Watanzania tunajiweka nyuma!

MAMMAMIA

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
3,811
1,604
Ulimwengu Umeamka!
Vijana Wameamka!
Wananchi wote Wameamka!
Hasa vijana ambao ndio wahanga wakubwa wa matatizo yanayosababshwa na wanasiasa ulimwenguni. Walianza vijana wa kiarabu, Misri na Tunisia kwa kile walichokiita "Arabic Spring" kwa sababu ndio majira waliposema BASI! Basi kwa Mubarak. Basi kwa Ben Ali. Waliteswa, waliuawa lakini hawakurudi nyuma. Badaye vijana wa Yemen, Libya, Syria wakaingia mitaani. Nchi nyengine kama Morroco, Algeria, Jordan baada ya kuona wimbi hili wakaamua kufanya marekebisho haraka.

Lakini Mapinduzi haya ya Dunia (ya Vijana) hayakuishia kwa Waarabu tu. Moto ulisambaa hadi Israel na nchi nyengine duniani: USA, Belgium, Spain, Chile n.k.Mote humo ni vijana ambao wanaandama na kukusanyika kwa njia za amani kutoa vilio vyao: Ubovu na ughali wa elimu, kukosa ajira, kutokuwa na hatima yoyote kwa sababu bado wanasiasa wanaimba "Vijana ndio taifa la kesho" wakati wao wanafaidika na taifa la leo.

Watanzania je, tumefanya nini? Vijana wa Chadema waliwahi kuingia mitaani, lakini chama tawala na vibaraka wao (vyama vyengine vya siasa vya upinzani na jumuiya za kidini) wakaanza kueneza sumu kuwa Chadema wanavunja amani. Ndugu zangu, wanaoumia si vijana wa CDM peke yao: Ni vijana wa Tanzania wote. Giza la kudumu, ukosefu wa elimu, huduma duni za afya, ukosefu wa ajira... havichagui wanachama. Sote tunaathirika. Sote ni wahanga wa maamuzi mabovu ya serikali, rushwa, wizi na ubadhirifu wa mali na rasilimali zetu. Vijana, msidanganywe, msirubuniwe, msitishwe. Wakati ni huu wa kuingia mitaani kwa njia ya amani kuwahamasisha wananchi na kuwaambia viongozi wanaojidai nchi hii ni yao kuwa TUMECHOKA! TUNATAKA MABADILIKO YA KIJAMII.

WITO KWA VIJANA:
Kesho kutakuwa na maandamo ulimwenguni kote (mpaka sasa zaidi ya nchi 80 zimethibitisha kushiriki) ya vijana kuandamana kwa amani kuonesha kukerwa kwao na mfumo wa kisiasa na kiuchumi wa dunia. Ni wakati mzuri kwa vijana wa Tanzania tukajipanga kuonesha kukerwa kwetu huko. Tujiandae. Tujitokeze
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom