Watanzania tunapowasifia Kenya kwa Demokrasia pevu, pia tutafakari na hili

voicer

JF-Expert Member
Jul 13, 2020
5,553
11,885
Wakati Huku TZ tukiwasifia kwa Demokrasia pevu wakenya, pia tutafakari na hii:

41Bilions K/shs,+ 4.1bilions K/shs,+700 milionsK/shs,+ 851 millions, K/shs.+800millions, K/shs!

Ebu jumlisha hizo pesa, kisha Convert hizo pesa kuja Tanzania Shillings, halafu unaambiwa ni ukwasi wa watu waliowahi kuhudumu katika serikali.

Nimetafakari sana kusikia kwamba Ukwasi walioutaja leo ambapo wamehojiwa Mawaziri watatu pekee.

Kwanza nianze na Rais Ruto pekee ambaye yuko kwenye orodha ya matajiri kumi wa Kenya akiwa na ukwasi wa 41 billions Kenya shillings.

Halafu makamu wake Richard Gachagua yeye anao ukwasi wa 800millios, Kenya shillings, pamoja na zile 200 millions Kenya shillings ambazo zilikuwa zimetaifishwa na serikali anafikisha jumla ya ukwasi wa 1 bilion, Kenya shillings.

Leo hii Musalia Mudavadi ambae ni waziri mkuu mteule, Ametaja kuwa ukwasi wake ni 4.1bilions Kenya shillings.

Kuna mwanasheria mkuu mteule Justin Muturi ambae amesema ana ukwasi wa 700 millions, Kenya shillings.

Mwingine aliefika leo mbele ya kamati hiyo ni Waziri wa Ulinzi mteule Hassan Dualle ambaye ametaja ukwasi wake kuwa ni 851 millions, Kenya shillings.

Hao ni kwa uchache, lakini orodha ni ndefu na pia ukwasi ni mkubwa sana!
Kesho orodha itaendelea kwenye kamati hiyo.

MY Take: Ni kwa namna gani hawa watu ambao miaka michache tu iliyopita waliingia serikalini kuhudumu kama watumishi wa umma. Wameweza kujikusanyia ukwasi wote huo?

Walau Rutto tunajua alineemeka pale Rais Moi,alipomlazimusha kuacha masomo yake chuo kikuu Nairobi na akamteua kuongoza YK92, ambapo alipewa jukumu la kuhakikisha anawalainisha wapinzani wote wa Moi, ili kumuunga mkono katika uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi nchini humo.

Ni hapo ambapo alijinufaisha na mamilioni yaliyotolewa na Moi ili kuwahonga wapinzani wake.

Sasa kwenye uchaguzi uliopita!
Rutto aliweza kuwaaminisha walalahoi wa Kenya kuwa anatetea hustlers wa Kenya akijinasibu na lile toroli.

Lakini ukweli ni kwamba uchaguzi ule ulikuwa ni upinzani kati ya kambi mbili ambazo ni:

Ile ya watoto wa wanasiasa wenye majina katika historia ya Kenya kina Uhuru Kenyatta, Gideon Moi, Raila Odinga na wenzao wengine
Dhidi ya kundi la waliowahi kuwa watumishi wa umma na kujitajirisha kupitia ufisadi mbalimbali, kulingana na nafasi walizowahi kuhudumu hapo awali, wakiongozwa na William Samoei Ruto, Musalia Mudavadi na Richard Gachagua na wenzao.

Kwa ukwasi huo hapo juu ni wazi kwamba wakenya wameruka matope na kukanyaga maji.

"Mwanasiasa akikwambia usiku umeingia, huku mkiwa ndani, vema utoke nje ukajiridhishe mwenyewe"

Alamsikhi
View attachment 2390694
 
Bora Wakenya wanasema utajiri wa viongozi na kuweka wazi. Hawa wa Tanzania nani anajua wana ukwasi wa kiwango gani? Kwa vile wapo kimya ndiyo unadhani siyo mafisadi? Siku wakitaja utajiri wao si utazimia... Fikiria tena mara 2...
Nielewe vizuri hoja yangu hapo mkuu.
Hakuna mahali nimeandika kwamba Tanzania hakuna mafisadi.
Ninajua wapo na iko siku nitaeeka topic hiyo humu.

Mimi hoja yangu kubwa ni kuonyesha jinsi watu tunaowaita "State Capture" wanavyojipanga,na hatimae kumlaghai maskini mpiga kula kwa Slogan ya Mhangaikaji "Hustler" au tuseme kabwela.

Wakati sio kweli bali anawarudishia kilekile alichowapora awali.

Nimejaribu kusema kwamba hapo hakuna Hustler bali mataikuni watupu.
Na mkenya aendelee kujiandaa kukamuliwa upya.
 
Hata sisi kama tungeweka misingi sawa tukaacha kuiba kodi za raia tukaanzisha viwanda kama Kenya na private sekta ikafanya vizuri what is a problem mtu kuwa na hizo change?
Yaani mtu kuwa na 800M ndiyo ukwasi? Nakuhakikishia kama siyo huu ukiritimba watanzania wengi sana wanaweza kuwa na hata zaidi ya hizo tena bila kuwaibia raia kodi zao
 
Watanzania wengi ambao hawajui ku create wealth wanadhani mtu akiwa hana ukwasi ndiyo anayefaa kuongoza, yet the vice versus is true...Mtu yeyote ambaye hawezi ku create wealth atasaidiaje nchi? You cannot give what you do not have...Ili uwe wa msaada anza kuonyesha katika ngazi ya familia yako kwanza ndipo uje kwenye public bila kuwa na access na public funds...Hii inawezekana tu kwa wale ambao wana patience ya ku grow with their carrier kila hatua akiongeza welfare yake na ya jamii inayomzunguka pasipo kui nyonya...

Wengi ni ma opportunists wasiojua kuzalisha zaidi ya kutumia na ndiyo sababu wanaishia kudokoa hazina na kuifilisi badala ya kuzalisha goods and services ili hazina ikijaa na wao iwe halali kutumia...mtu kuwa mwema au kiongozi bora siyo yule ambaye hana access akawa hana kitu, bali yule ambaye pamoja na access akaweza kuiongeza ukubwa wa hiyo hazina bila kutumia njia za panya kudokoa ambacho hajakizalisha huku akijua kukusanya kwakutumia nguvu ya sheria ama dola, kuwakamua ambao wala hajawawezesha kuzalisha...Wamejaa kila mahalili watu wa hivyo na wazuri kweli kwenye kujipendekeza na kujifanya kama vile ni watii kumbe ni mbwa mwitu kwenye ngozi ya kondoo, hawaoni huruma kusotesha watu wasio na uwezo kwa michango yao bila kujali kama inawafaidisha raia au la, zaidi ya wao kujigawia mapande makubwa na kutumia kwa anasa.. ..Hawa hawana tofauti na wanaotumia mitutu kuvunja ma banks, tofauti ni njia wanazotumia, moja ipo justified nyingine ipo demonized but are the same type of the people...
 
Acha kelele, Kenya ina uchumi mkubwa na tajiri zaidi kuliko Tanzania.
Nielewe vizuri hoja yangu hapo mkuu.
Hakuna mahali nimeandika kwamba Tanzania hakuna mafisadi.
Ninajua wapo na iko siku nitaeeka topic hiyo humu.

Mimi hoja yangu kubwa ni kuonyesha jinsi watu tunaowaita "State Capture" wanavyojipanga,na hatimae kumlaghai maskini mpiga kula kwa Slogan ya Mhangaikaji "Hustler" au tuseme kabwela.

Wakati sio kweli bali anawarudishia kilekile alichowapora awali.

Nimejaribu kusema kwamba hapo hakuna Hustler bali mataikuni watupu.
Na mkenya aendelee kujiandaa kukamuliwa upya.
 
Mbaya zaidi kwenye serikali yake sioni Kabwela na Mama Mboga.

Aliwaaminisha na wao wakajaa wazima wazima ,majuzi anawaambia ile pesa ya makabwela itatoka kwa masharti.

Hakuna Pesa ya bure, ukipewa lazima urudishe tena kwa riba nafuu ni siasa nyingi tu.

Wapo gizani kama wa huku kwetu wakishapewa T -Shirt na Kofia nao pia wanajaa wazima wazima .

Miaka 5 shida zinawachapa mpaka basi.
 
Ukumbuke tu Kenya ni mabepari, kila mtu anaruhusiwa kuchuma utajiri jinsi anavyoweza ndani ya sheria zao, kama ni mafisadi mbona hawapelekwi mahakamani?
Umasikini siyo sifa, ila haifai kuchukua mali ambayo hujaizalisha...
Kuwa na mlengo wa kibepari sio sababu ya kukwapua mali za jasho la walipa kodi na kujilimbikizia,hapo unabadilika na kuwa Bwanyenye.

Pia kuhusu kutokamatwa kwao au kishitakiwa ni kwamba woote hao wameshinda uchaguzi huko,lakini wanazo kesi mahakamani wakiwa watuhumiwa.

Tena mfano ni Malamu Rais Gachagua ambaye ana kesi mbili na pia 200m zake zilitaishwa na serikali kwenye moja ya hukumu za mahakama.

Ndio maana unaona walichokifanya hata kabla ya kuteua baraza la mawaziri.
Rutto amewafutia kesi wote ambao wako mahakamani.
Kina Aisha Jumwa,Richard Gachagua na wengine wengi humo "UDA".
Na hivi tunavyoandika humu tayari kenya law society wameisha weka Petition mahakamani na kesi ya kupinga hilo jambo,iko kwenye maandalizi mahakamani kenya.

Fuatilia......
 
Hata sisi kama tungeweka misingi sawa tukaacha kuiba kodi za raia tukaanzisha viwanda kama Kenya na private sekta ikafanya vizuri what is a problem mtu kuwa na hizo change?
Yaani mtu kuwa na 800M ndiyo ukwasi? Nakuhakikishia kama siyo huu ukiritimba watanzania wengi sana wanaweza kuwa na hata zaidi ya hizo tena bila kuwaibia raia kodi zao
Hiyo 800 sio madafu ya kitanzania brother.

Ni kenya shilings.....

Kwa Tanzania hiyo ni sawa na 16 B.
 
Ubaya moja wa Kenya ni kutumia nafasi hizo kufanikisha connections zao, typical of African countries...
Na hiyo ndio hasa nilichokilenga mimi.

Pia ubaya mwingine ni pale wanapo fanya "Brainwash" kwa wapiga kura na kujiita "hustlers "wakati ni waizi na mabepari watupu.

Hizo brain wash ndio CCM pia wanazifanya kwa kujiita chama cha kutetea "wanyonge" kumbe "kinawanyomga"
 
Tatizo lako mleta mada unasumbuliwa na akili za kimaskini

Masikini au mtu asiyejua namna ya kutengeneza hela na utajiri hawezi kukufanya wewe au nchi yako kuwa tajiri au kuwa na maendeleo.

Hizo akili za kipumbavu ndo zinafanya Tanzania kuwa maskini hadi leo. Kenya wanafanya mataifa mengi duniani kwa sasa yanafanya. Kuwapa matajiri uongozi. Maana mtu mwenye akili za kitajiri na kutafuta pesa hawezi kuweka sera za kimaskini katika kuendesha nchi
 
Maana ya hustler ni mtu aliyekomaa kutoka chini kwenye umaskini hadi kuwa tajiri. Ni muhangaikaji aliyepata kutokana na kuhangaika kwake. Sasa Ruto anatumia hii slogan kuwa motivate wakenya kuwa hajapata utajiri kwa kurithi kama Uhuru na Odinga ila ameuhangaikia.

So usipotoshe. Kama huelewi uliza
 
Mbaya zaidi kwenye serikali yake sioni Kabwela na Mama Mboga.

Aliwaaminisha na wao wakajaa wazima wazima ,majuzi anawaambia ile pesa ya makabwela itatoka kwa masharti.

Hakuna Pesa ya bure, ukipewa lazima urudishe tena kwa riba nafuu ni siasa nyingi tu.

Wapo gizani kama wa huku kwetu wakishapewa T -Shirt na Kofia nao pia wanajaa wazima wazima .

Miaka 5 shida zinawachapa mpaka basi.
@Mkendo!
Uko sahihi mkuu 100% true.hicho ndio kinaendelea hapa Tanzania.

Aheri wakenya wanathubutu kusema hadharani kuliko haya majizi ya huku kwetu.ambayo yanaiba na kuficha huko nje ya nchi.

Kisha ikitokea akaunti zikafungwa na intepol....wanaishia kufa ghafla kwa presha huku Tanzania.!

Kuhusu kuwarubuni watanzania pia ni kweli kabisa.walau kule kenya Rutto alikuwa akitembea na gari ya hela na kupenyeza rupia kweye aliona pana kadhia.

Wa kwetu wao wanahonwa pilau,t-shirt,kofia na pesa kiduchu za kujikimu wanapopandishwa malori kwenda kushangilia ujinga majukwaani.
 
Tatizo lako mleta mada unasumbuliwa na akili za kimaskini

Masikini au mtu asiyejua namna ya kutengeneza hela na utajiri hawezi kukufanya wewe au nchi yako kuwa tajiri au kuwa na maendeleo.

Hizo akili za kipumbavu ndo zinafanya Tanzania kuwa maskini hadi leo. Kenya wanafanya mataifa mengi duniani kwa sasa yanafanya. Kuwapa matajiri uongozi. Maana mtu mwenye akili za kitajiri na kutafuta pesa hawezi kuweka sera za kimaskini katika kuendesha nchi
Tatizo sio utajiri mkuu!
Tatizo ni umeupataje huo utajiri.

Wewe ni aina ya majizi wengi waliojificha kwenye siasa barani Afrika na kuifanya Africa nzima kuendelea kuwa ombaomba huku ikiacha maiasili zake kukombwa na wazungu,kwa msaada wa viongozi majizi waliotapakaa kila kona ya bara hili.

Tunaposema matajiri lazima uonyeshe chanzo cha utajiri,na ndivyo inavyofanyika huko kwenye nchi zilizoendelea.

Matajiri tukimaanisha mtu kama Bakhressa akiamua kuingia kwenye siasa hapo atatambulika kama tajiri aliyeingia kwenye siasa.

Sio hao unaotaka kujinasibu wewe,huku ukiwa huijui hata historia yao.
Kilichowapata wakenya ni..

"wamekaangwa kwa mafuta yao wenyewe"
 
Back
Top Bottom