Watanzania tuamke, viongozi wanatudharau

Kuna mjadala wa kuletewa msaada wa mchele na nchi ya Marekani na walengwa ni vijana wetu walioko mashuleni.

Kwa bahati mbaya kizazi hiki hakina uwezo wa kuhoji na wazazi wao wamekuwa machawa wanaosifia kila kitu kinachofanywa na mabwana wakubwa bila kujali madhara ya kitu chenyewe.

Wazazi na wanafunzi wa shule hizo wanahaki ya kufahamu kama;

1.Shule hizo zilikuwa hatarini kiasi gani kufungwa sababu ya uhaba wa chakula?

2. Wakuu wa shule hizo waliandika barua wizarani kuomba msaada wa dharula wa kupatiwa chakula? Kama hawakuandika, serikali imejuaje kama wanahitaji msaada?

3. Wazazi walihusishwa kwenye majaribio ya project hiyo ya GMO? (Walijaza consent form?) ya kukubali msaada huo wa chakula? Kitu cha kupewa bila kuomba unayo haki ya kupokea au kukataa na kisheria watoto maamuzi yao hufanywa na wazazi

Kama wazazi na uongozi wa shule walishirikishwa hatua kwa hatua na wakakubali wenyewe, basi sasa ni zamu yetu kuhoji kwasababu hatukuwa na taarifa na ni haki yetu kufahamu pale maslahi ya kiafya ya watanzania wenzetu yanapokuwa mashakani.

Hata kama yote hayo yalifanyika, yatupasa kufahamu kwamba wakulima wa mchele "originale" huko mashambani wanalanguliwa na madalali mchele wao mzuri kwa bei rahisi sana na mchele wao kusafirishwa nchi za nje kwa bei ya super normal profit, halafu watoto wao wanafanyiwa majaribio kwa kulishwa mfano wa mchele uliotengenezwa maabara na viongozi wao wanachekelea mbele ya camera

Tutambue kwamba hayo mazao ya GMO ni project ya muda mrefu yenye malengo maalumu ambayo ki uhalisia wanaofahamu ni wao wenyewe.

Ni jambo la ajabu sana kuruhusu wafanye majaribio ya miradi yao kwa watoto wetu. Huu ni wenda wazimu

Kama zamani, watoto hawa walitakiwa wagome kula na waandamane kudai haki yao ya kula chakula kizuri.

Wazazi nao huku mtaani walitakiwa waifundishe serikali kwamba hawajashindwa kuwapa watoto wao chakula kizuri. Wazazi wafungashe viroba vya mchele kutoka Kyela na Kilombero na madumu ya mafuta ya alizeti kutoka Singida wawapelekee watoto wao shuleni kama ishara ya kuonyesha kwamba Tanzania hatujafikia hatua ya kupewa msaada wa chakula.

Kwanini chakula hicho kipelekwe kwa vijana? Watanzania tuamke
Kwani maghala yetu ya Taifa kuhifadhia chakula yananini humo ndani na kazi kuhifadhi chakula ni nini?
Je kwa mwaka wanatoa kiasi gani kwa wananchi wenye njaa au maafa?

Pesa zote za misaada wanafanyia nini?
Waialua kupunguza matumizi na anasa za magari kwenye msafara, wabunge wakichangia kila mwezi hayo mapesa wanapokea si tayari wanafunzi wamekula! Na sio mashule zote wanahitaji hizo chakula kwingine wanajitosheza.
 
Kwani maghala yetu ya Taifa kuhifadhia chakula yananini humo ndani na kazi kuhifadhi chakula ni nini?
Je kwa mwaka wanatoa kiasi gani kwa wananchi wenye njaa au maafa?

Pesa zote za misaada wanafanyia nini?
Waialua kupunguza matumizi na anasa za magari kwenye msafara, wabunge wakichangia kila mwezi hayo mapesa wanapokea si tayari wanafunzi wamekula! Na sio mashule zote wanahitaji hizo chakula kwingine wanajitosheza.
Kauli ya Waziri Bashe ndo inazidi kuiacha serikali uchi kabisa kuonyesha kuwa serikali yetu mifumo haisomani.

Kwamba chakula kimeombwa na NGO bila serikali kufahamu? Je, jukumu la serikali kuwalinda wananchi wake limekaaje hapo? Kuangusha lawama kwa NGO haisaidii lolote kwasababu hiyo NGO inatakiwa kuthibitiwa na serikali

Shughuli zote za NGO yoyote hazipaswi kutofahamika serikalini. Anaposema NGO hiyo iwaambie wamarekani walete pesa badala ya chakula, wao walikuwa wapi hadi chakula kinaingia nchini?

Taarifa ya Mwakyembe ya hivi karibuni ilionyesha namna NGO nyingi zinavyofadhili vitendo viovu ikiwemo kuhamasisha na kutoa elimu ya maswala ya ndoa za jinsia moja.
 
Hivi,kwanza vyombo husika kweli walithibitisha unafaa kuliwa?
Je,kwa nini marekani haiwagawii raia wake wanaolala na kushinda njaa au kula vya jararani! Kwa nini basi haiuzi na kuwasaidia hata makazi!!! Mtanzania anaelala kwenye chumba cha kawaida chenye bati,na mmarekani anaelala nje kwenye box,yupi bora!!! Bora Kim Jong Un kuliko huyo Biden. Japo kosa ni la walioomba
Hahaha sasa Nani wa kulaumiwa mkuu, aliyetoa msaada au aliyeomba?
 
Tanzania Food and Drug Administration...food hapo inafanya kazi gani?
TFFA ilishafutwa kwenye uso Wa Dunia wakati wa Jiwe. Issues zote related to cosmetics and food safety administration yalihamishwa TBS. Kwa Sasa mambo ya food safety yapo TBS..
Iliyokuwa TFDA ikawa inaitwa TMDA ambayo mandate yake Sasa ni pharmaceutical drugs, antibiotics and medical devices adminstration. So that's that.
 
Pili, why call him hopeless? Kwani huwezi kumjibu bila kumtukana?
Niliona ana dalili ya ujuaji na mm huwa nawachukia sana makanjanja. Hukuona wewe nimekujobu vizuri?! Niliona Kuna information umekosa na umeuliza kwa Nia njema
 
Chakula cha mashoga hicho kipelekewe ikulu wakale wao kama kinafaa
 
Utajua mwenyewe. Siku ingine achana na ujuaji wa kipumbavu
Komaaa. Kama siyo mpumba
Hahaha sasa Nani wa kulaumiwa mkuu, aliyetoa msaada au aliyeomba?
Mi naona alieomba na aliepokea.
Japokuwa wote wanalinda sahani zao,ila,ni aibu. Mchele unaolimwa nchini,nchi jirani zote zinategemee nchi hii, hao hao hao waje wasikie pamoja na kilimo cha kuuzia wengine,bado wanapewa misaada. Af, ulioongezewa virutubisho. Alieomba alijua utakuja mchele gani,aliepokea alijua anapokea nini. Ndege haijatua Dodoma,wakasafirisha kwenda huko. Wakachagua na shule.
Mbona hawajawagawia shule kubwa kubwa Dar?!
Kipi walichoomba hakizalishwi humu nchini! Kuna walakini
 
Back
Top Bottom