Watanzania Tubadilike, Tujadili Maendeleo!

ZeMarcopolo

Platinum Member
May 11, 2008
14,017
7,220
Watanzania hatutumii muda wa kutosha kujadili maendeleo. Muda mwingi tunajadili mapenzi na kidogo siasa za ushabiki. Iwapo tutaendelea hivi, basi nchi yetu itaendelea kuogelea kwenye dimbwi la umasikini na kuyumbishwa na wanasiasa. Nimefanya survey ya makundi (groups) za Jamiiforums na idadi ya wana JF waliojiunga na makundi hayo (ona kiambatanisho chini). Matokeo ni kama ifuatavyo.
Asilimia 74.43 wamejiunga ni vikundi vya mapenzi
Asilimia 2.91 wamejiunga na kikundi cha IT
Asilimia 2.5 wamejiunga na kikundi cha CHADEMA
Asilimia 1.7 wamejiunga na kikundi cha "machalii"
Asilimia 1.12 wamejiunga na kikundi cha mazingira
Asilimia 0.56 wamejiunga kikundi cha elimu ya ushuru
Asilimia 0.112 wamejiunga na kikundi cha watu wa mahubiri ya Bwana Wetu Yesu Kristo
Asilimia 0.112 wamejiunga na kikundi cha ujasiriamali

SOFTWARE ENGINEERING COURSE
26 member(s)

Mapenzi ya dhati 362 member(s)

Mapenzi 302 member(s)

Matumizi Endelevu ya Maliasili 10 member(s)

Christ's Gospel People 1 member(s)

BIDII YETU ITAINGIZA CHADEMA MADARAKANI 22 member(s)

MACHALII YA ARA 15 member(s)

Marafiki wa JF 148 member(s)

TAX EXPERTSIM AND ACCOUNTS SOLUTIONS GROUP 5 member(s)

Small business and innovations 1 member(s)
 
Huku kwenye siasa ni matusi na ukada tu, cha mno kujitia makunyanzi usoni nini? Kule kwenye mapenzi hukuti matusi ni upendo tu. Bora uende kule ukafurahi kuliko huku. Hapa nilipo nimevimba na mihasira kuna mtu kaniita kilaza.
 
Maendeleo ni nini??

Misururu ya magari??

Wingi wa majengo makubwa Dar??

Kwa nini hakuna waliojiunga na CCM??

Nadhani tokana na hali ngumu ya kimaisha watu wamejiamulia kuingia katika makundi ya kimahaba kujiliwaza, hizi kodi tunazokatwa zingekuwa zinatumika vyema nadhani sasa watu wangeshajadii mipango ya kiserikali kuwaletea maendeleo!

Mikakati karibu yote tunayoletewa ya maendeleo kwa sasa si people centered imeamuriwa toka huko ambako bwana mkubwa hua anaenda kuomba msaada wakati amekalia kigoda cha dhahabu, msingi hapa ni kuondoa mfumo uliopo halafu mwngine yatafuata!

Mtazamo wa kisaikolojia unatafsiri maendeleo hivi;
Development describes the growth of humans throughout the lifespan, from conception to death. The scientific study of human development seeks to understand and explain how and why people change throughout life. This includes all aspects of human growth, including physical, emotional, intellectual, social, perceptual, and personality development.

Nadhani kiambatishi ulichoweka hapo juu kinaonesha namna watu walivyokata tamaa na hawawezi kujadili maendeleo kwa mtindo uliopo kwa sasa!
 
Watanzania sisi ni wabinafsi sana,wengi humu tayari wana maendeleo yao binafsi,so hawaoni umuhimu wa kujadili maendeleo ya nchi ambayo wao wanaona ni kama maendeleo ya watu wengine.

Hao ndo wale wenye kudhani kwamba maendeleo ya few individuals ndo maendeleo ya Taifa.Hawadhani kama umasikini wa wengine ni jambo lenye kuwahusu.

Ndo maana ni mapenzi na chit chat,sometimes siasa,lakini siasa ni za unazi,siku hizi mashindano,si ya kuwaletea wananchi wengi ambao ni masikini maendeleo,bali majungu,fitna na uongo,yani vurugu tupu.

Siasa nazo zimekuwa unazi badala ya kujadili how to move forward as a nation.

Tuna challeneges za kufa mtu,lakini "we are a joke"
 
Watanzania hatutumii muda wa kutosha kujadili maendeleo. Muda mwingi tunajadili mapenzi na kidogo siasa za ushabiki. Iwapo tutaendelea hivi, basi nchi yetu itaendelea kuogelea kwenye dimbwi la umasikini na kuyumbishwa na wanasiasa. Nimefanya survey ya makundi (groups) za Jamiiforums na idadi ya wana JF waliojiunga na makundi hayo (ona kiambatanisho chini). Matokeo ni kama ifuatavyo.
Asilimia 74.43 wamejiunga ni vikundi vya mapenzi
Asilimia 2.91 wamejiunga na kikundi cha IT
Asilimia 2.5 wamejiunga na kikundi cha CHADEMA
Asilimia 1.7 wamejiunga na kikundi cha "machalii"
Asilimia 1.12 wamejiunga na kikundi cha mazingira
Asilimia 0.56 wamejiunga kikundi cha elimu ya ushuru
Asilimia 0.112 wamejiunga na kikundi cha watu wa mahubiri ya Bwana Wetu Yesu Kristo
Asilimia 0.112 wamejiunga na kikundi cha ujasiriamali
Small business and innovations 1 member(s)

ZeMarcopolo, naona kuna mkanganyiko kwenye hoja yako. Nasema hivyo kwa sababu sijaelewa unahoji muda wanaotumia watu kwenye forum fulani au unahoji idadi ya waliojiunga? Niajuavyo mimi kujiunga na JF ni once, na baada ya hapo mtu anaweza kuchangia forum/sub-forum yoyote. Au unaamanisha idadi ya watu wanaotembelea forum/sub-forum moja at any given time?

Pili, kwenye muda. Ume-calculate vipi kujua kuwa watu wanatumia muda mwingi kwenye forum hii na sio ile? How did you monitor time spent for each forum ndio unatoka hiyo list?

Kwenye red: Hivyo vikundi vinapatikana wapi hapa JF? Sijaona forum ya machalii? iko wapi?
 
FJM, ni kweli amezungumzia kujiunga na makundi ambayo yamo humu.Lakini on the other hand,ni ukweli usiopingika kuwa watu chit chat, mapenzi na siasa.Na sometimes sports.However,kwenye siasa kuna tabaka la walioko madarakani walikuja wakaingiza utani na maudhi ambapo wengi wenye hasira na nchi walipata shida,wengine kufungiwa kwasababu ya hasira nk.Walifanikiwa kwa kiasi kikubwa.Kuna great thinkers forum,lakini haina wingi wa watu.Wengi ni siasa,lakini si mijadala ambayo ni constructive kama ilivyokuwa huko nyuma.
 
Maendeleo sio mijadala. Ukiona mtu anatoa mada humu ujue asha piga mzigo tayari. Kuongea ni kubadilishana mawazo na ni aina ya burudani sio kila muda ni kazui tu. hayo ni matumizi ya muda wa mapumziko. Usiwe one sided what a boring world it will be kama tutakuwa na mada moja. Usiwe mbinafsi bana aah.
 
Si ndo hapo?ni bora ibadilishwe iitwe "The home of relaxation, hapiness and love"
 
Maendeleo sio mijadala. Ukiona mtu anatoa mada humu ujue asha piga mzigo tayari. Kuongea ni kubadilishana mawazo na ni aina ya burudani sio kila muda ni kazui tu. hayo ni matumizi ya muda wa mapumziko. Usiwe one sided what a boring world it will be kama tutakuwa na mada moja. Usiwe mbinafsi bana aah.

Mkuu kweli tunapenda mapenzi na hiyo avatar yako mkuu!
 
Uwezo mdogo wa kufikiri manbo na kukazania Kutangaziana mambo ya Sera za chama kati ya CDM na CCM.
 
Maendeleo hayajadiliwi, ni mipango na utekelezaji. Siasa kujadidiliwa ndio mahali pake hasa.
 
Maendeleo hayajadiliwi, ni mipango na utekelezaji. Siasa kujadidiliwa ndio mahali pake hasa.

Mipango hujadiliwa,hata kabla ya utekelezaji.Utekelezaji wenyewe unajadiliwa kabla ya kutekelezwa kwake.Amka umelala wewe ndo maana wanasiasa wanakupigeni mibao.Maendeleo yanajadiliwa na kutekelezwa chini ya siasa safi na uongozi bora.
 
tusiwe na ufinyu wa mawazo maana sielewi maana na neno maendeleo kama wewe ulivyo tofasiri mimi kwa ulewa wangu hata kuonekana kwenye kuchangia nakupeana taarifa muhimu za jamii na kufundishana ni maendeleo na siamini kama kuana mtu anashinda kwenye mtandao siku nzima bial kufanya kazi. ni kwamaba wanafanyakazi akishapumzika naingi kuona nini kinaendelea dunia na ndani ya nchi
 
Ndo ubinafsi niliouzungumzia,huwezi kuondoka nje ya "personal box"Maendeleo ni kuacha kuomba omba kama taifa,na kutokuwepo kwa abject poverty.Yani unajiuliza maendeleo ni kitu gani kwenye taifa la tanzania?Huna jirani,ndugu ama rafiki amabaye ni masikini wa kutupwa?Maendeleo ni jamii kutoka kwenye stage moja kwenda nyingine kiuchumi,kijamii nk.Funguka!
 
Sisi wa kikundi cha uamsho mbona umeturuka?
Utakuwa mdini wewe
 
Shida ninayoona ipo,ni ukweli kwamba utekelezaji wa shughuli za kimaendeleo unasimamiwa na wanasiasa,however wananchi wengi hawana ufahamu ama hawajui linkage kati ta maendeleo na siasa.Hapo huwa wanapigwa bao na wana magamba kwa kambiwa wafanye kazi ambazo hazipo.Huo ni utapeli wa wanasiasa dhidi ya wananchi ambao ndo wanawalipa ili waje na mipango ya maendeleo na namna/njia za utekelezaji wake.
 
mkuu ... wewe uponyuma sana ...kuna groups nyingi sana za maendeleo zilizozaliwa humu JF na zinafanya kazi kwa kwenda mbele .... je umeshawahi kuisikia Jamii Empowernment Saccos (JE SACCOS) ambayo tayari imeshasajiliwa na ina offisi yake na members zaidi ya mia moja , je unajua Umoja Farm ambayo tayari ina shamba la mbuzi
 
Back
Top Bottom