Watatu Mbaroni kwa mauaji ya mfanyakazi wa Mgodi wa GGM Milembe Selemani

Kitimoto

JF-Expert Member
Aug 25, 2012
5,017
4,675
Jeshi la Polisi limewakamata watuhumiwa watatu waliofanya mauaji ya mfanyakazi mmoja wa Mgodi wa GGM kwa jina la Milembe Selemani katika mtaa wa Matulole, Kata ya Buhalahala mkoani Geita.

Aidha Mtuhumiwa wa nne (Pastory Lugodisha), baada ya kupata taarifa ya kukamatwa kwa wahalifu wenzake aliamua kujinyonga kwa kutumia mkanda wa suruali katika pori la hifadhi ya Buhindi Wilayani Sengerema.
56877832.jpg

"Kutokana na Uchunguzi makini wa askari wanaochunguza matukio ya mauaji wamefanikiwa kukamata watuhumiwa watatu kuhusiana na mauaji ya mfanyakazi mmoja wa Mgodi wa GGM Milembe Selemani aliyekua maarufu kwa jina la Hungwa siku ya Aprili 26, 2023 katika mtaa wa Matulole kata ya Buhalahala Mkoani Geita."

SACP- Misime Amesema watuhumiwa hao wameonyesha vielelezo walivyotumia katika Mauaji hayo ikiwa ni pamoja na baadhi ya mali za marehemu, na watafikishwa mahakani wakati wowote.

"Mtuhumiwa wa nne katika tukio hili baada ya kupata taarifa ya kukamatwa kwa wahalifu wenzake na kwamba askari wamefika nyumbani kwake, aliamua kujihukumu mwenyewe kwa kujinyonga, Mtuhumiwa huyo amejulikana kwa majina ya Pastory Lugodisha @ Buchuchu na alijinyonga mei 06, 2023 kwa kutumia mkanda wa suruali katika pori la hifadhi ya Buhindi Wilayani Sengerema".Ameeleza SACP- Misime

Pia, Soma: TANZIA - Afisa Ugavi wa mgodi wa Geita, Milembe Suleiman auawa na viganja vyake kukatwa
 
Shida ya Mauaji ya kukusanyana.

Muuaji angekuwa mmoja na anajielewa wasingemdaka.

Hata hivyo kitendo cha kuondoa uhai wa mtu ni jambo zito mno
 
Watu wa vijijini wanafanya uhalifu wa kishamba sana ambao kukamatwa ni kesho asubuhi. Wanaacha alama nyingi sana.


hakuna tukio kama hiloo usiache starting point damu ya mwanadamu ni hatari sana. ata uko kwa wazungu hii ngoma wameshindwa. kianzio cha ushaidi kitapatikana tuu.
 
Watu wa vijijini wanafanya uhalifu wa kishamba sana ambao kukamatwa ni kesho asubuhi. Wanaacha alama nyingi sana.
Kuna vijana walikodiwa kuua na kumkatakata vipande mzee mmoja huko Dodoma,kwa malipo ya gunia 4 za karanga,by then gunia moja lukiuzwa tsh15000/=, hapo ndipo nikagundua kuwa kule pori naweza kuwawa kijinga, maana Nilikua nanunua mahindi,nalala nacash 2 m, ikanibidi ninunue sime la kimasai kwa self-defense,huko vijijini unaweza kupotezwa Kijinga tu
 
Back
Top Bottom