Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,566
- 41,085
Kama una mpinzani au mshindani, halafu ukafanya jambo ambalo mshindani wako huyo alitarajia utafanya, na ukafanya kwa namna ile ile huyo mshindani wako alitarajia, wewe uliyefanya utakuwa umefeli na unathibitisha jinsi ulivyo na uwezo mdogo kiakili na kimbinu.
Kwa mfano ukiwa na timu mbili shindani A na B za mpira. Timu A ikitaka kuishinda timu B, cha kwanza inabidi ijenge hypothesis ya namna gani timu B itacheza, itawatumia wachezaji gani, itatumia mfumo gani katika ulinzi na ufungaji. Na kisha timu hiyo A, kwa kutumia hypothesis hiyo, ndipo itatengeneza mbinu ya kuishinda timu pinzani B. Kama timu B itacheza kwa namna ile ile timu A ilivyotarajia, kutakuwa na uwezekano mkubwa wa timu B kufungwa, kwa sababu ile timu B itakuwa imefanya kama timu A ilivyotegemea, na timu A itakuwa imejipanga kwa hilo lililotegemewa.
Kama timu B itakuwa na kocha mzuri, nayo itakuwa imeweka hypothesis yake ni kwa namna gani timu A inataka iupate ushindi. Hivyo, au tangu mwanzo wa mchezo, au wakati mchezo unaendelea itabadilisha mbinu ili timu A isipate ushindi dhidi yake.
Serikalini, bila shaka wamekaa watu wenye uwezo mdogo sana, watu ambao zaidi wanatumia nguvu ya mwili kuliko nguvu ya akili.
Dr. Slaa wakati akipambana kutetea rasilimali bandari isiporwe na waarabu kwa msaada wa watawala wabinafsi na wala rushwa, alisema kuwa alikuwa amesikia kuwa wanataka kumnyang'anya hadhi ya ubalozi, na akasema wazi kuwa wamnyang'anye huo ubalozi hata siku ile ile, lakini hawezi kukaa kimya. Cha ajabu, watawala hawa, sijui ni kwa kukosa maarifa au akili, wamefanya vile vile kama Dr. Slaa alivyotarajia. Kwa hapa ni watawala waliofeli, wamedhihirisha uwezo mdogo wa akili.
Hadhi ya ubalozi ni nini mbele ya hadhi ya utu wa kupigania? Ni takataka tu. Hadhi iliyo kubwa kuliko zote, na ambayo hupewi na mtu bali Mungu pekee yake, ambayo una uwezo wa kuilinda au kuipoteza, ni utu wako.
Mathalani, hawa watu majizi na wala rushwa, waliouza bandari zetu kwa malipo ya rushwa, hata kama wanaitwa Mawaziri, mabalozi au hata wangeitwa mawaziri wakuu, marais, marais wastaafu, n.k. wana hadhi gani wakati wamepoteza utu wa heshima na haki?
Furahini nyote mnaosumbuliwa, mnaoteswa na mnaoonewa na watawala waliokosa utu, kwa sababu tu mnatetea na kupinga uporwaji wa bandari za nchi yetu, kwa kuwa ninyi ni wakubwa kuliko watawala wevi na wanaouza bandari kwa malipo ya hongo, majina yetu yana utu katika Ulimwengu wa haki, na ni washindi dhidi ya uovu. Ninyi mna ushindi wa kudumu, na hawa watawaka wevi na wala rushwa wana ushindi bandia wa muda mfupi.
Dr. Slaa unastahili kushukuru kwa sababu katika Ulimwengu wa Roho, umetenganishwa na uovu na waovu, kamba iliyokuwa inakuunganisha na uovu, waovu wenyewe wameikata. HONGERA SANA.