Watanzania wenzangu, kuna siku tutawakumbuka CHADEMA

bampami

JF-Expert Member
Nov 5, 2011
5,697
4,107
Habari ya mchana!

Nimewaza sana sana leo, toka upinzani wa kweli uanze katika historia ya nchi yetu, ni wazi kuwa kuna kundi la watu ambao wameunda chama despite of their weakness lakini wamekuwa kiungo mhimu sana kwenye maendeleo ya nchi yetu.

Ni wazi kuwa toka CCM iwe madarakani imeleta mendeleo mengi despite of their weakness lakini kuna mambo mengi upande wa negative ama kwa kupanga ama kutopanga lakini yameiathiri sana nchi yetu. Lakini upinzani ama chadema wamekuwa mstari wa mbele sana kuyafichua/kuyapinga kwa nguvu zote japokuwa wapo wachache na ingawa wamedhurika sana na maamuzi yao lakini wamekuwa si watu wa kukata tamaa.

Ninani asiyejua ufisadi mkubwa tena wa aina mbalimbali uliofanywa na serikali kuanzia awamu ya tatu lakini ukafichuliwa na upinzani?!!

Hawa watu wachache kati ya wengi,
• Wamepewa makesi ya kutosha
• Wamewekwa ndani vya kutosha
• Wamepigwa risasi vya kutosha
• Wamekejeliwa na kukebehiwa vya kutosha
• Wamepotea mpaka leo wengine bado hatuwaoni
• Wangapi waliokufa kwa kupigani HAKI?
• Wangapi FAMILIA zao zimeathirika na upiganiaji
wao HAKI katika nchi?

Hawa watu (wapinzani wazalendo) pamoja na wanaharakati waliobaki na wasiokata tamaa kupigania HAKI nchi hii, wangeweza sana kuunga mkono juhudi lakini bado misimamo yao na uzalendo wao umebakia mioyoni mwao.

Yote hayo ni kwa ajili yetu sisi watanzania.Lakini pamoja na yote bado tumekaa kimya hatuwapi support katika uzalendo wao katika nchi hii.

Tunakoelekea hata wao watachoka, wataona bora walinde familia zao kuliko kulinda watanzani sisi ambao hatuna msaada kwao ili hali wapo kwa ajili yetu kutetea:

•Haki zetu
•Maisha yetu
•Kazi zetu
•Biashara zetu n.k n.k

Tunakoelekea kama taifa tusipoungana nao kulinda: •KATIBA YETU
•UHURU WETU n.k n.k

~kuna siku watu watajimilikisha maliasili za nchi hii tutashindwa cha kuwafanya kama wale wa huko walivyojimilisha mgodi.

~Kuna siku watauwawa na kupotezwa familia zetu kabisaa tutashindwa cha kuwafanya kwa sababu tuliwaachia akina LEMA, MBOWE, MDEE, HECHE, ZITTO n.k waongee, wapiganie haki zetu. Sisi tukikaa kimya.

LEO WAO BADO WANAPUMZI, KESHO PUMZI ZAO ZITAKATA, WATAKAA KIMYA. TUTAGUSWA FAMILIA ZETU, WAUME/WAKE ZETU. NDIPO AKILI ITAKAA SAWA NA KUKUMBUKA HARAKATI ZA AKINA:

Zitto kabwe
GODBLESS lema
Halima Mdee
Marie sarungi
Fatma karume
freeman mbowe
Maxence Melo
jebra kambole n.k n.k


*Leo tunafurahia ama tunakaa kimya kwa miswada ya ajabu inayobadilishwa huko mhimili fulani.

*Leo tunakaa kimya kwa matamko yanayoonyesha katiba yetu kuvunjwa wazi wazi

*Leo watu wanapigwa risasi, wanawekwa rumande mda mrefu bila kufikishwa mahakamani, tumekaa kimya tunawasubiri akina kigogo sijui, akina zitto, akina lema, msigwa, mdee, fatma waongee eti kwa kuhofia tukiongea tutakufa, tutafungwa kesho hawatakokuwepo hao, mme/mke/ndugu yako wa karibu atafanyiwa mabaya sana. Nani atakutetea?!!

*Leo nasikia wanamkakati wa kuongeza zaidi ya 10 eheee...sisi tupo tu mtaani yaani as if maisha tumeyapatia kweli kweli, uoga unafki umetujaa mioyoni na midomoni kwetu yaaani as if tumeshiba hela zetu kumbe:

✓Makazini hakuna ongezeko lolote la mishahara.
✓Mishahara inapigwa makodi mpaka unashangaa
✓Mpaka leo hujaajiriwa na ajira hakuna
✓Umelima mazao yako unasubiria kupangiwa bei
✓Biashara ina makodi mpaka huoni faida.
✓Tuna madeni mpaka mpaka huzuni

Lakini mitaani tumekaa kusema HAKUNA KAMA YULE, AMELETA MAENDELEO. Tunasahau kujiuliza binafsi tumetosheka na maisha haya. Zile barabara zilizojengwa mwakaubungo, zinanisaidia nini mimi wa huku inyonga katavi, au jamaa wangu kule majimoto au bunamu yangu pale mvomero kaka yanhu hapo isongole ileje, au sister wangu kule endala karatu.

Akina TL wamepigwa risasi kwa ajili ya kutetea HAKI zetu, Maendeleo yetu. Sisi tumekaa kimya tunafurahia wao kuumizwa, kupigwa risasi...Dah HIVI NINANI ALIYETUROGA?????!!!

Nakumbuka yule "ngema" aliyeko alishawahi kusema mimi nimejitoa sana kuwapigania ila nasikitika badala ya kuniunga mkono kwa vitendo, mmebaki kunishangilia na kunisifia huku matatizo yenu yamebaki pale pale.

NIWAAMBIE TU WATIZEDI WENZANGU, TUNAKOELEKEA NIKUBAYA SANA KULIKO TULIKOTOKEA, LAKINI SISI TUNAFURAHIA MAROAD, MABRIDGE, MAVIVUKO N.K N.K Lakini kuna maelfu ya watu wapo gerezani miaka na miaka kwa sababu eti upelelezi haujakamilika.

Kuna watu wamepoteza Baba zao, waume zao watoto zao n.k kwa sababu ya kupigania haki.

Leo CHADEMA BADO WANANGUVU,KESHO NAO WATACHOKA, WAKICHOKA UKAGUSWA WEWE NA FAMILIA YAKO NDIPO UTAELEWA NINI NIMEONGEA.

Asomaye na Aelewe. Alitunze akili huku akimwomba Mungu ampe miaka mingi ya kuja kushuhudia haya mbeleni nini hiki nilichokiandika.

Nawatakia siku njema.




=========================================
NIMERUDI TENA, TUSICHOKE KUAMBIANA UKWELI
=========================================



Nashukuru sana kwa wale walionielewa nini nimeandika.. Kuna Msemo alishawahi kuongea LEMA kuwa namkuu "wakimaliza kwetu wataamia kwenu". Kama leo mmachinga anapewa kitambulisho kwa Tshs.10,000/- kwa mwaka wakati mtaji wake ni 5,000/- unategemea nini?! kwa rasilimali tulizonazo tulipaswa kuwawezesha wamachinga na kuwatengenezea miondo mbinu ya kufanyia biashara ili wakue then walipe kodi.



Kama leo wakulima kule mtwara wanauzia mazao ya kwa mhimili badala ya kuuza mazao yao moja kwa moja kwa wanunuzi.Na bado wanapangiwa bei Kesho yao itakuwaje?


Kama leo vijana wenzangu mnaotukuza usiku na mchana kwamba mtu fulani oyeee, nani kama mtu fulani. Wakati huna ajira mwaka wa tano huu, na bado Bodi ya mkopo inakusubiria uanze kulipa mikopo, isitoshe Mama na Baba yako au wadogo zako wana maisha magumu sana kule kijiji cha ikumbilo walaya ya ileje. Wanategemea mazao waliyolima ndo wale, yaani msosi wao ni ugali na kande au viazi vitamu wamebadilisha sana wali napo wakila wali ni sikukuu kweli kweli. Wewe umekaa mjini dsm unasema oyeeeeeeee kisa unaona maroad, na maflaiova ya ubungo. Unaishi kwa kuunga unga tu...Leo wamekupa 7,000 kawatukane akina mbowe twitter unaenda. Kesho yako hujui itakuwaje.

Kama leo ukienda vijijini kuna baadhi ya wazee unawakuta wamevaa kofia za mh. wa nchi zimeandika hapa ni mbombo tu. Lakini ukiangalia maisha yao bado wanachota maji kwenye madimbwi, mazao yao yanaozea ndani kwa kukosa soko. Hata ng'ombe/mbuzi/kuku walizonazo wakitaka kuuza wanalanguliwa bei mpaka aibu.am talking about mangula huko kilombero kwa jamaa yule kijana mwenzangu aliyeahamia huko kijani.


Leo unamkuta mama anaenda umbali mrefu kuchota maji, kupata clinic akisubiri mwezi wa nane aletewe kanga ya kijani na kitambaa kujifunika kichwani. Kesho yake amesahau kuwa hajapewa huduma mhimu na hao wanamkejeli kwa kumpa vitu vidogo vidogo.


Leo mdogo wangu wa shule kapata mimba. Kesho anakatazwa kurudi shule kwa matamko tu, na watanzania tumekaa kimya kwa kusubiri mnyika, mbowe na lema waombe mwongozo ama kwa kusubiri maria sarungi na fatma waanzishe hashtag twitter. Sisi waanga tupo kimya tunasubiria hao watusemee...

Jifikirie kuwa wewe ni Mke wa Azory gwanda, unavaaje kiatu chake hujamwona Mmeo kwa miaka sasa na hakuna jibu lolote toka kwa uliowapa kura yako kuwa watakulinda na kuilinda katiba????


Fikiria wewe ni mke wa saa nane, mpaka leo hujui mmeo yuko wapi amekufa ama amefungwa anajisikiaje huko aliko. Na je kama alipotea serikali inampa mjane fungu lolote wakati ikiendelea na kumtafuta??!!!!


Vaa kiatu cha tundu lisu pamoja na Mungu kumwokoa dhidi ya shambulio lile. Lakini mpaka leo hakuna aliyekamatwa zaidi sana bado hata yeye mwenyewe mpaka sasa 'ni kama' anaogopa kurudi kwenye ardhi aliyozaliwa, ardhi yenye AMANI na UTULIVU ambao Baba wataifa alitumia nguvu nyingi na akili kuifanya iwe hapo ilipokuwa.



Vaa kiatu cha mbowe mda huu!!!

Tujiulize yafuatayo:
✓Amefanya kosa gani mpaka yamkute hayo
✓Lengo lao hasa ninini kumfanyia hivyo
✓Je kuongoza chadema ni kosa?!!?
✓Kuikosoa serikali ni kosa?!!!, Kama ni kosa kwanini asikamatwe afunguliwe mashtaka rather unakwenda kumvunja miguu, halafu unasikia sauti za baadhi ya waheshimiwa kwenye mhimili ndani kule wakiwa na viongozi wakubwa tu wa nchi ileeee hiii wakitoa maneno mazito yenye kejeli, kebehi na uzandiki. yaani hata siku toka afanyiwe tukio hilo haijaisha?!?

Fikiria kuhusu Maxence Melo ambaye amkuwa na kesi ya mda mrefu kwa sababu ya kutetea uhuru wa kutoa maoni. Aliteseka kwa ajili yangu na wewe, na watanzania kwa ujumla, angeweza kufanya majukumu yake mengine nje ya haya. angeweza kuunga juhudi na akapewa hela ndefu ili awatangaze, lakini mpaka naandika uzi huu sidhani wala sijaona dalili hizo... Kesho wanaweza mtingisha zaidi na kupelekea either jf ifungwe (Nadharia tu) NA SIOMBEI.

JE, tutapeleka wapi hoja zetu?!!! kama leo tutawaacha hawa wanaharakati watutetee bila kuwaunga mkono?!!! tukumbuke kuwa yanayotokea kwa jirani leo, kesho yatakuja kwangu na familia yangu, tusipoweka tabia ya kusaidiana..kesho yakija kwangu sitapata pia msaada.


SASA HAYO YOOOTE NILIYOYAELEZA HAPO JUU, NDIYO UMHIMU WA KUWA NA WATU WACHACHE WATAKAOTUSEMEA, NA KUTULINDA DHIDI YA UVUNJWAJI WA KATIBA YETU.

Sasa tusipowalinda hao, iko siku watesi wetu watakuja kwetu moja kwa moja....na wameshaanza taratibu wanakuja kutugusa kila mmoja kwenye familia yake....ni mpaka watuguse soooooote ndipo tukumbuke chadema na kusema bora chadema wangekuwepo wangetutetea kwa niaba....



TUSICHOKE KUAMBIANA UKWELI, TUKUMBUSHANE KWANI KAMA HAYATATUKUTA SISI, YATAWAKUTA WATOTO WETU, KAMA SI WATOTO WETU KIZAZI CHETU KITAATHIRIKA KWA HAYA YANAYOENDELEA KUTENDEKA LEO.

Tusijisahau


Ahsanteni sana wanajamiiforum
 
Usifikiri kwmba watanzania hawataki upinzani, no.

Watanzania wanataka upinzani imara, ambao hata ccm ikiboronga tunaiweka pembeni tuna weka mwingine, nae siku akiboronga tunamuweka pembeni tunamrudisha ccm.

Sasa siyo hawa upinzani njaa
 
Wapinzani wote wanakumbukwa na wataendelea kukumbukwa! Kuanzia NCCR ya Mrema mpaka CUF ya Lipumba miaka ya 2000 to 2005 ya haki sawa.
 
Kuna Wapuuzi watakuja sasa hivi kutukana
Wakaribie tu, ila nimesema ya moyoni. sidhani kama nimekosea. Iko siku chadema na upinzani mwingine watachoka, wataacha. Tutaguswa kila mtu na familia yake ndipo tutawakumbuka. Kitu ninachoamini hakuna aliyeko KIJANI yupo kwa ajili ya watanzania. Mienendo yao inawatambulisha wazi wazi. Nitajie mmoja wao nikupe details zake.
 
Hii kitu ndio habari ya mjini, hadi bei imeongezekaView attachment 1474214
Yote ni mema, sikuja kumtetea mbowe. Nilikuja kuandika uzi huu ili wewe ujiulize mbali na ushabiki wako kwao. Je familia/ukoo wako uko salama kiuchumi, kiafya n.k? au wewe tu uko vizuri wengineo watajijua? Sasa wapo watu wangeweza kufanya biashara zao ama kuuunga jitihada, siku hao watu wataacha kututetea hapo ndipo ule mwisho wetu utakapokaribia.


Hivyo yote ni mema kwa sasa, kesho yetu hatuijui japokuwa tunaona yanayoendelea sasa ila hatuna reflection ya kesho.
 
Usifikiri kwmba watanzania hawataki upinzani, no.

Watanzania wanataka upinzani imara, ambao hata ccm ikiboronga tunaiweka pembeni tuna weka mwingine, nae siku akiboronga tunamuweka pembeni tunamrudisha ccm.

Sasa siyo hawa upinzani njaa
Ni suala la muda tu
 
Upo sahihi sema wapo wanao ona mambo flani kwa urefu wa Pua zao, hao ndio wata sumbua hapa .
 
Baba wa taifa anasema dhambi ya ubaguzi uwa haifiki mwisho mtaanza uyu ni chadema wakiisha mtaenda uyu sio kanda ya ziwa mtaenda uyu sio msukuma mtaenda uyu sio wa chato mtaenda uyu sio wa familia.

Utafikia muda ajira unakuta wamepangana tu mkuu wa majeshi mtoto, TISS Mtoto wa dada au shangazi. Mke waziri au Makamu wa Rais

Kama ameweza kuweka ndugu zake kwa kipindi cha miaka 5 kama alivyofanya kwa Dotto.itakuwaje baada ya miaka 15? kama ataongeza muda?
 
Wakaribie tu, ila nimesema ya moyoni. sidhani kama nimekosea. Iko siku chadema na upinzani mwingine watachoka, wataacha. Tutaguswa kila mtu na familia yake ndipo tutawakumbuka. Kitu ninachoamini hakuna aliyeko KIJANI yupo kwa ajili ya watanzania. Mienendo yao inawatambulisha wazi wazi. Nitajie mmoja wao nikupe details zake.
si kijani wala huko kwingine, wote wapo kwa ajili ya matumbo yao. sasa hivi bei ya mafuta ni chini ya sh 1,600 kwa lita, fuatilia ujue wabunge wanajilipa sh ngapi kwa lita kama posho ya mafuta halafu uje utueleze kiongozi mmoja wa huko kwingine ambaye amewahi kukemea hili.

wote wanatembelea kwenye mgongo wa ujinga wetu.
 
Usifikiri kwmba watanzania hawataki upinzani, no.

Watanzania wanataka upinzani imara, ambao hata ccm ikiboronga tunaiweka pembeni tuna weka mwingine, nae siku akiboronga tunamuweka pembeni tunamrudisha ccm.

Sasa siyo hawa upinzani njaa
Bila shaka unataka upinzani utoke mbinguni? yaani uje na pesa ukugawie, uje na katiba mpya, uje na ugali wakusongee wakulishe wakuoshee vyombo umelala tu hakuna upinzani wa hivyo hata marekani.
 
Usifikiri kwmba watanzania hawataki upinzani, no.

Watanzania wanataka upinzani imara, ambao hata ccm ikiboronga tunaiweka pembeni tuna weka mwingine, nae siku akiboronga tunamuweka pembeni tunamrudisha ccm.

Sasa siyo hawa upinzani njaa
Sioni CCM ikiruhusu hilo litokee, sana sana mwenyekiti wa CCM ndo atakuwa mwenyeviti wa vyama vyote vya siasa.
 
✓Makazini hakuna ongezeko lolote la mishahara.
✓Mishahara inapigwa makodi mpaka unashangaa
✓Mpaka leo hujaajiriwa na ajira hakuna
emoji23.png

✓Umelima mazao yako unasubiria kupangiwa bei
✓Biashara ina makodi mpaka huoni faida.
✓Tuna madeni mpaka mpaka huzuni
Watanzania wameridhika na maisha mabovu waliyo nayo
 
Back
Top Bottom