Watatu mbaroni mauaji ya wanandoa Shinyanga

Oldmantz

JF-Expert Member
Jan 24, 2023
430
996
Shinyanga. Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kuwashikilia watu watatu kwa mahojiano kuhusu tukio la mauaji ya wanandoa wawili yaliyotokea katika Kijiji cha Mwagimagi Wilaya ya Kahawa mkoani Shinyanga.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Janeth Magomi amesema mauaji hayo yalitokea usiku wa Juni 29, mwaka huu ambapo watu wasiojulikana wanadaiwa kuwaua mume na mke kwa kuwakata shingo kwa kitu chenye ncha kali.
Akizungumza na Mwananchi Julai 7, 2023, Kamanda Magomi amewataja waliouawa katika tukio hilo lililoacha hofu miongoni mwa wakazi wa kijiji hicho kuwa ni William Manyama (60) na mkewe Christina Mahela (50).

Mwenyekiti wa Kijiji cha Mwagimagi yalipotokea mauaji hayo, Fabian Vitalis ameiomba Serikali kuwajengea kituo cha polisi kutokana na kukithiri matukio hayo akidai hata wanandoa hao walikutwa na madhira hayo wakiwa wamelala.

Vitalis amesema wako mpakani na hifadhi ya Kigosimoyowosi eneo ambalo linahitaji kuwa na ulinzi wa kutosha ili kudhibiti matukio ya uhalifu na mauaji ya watu wasiokuwa na hatia.
Amesema matukio ya mauaji yamekuwa yakitokea mara kwa mara ambapo mbali na mauaji ya mke na mume yaliyotokea Juni 29 pia kuna mwanamke mwingine miezi michache imepita alikutwa ameuawa kwa kukatwa mapanga mpaka leo hawajui nani alihusika hivyo kuwa na hofu.

"Matukio haya yanatuumiza sana kama hili ambalo limetokea wiki iliyopita, tunaomba Serikali iliangalie hili kwa kweli hali siyo nzuri ulinzi unahitajika tupate msaada wa polisi katika eneo hili"amesema Vitalis
Akisimulia tukio la wazazi wake kuuawa, William Charles amesema mauaji hayo yalifanyika usiku wakiwa wamelala na wala hawakusikia kelele za wazazi wao kuomba msaada, baada ya kuamka asubuhi walikuta damu sebuleni na walipofungua mlango wa chumba walikuwa tayari wamekufa huku shingoni wamekatwa na na kitu chenye ncha kali.

Baadhi ya wakazi wa Kijiji hicho wanayahusisha matukio ya mauaji na imani za kishirikina kutokana na namna yanavyotokea huku wakiomba uchunguzi wa kina ufanyike ili kujua chanzo chake na kuwaondoa hofu wananchi.

Naye Mbunge wa Ushetu, Emannuel Charehani amesema watu wote waliohusika na mauaji hayo watakamatwa kutokana na uchunguzi wa jeshi la polisi unaoendelea ili kukomesha mauaji hayo.

Amewataka pia wanachi kuacha kupokea wageni ambao hawawafahamu na kukaa nao bila taarifa kwa viongozi wa Kijiji.

CREDIT: MWANANCHI
 
Back
Top Bottom