Watanzania wanakataa Mchele lakini wanakubali Kondomu, Chanjo na Dawa za Mmarekani

Ni hofu tu, huo mchele tungeula tu wala hauna madhara ya kuhofiwa. Mamlaka za kupima ubora wa vya vyakula zipo zingepima tu
 
Waziri husika, anasema ameagiza badala ya kuletewa kutoka Marekani, wawekeze kwenye mpunga wa Tanzania ili kupata mchele bora... ama watupe fedha tuwekeze wenyewe
 
Hili nalo ni moja ya Ajabu la Dunia kutoka Tanzania.

Inaonekana hata hujui watu wanacho biashania;
Hakuna hata mtu mmoja anayekataa mchelele wa marekani, wanachodai Watanzania wenye MAARIFA ni kuwa, Tanzania tuna mchele wa kutosha kabisa kwa msimu huu, kama wanataka kutusaidia wangeleta fedha tununue huku kwa wakulima walio nao mwingi usambazwe kwa wengine kwa bei nafuu kabisa au basi watusaidie kwenye nyanja ambazo tuna mahitaji makubwa ya saiyansi na technologia au miundombinu.
Hata hivyo tusiwalaumu Wamarekani hasa baada ya kuambiwa ni mwenzetu (NGO) alienda kuwaomba mchele...
 
Tatizo sio misaada tatizo kupewa msaada kwa kile tunachoweza kuzalisha kwa wingi na kikabaki. Hatuna uwezo wa kuzalisha ndom,chanjo,dawa ila kilimo kimo ndani ya uwezo wetu tusibweteke kisa tunapewaga misaada ya dawa na chanjo
 
Hili nalo ni moja ya Ajabu la Dunia kutoka Tanzania.
Baadhi ya watanzania usipo wafahamu vizuri utazani wanachukia mchele wa bule

Au atadhani wanauchukia ccm kumbe waongo wakubwa chuki yao iko kwa yule alie agiza mchele hule tu
 
Back
Top Bottom