Watanzania tunamuhitaji Musa kutupeleka nchi ya ahadi



Katikati ya Afrika ya Zamani na Afrika Mpya kuna daraja la mauti. Watu wa Afrika hawana budi kufa ili kuzaliwa upya katika nuru na 'mwongozo mpya' kutoka ndani na ndani ya nafsi zao na ili kumalizana na ulimwengu hadaa wa leo wa ufikirifu pofu wa kimakundi. Sehemu ya jitihada ya kushiriki haya yote ni katika kule kuchochea mawezekano ya fikra za mtu mmoja mmoja katika kule kujaribu kunasua mtu na ukundiko wake wa kiimani ama dini--hakuna jinsi, kila mtu hana budi kubeba mzigo wake katika wakati hu muhimu. Yeyote anayeona 'hajiwezi' ila kubakia na makundi yake ya usadikifu hata kwa mambo ambayo ingelimpasa sana kujimulika mwangaza--kwake huyo hakuna jinsi ila Wakati kuwa muamuzi wa mavuno ya ustahili wa wale wenye kufaulu kujinasibu katika kule kuzaliwa upya ajili ya fahari mpya.


Ni mtu mmoja mmoja aliyejikwamua kiakili ataungana na mwenzake katika shauri lenye kheri zaidi na kuzaa ushirika na taasisi zenye Nguvu Mpya, Ari Mpya na Hadhi Mpya. Mtu wa zamani ni kimeo taslim na wala hata nusa wala kuonja harafu ya marashi ya ustawi mpya wenye mawezekano; lake itakuwa ni kusakamwa na maradhi na kule kutokomea katika migogoro isiyo na suluhu na pia maangamizi ya taasisi na mifumo isiyofaa tena.


huuuu...hoi
Kipengele hicho hapo juu ndio nilichokielewa zaidi, kwa kuwa haya ni maono yako nafikiri itanichukua mda mrefu kidogo kuona kwa macho yako. Nategemea kujifunza kutoka kwako kwasababu siwezi kukataa wala kukubali kitu nisichokielewa, nakuomba utumie lugha nyepesi kwa siku zijazo.
 
​Wengi wetu nataraji tutakuwa waumini wa dini na bila kuzitaja dini hizo naamini asilimia kubwa ya sisi waumini tumeshasikia hadithi za Musa/Moses. Katika hadithi hizi sehemu kubwa inaelezea safari ya kuwatoa utumwani Waisraeli(Tanzania) na kuwaongoza katika nchi ya ahadi(Tanzania yenye Ustawi).

Kuna mambo mengi sana ya kujifunza katika safari hiyo ya kuelekea nchi ya ahadi, nitaorodhesha machache hapa chini.
1. Haikuwa rahisi kutoka kwenye mikono ya Farao (Mafisadi papa na Nyangumi)
Japokuwa Mungu aliwaadhibu Wamisri (SISIEM) kwa mapigo kadhaa watu hawa hawakukubali kirahisi kuwaachia watumwa wao(Watanzania), hii inaonesha ni kiasi gani Farao(Viongozi wa Magamba) alinogewa na kula vya bure kiasi cha kuvumilia mapigo na hata alipowaruhusu alituma majeshi yake kuwafuatilia.

2. Manung’uniko ya Waisraeli safarini (Manughuniko ya Wa Tz)
Japo watu hawa walifahamu kuwa wanaenda kwenye nchi ya ahadi(Japo watanzania wanafahamu nchi inaweza kupata mafanikio), nchi yenye neema za kila aina na hawatakuwa watumwa bali wenye nchi lawama na manung’uniko yalikuwa hayaishi. Kitu cha kusikitisha ni kwamba ilifika wakati wapo waliosema ni bora wangelikuwa Misri(i.e Wa TZ wanalalamika sana na kwa ujinga inafikia wanasema bora tueendelee kuongoza na SISIEM) utumwani kuliko mateso wanayoyapata huko jangwani.

3. Musa hakufika katika nchi ya ahadi
Safari ambayo Musa aliwaongoza Waisraeli iliyojaa changamoto( Maisha kuwa magumu,Bei ya umeme kupanda mara dufu,Bei za vyakula kupanda,Mfumuko wa bei,Elimu mbovu,Ufisadi kupindukia,Uizi wa mali ya uma,Ubabe wa kijinga,Uminyaji wa demokrasia,Kuua raia wasio na hatia!) za kila aina toka kwa adui na watu aliowaongoza, kwa kiongozi huyo iliishia mpakani na aliishia kuiona kwa mbali tu. Kazi kubwa ilifanywa na Musa lakina Yoshua ndio aliyeimalizia na kuwavusha mto jordan kuingia nchi ya ahadi.

Nimejitahidi kuelezea kwa kifupi bila kuingia kwa kina sana ili kujenga tu taswira ya ninachotaka kukielezea.

Watanzania ili tufike nchi ya ahadi tunahitaji tumpate Musa wa kutuongoza lakini aelewe yafuatayo.
1. Imani na uthubutu
Kama nilivyoelezea hapo juu kwenye namba moja, kazi ya kuwatoa Waisraeli Misri haikuwa rahisi vivyo hivyo kazi ya kuwatoa Watanzania walipo haitakuwa rahisi. Farao(wanao nufaika na hali duni yetu) hatokubali kirahisi kuachia watumwa wake, Musa anatakiwa aamini anaweza na athubutu kutuongoza.

2. Uvumilivu na hekima
Katika safari hii lazima Musa aelewe kwamba yeye ndio kiongozi na ndio mwenye maono lakini anaowaongoza wanaweza wasimuelewe wakati mwingine. Aelewa kwamba tunakoelekea ni kwenye neema na yupo tayari kuwaongoza watu wake katika nyakati za maatabiko akiamini tukifika mambo yatakuwa mazuri kwa kila mmoja.

3. Kujitoa mhanga
Sio rahisi kukubali kufanya yote aliyoyafanya Musa kama utatambua kuwa mwisho wa safari hutakuwepo kula mema ya nchi. Lazima Musa aelewe kwamba akienda kinyume au kwa sababu nyingine yoyote kuna uwezekano wa yeye kutofika. Baada ya kutambua hilo anatakiwa kuwaandaa kina Yoshua kupokea kijiti na kuhakikisha tunafika katika nchi ya ahadi.

Sijui safari hii itachukua miaka 40 au minne, sijui kama Musa ameshazaliwa, yupo kwenye kikapu kuepushwa na mauaji ya Farao, analelewa kwenye familia ya kifalme ya Farao au yupo mlima Sinai.

Nawasilisha,

KXY.

Kweli tunamhitaji musa!
 
Back
Top Bottom