kabisa, na kwa kuwa imani yangu kwa Taifa Gas ilikuwa imepungua nikaamua kuupima. Amini usiamimini, nao ukawa umepungua! Nikachukua mtungi mwingine, nao ukawa umepungua vilevile hadi nilipopata mtungi wenye uzito sahihi.
Kwa uzoefu huu nawafahamisha wateja wenzangu wa Taifa Gas kuwa makini wanapobadilisha mitungi hiyo. Wito wangu kwa Taifa Gas ni kuwa watutendee haki wateja wao, mwenye duka aliniambia Oryx ndio mitungi ya uhakika, Oryx sio kampuni ka kizalendo, faida yao kwa sehemu kubwa inaenda kwa Wazungu, sasa huyu Mtanzania mwenzetu wa Taifa Gas anavyotufanyia uzalendo unaanza kunishinda.
Vv