Watanzania ni watu wa ajabu sana!, Wanamwaminije Gwajima kuliko Rais wao?

Binafsi nimemwelewa ..mwenye kusoma kwa jicho pevu ataelewa!!hapa ni kebehi kwa bashite na Bwana Yule
Paschal alikua anatumia njia ya jicho la tatu kufikisha ujumbe kinyumenyume. Mwisho wa siku nae kawa teja hisia zimemgonga sasa yupo realy anatafuta maslahi fulani.

Kwenye mada hii paschal mshindi, magufuli akimtumbua makonda atasema niliandika kwa wenye uelewa wa jicho la tatu ni aina fulani ya shinikizo. Hasipomtumbua atasema si niliwaambia Makonda a.k.a bashite hana makosa, vetting ilifanyika na ana vyeti halali.
 
  • Thanks
Reactions: 911
Wanabodi,
Ni ukweli usiofichika watu wana mwamini zaidi Mchungaji Gwajima na uongo wake kumhusu Makonda kuliko wanavyo mwamini rais wao na ukweli wake kuwa Makonda is clean, hajaghushi cheti chochote wala hajafoji jina! .

Kuna ule msemo usemao "you can fool some people for sometimes but you can't fool all the people all the time" ukimaanisha unaweza kuwadanga baadhi tuu ya watu kwa wakati fulani au kwa muda fulani tuu lakini huwezi kuwadanganya watu wote na kwa wakati wote au mara zote na siku zote, lakini Watanzania ni watu wa ajabu kweli, unaweza kuwadanganya wote wakati wote!. (Taking JF as sampling ya Watanzania wote).

Kwa muda mrefu nimekuwa nikijiuliza hili swali "how does it come the same people wanachaguliwa katika chaguzi mbalimbali kwa kuja na ahadi kem kem, mwisho wa siku, wanashindwa kuzitekeleza, na bado wanawarudia na ahadi nyingine kem kem na mnawachagua tena? . Yaani wanawadanganya all the people all the time na bado tunawachagua?. Kipindi cha uchaguzi niliwahi kuuliza swali hili, sikupata majibu ya kuridhisha.

Hii kadhia ya Mkuu wetu wa Mkoa kusingiziwa uongo, imenifundisha kitu. Watanzania ni watu wa ajabu sana, ni warahisi kudanganyika na wepesi wa kusahau.

Juzi kati Mchungaji Gwajima aliibuka na uongo wa mchana kweupe na kumsingizia Makonda ameiba jina la Paul Christian, na ameghushi vyeti vya Paul Christian kujifanya ndio yeye na akafoji kuvitumia kusomea chuo kikuu na kupata ajira ukiwemo uteuzi wa rais wa JMT kuwa DC na sasa ni RC. Mchungaji Gwajima akadai kuwa jina halisi la Makonda ni Daudi Albert Bashite. Uongo huo haukuishia hapo bali alidai kuwa anavyo vyeti vya Daudi Bashite vinavyoonyesha alipata Division 0 na pia anavyo vyeti vya Paul Christian ambavyo Daudi Bashite aliviiba na kuvitumia kama vyake.

Baadhi ya sisi wenye imani haba, kama Tomato tulionyesha kutomwamini Mchungaji Gwajima kwa kumuita ni muongo hadi pale atakapoonyesha hivyo vyeti tuvione ndipo tuamini.

Kitu cha ajabu sana Watanzania wengi wamemwani Gwajima, hivyo sio tuu kumtaka Makonda aonyeshe vyeti vyake bali hadi kushinikiza ajiuzulu au atumbuliwe! . Ajiuzulu kwa kosa lipi au atumbuliwe kwa lipi? .

Gwajima ni Muongo.
Kitendo cha kuhubiri uongo na kudanganya kuwa una ushahidi lakini huutoi huo ushahidi ni uthibitisho tosha ule ulikuwa ni uongo tuu wa mchana kweupe.

Bahati yake Makonda sio tuu ni Msukuma ambapo Wasukuma hawana makuu na wana madharau sana, hivyo amemdharau, bali pia Makonda ni Mlokole hivyo amemshtakia kwa Mungu, akalia machozi madhabahuni na kusamehe.

Kwa Nini Gwajima ni Muongo? .
Kiongozi yoyote kabla ya kuteuliwa na rais, hufanyiwa vetting hivyo vyombo vya serikali vinazo taarifa zote sahihi kumhusu Makonda.

Sasa tangu kutolewa kwa uongo huu, ungekuwa na ukweli hata chembe, tungeshuhudia hatua zikichukuliwa dhidi ya udanganyifu huu.

Kitendo cha mpaka sasa hakuna hatua zozote zilizo chukuliwa dhidi ya Makonda ni uthibitisho kuwa vetting ilifanyika vizuri, jina la Paul Christian Makonda ni jina lake halisi, Mkuu wetu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Na vyeti vyake ni vyeti vyake halisi ambavyo viko kwenye mamlaka yake ya uteuzi, hivyo Paul Makonda hapaswi kumuonyesha mtu yoyote vyeti vyake ili tuu kujibu uongo wa Gwajima.

Sisi Watanzania wote katika umoja wetu ndio tuliomchagua kwa kura nyingi, Dr. John Pombe Magufuli awe rais wetu, kama rais wetu amemwamini Makonda, who is Gwajima kutuletea uongo na kuuamini.

Wewe ambaye unajiita ni Mtanzania mzalendo, unawezaje kumwamini Gwajima kuliko unavyo mwamini rais wako?!.

Nikikuuliza kati ya uongo wa Gwajima kuwa Paul Makonda ni Daudi Bashite na ukweli wa rais Magufuli kuwa Paul Makonda ni Paul Makonda ndio maana mpaka sasa ndiye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, unamwamini nani? .

Shuhudia katika bandiko hili jinsi Watanzania walivyo watu wa ajabu, yaani wanamwamini Mchungaji Gwajima kuliko hata rais wao?! .

Utafiti na Sampling ya Watanzania.
Utafiti huu uko based on jf sampling kuwatumia wana jf kama cross section ya ya Watanzania wote. Ukipandisha bandiko lolote kumtetea Makonda, posts za kukupinga ni nyingi kuliko posts za kukuunga mkono.

Huu ni uthibitisho kuwa sisi Watanzania we don't think, na ndio maana hata kwenye chaguzi zetu, hatuchagui kwa kufanya reasoning bali tunajichagulia tuu alimradi kwa kufuata mkumbo!.

When can we start to think and reason kabla hatujaendelea kudanganywa tena na tena na tena?!. Yaani hapa wamedanganywa na Gwajima na wameamini badala ya kushikamana ukweli halisi wa rais wao kwa mteule wake ni mtu safi kabisa, hajafoji jina lolote wala kughushi cheti chochote?.

Paskali.
Kuanzia leo, nimekudharau ndg. Paskal Mayalla. Yaani kwa usomi wako na ufuatiliaji wako wa mambo bado unaamini Rais anapaswa kuaminika kwa kila kitu? Kweli?!

Uanaamini kila anayeteuliwa kwenye nafasi yoyote anahakikiwa vyeti? Umesahau uteuzi wa makatibu tawala ambao baada ya kuteuliwa na wananchi kupaza sauti walitangaziwa waende na vyeti vyao? Unaimanisha vetting ya kuwapata hawa iliangalia vyeti?

Hivi mpaka leo hii hujui kuwa vetting kwa nafasi za umma hapa TZ huangalia zaidi itikadi ya kisiasa kuliko kigezo chochote Kile?

Paskali, umelipwa? Na nani? Sitaki kuamini hili! Umetishwa? Maybe!

Lakini pia nimeshindwa kukuelewa! Tangu sakata hili lianze umefungua nyuzi kadhaa zinazo kinzana! Huku ukitaka Makonda aweke vyeti wazi kama sululisho la tuhuma na ama ajitokeze kutoa ufafanuzi kama walivyo wahi kufanya waheshimiwa: Mwigulu na Dr. Kigwangala. Leo hii Unakuja kwa staili ya kukanusha mrengo wako katika swala la kufoji vyeti! Hii ni aibu kwa muandishi nguli kama wewe! Kwamba Nawewe unawaza kama Mrisho Mpoto?
Alafu unajifanya unawashangaa watanzania. Ni nani wa kushangawa kama sio wewe? Leo unaamini hiki, kesho Kile! Nakushauri Aidha uwe moto au uwe baridi. Ukiwa vuguvugu si watanzania tu watakao kutapika bali Mungu pia.

Didia
 
Unampata vyema huyu bwana
 
Mayalla kageuka Baba mzazi wa Makonda, jamani kwa umri wako niaibu, hukumuelewa Magufuli alichosema siku ile kwamba jina lako unaitwa NJAA, hata Rais alikunawa, hata ukishinda na kukesha kwenye mitandao wewe siyo chaguo lake nafasi hakuna, baki na njaa yako.
 
Kelele zote hizo zinatokana na mheshimiwa mwenyekiti wa chama cha kule kutajwa kuwa anauza ngada na hao wote wanaoshabikia porojo za Gwajima ni watu wa Chadema,toka lini Gwajima akawa mukweli?mtu anayedanganya umma kuwa anafufua misukule ,anayevunja ndoa za watu.Watu wa Chadema na sio Watanzania wote ndio wanashabikia ujinga huo,kwao wao mtu yeyote anayepinga upande wa serikali ni shujaa na yule anayepinga upinzani ni msaliti.Huyu Makonda akiamua kwenda Chadema utasikia wamepata jembe,lakini akiwa upande wa serikali anaonekana ovyo,wao kila kifanywacho na serikali kwao wao ni kibaya hata kama ni kwa manufaa ya wote,huko ndiko ilikofikia Chadema.Najua hapa watasema mbona nasema mambo ya Chadema wakati anazungumziwa Gwajima,najua kelele zote hizo chanzo ni wana Chadema,kisa wanakijua wao wenyewe.
 
Waswahili husema mchagua nazi mwisho huchagua koroma, nimeamini maana kuna mtu aliutangazia Umma kuwa alikesha kuchagua nazi mwishoni kweli ameambulia bashite
 
Pasco, kabla hujamsingizia Gwajima habari za jina la Bashite naomba msome kwanza Mamaphilipo:Hiyo post ni ya 2015... wakati huo wala hakuna aliyewahi kuota kwamba Makonda angemtaja Askofu Gwajima!!

Ukimsoma hapo, kisha msome hapa: Halafu unganisha dots na habari ya Mwanahalisi:
View attachment 477874

Mamaphilipo hapo juu, December 2015 anamuelezea Mzee Albert Bashite kama Kamanda wa Sungusungu kijijini Kolomije!

Miezi 15 baadae Mwanahalisi inamwelezea Mzee Albert Bashite kama Mwanajeshi Mstaafu aliyekuwa anafanyia kazi Tabora kabla hajarudi Kijijini Kolomije!!!

Siamini kama unaweza kushindwa kupata connection ya Ukamanda wa Sungusungu na mwanajeshi mstaafu!!!

Remember, hapo hapakuwa na Gwajima wala wauza mihadarati!

Kabla hujaweka nukta, pitia profile na posts za Mamaphilipo; halafu ongea na nafsi yako peke yako... kisha ongea wewe na Mungu wako tu halafu jiridhishe ikiwa Mamaphilipo anaonekana kuwa driven na chuki dhidi ya Makonda au anaonesha zile tabia ya zile siasa zetu!

Posts za Mamaphilipo zinapatikana hapa!!

Unless kama ana account nyingine; lakini kwa hiyo ID Mamaphilipo hajaingia JF since January 2017.

Huyu Mama Philipo kwangu mimi ndie mtu wa kwanza kufichua jina la Daudi Bashite!! Kama angekuwa ni mtu driven na kitu fulani dhidi ya Makonda basi baada ya sakata hili angeingia tu JF hata kama anaumwa manake anaonekana anamfahamu Makonda A-Z!!!!

Kwahiyo, acheni kumdondeshea jumba bovu Gwajima!!!
Well done chige.
Huyu Pascal anatuyeyusha hapa na longolongo zake.
Hajui JF ni kisima cha data.
Hata huyo makonda hakujua kuna "mama philipo" humu kamwaga data tangu 2015.
 
Kuanzia leo, nimekudharau ndg. Paskal Mayalla. Yaani kwa usomi wako na ufuatiliaji wako wa mambo bado unaamini Rais anapaswa kuaminika kwa kila kitu? Kweli?!

Uanaamini kila anayeteuliwa kwenye nafasi yoyote anahakikiwa vyeti? Umesahau uteuzi wa makatibu tawala ambao baada ya kuteuliwa na wananchi kupaza sauti walitangaziwa waende na vyeti vyao? Unaimanisha vetting ya kuwapata hawa iliangalia vyeti?

Hivi mpaka leo hii hujui kuwa vetting kwa nafasi za umma hapa TZ huangalia zaidi itikadi ya kisiasa kuliko kigezo chochote Kile?

Paskali, umelipwa? Na nani? Sitaki kuamini hili! Umetishwa? Maybe!

Lakini pia nimeshindwa kukuelewa! Tangu sakata hili lianze umefungua nyuzi kadhaa zinazo kinzana! Huku ukitaka Makonda aweke vyeti wazi kama sululisho la tuhuma na ama ajitokeze kutoa ufafanuzi kama walivyo wahi kufanya waheshimiwa: Mwigulu na Dr. Kigwangala. Leo hii Unakuja kwa staili ya kukanusha mrengo wako katika swala la kufoji vyeti! Hii ni aibu kwa muandishi nguli kama wewe! Kwamba Nawewe unawaza kama Mrisho Mpoto?
Alafu unajifanya unawashangaa watanzania. Ni nani wa kushangawa kama sio wewe? Leo unaamini hiki, kesho Kile! Nakushauri Aidha uwe moto au uwe baridi. Ukiwa vuguvugu si watanzania tu watakao kutapika bali Mungu pia.

Didia
Nyie ndizo sampuli za ajabu kabisa....nyie ndo mliogeuka na kutetea wauza 'unga'. Kwakweli ni aibu na aibu sana...sidhani kama 2020 watanzania watawapa hata viti 20 bungeni sidhani.
 
Haya sasa ni mahaba Cocochanel, lakini si umwambie tu aweke vyeti hadharani na aache kulia lia na longo longo nyingine!?

Hiyo ya wa JF mie simo, ungeandika wachache asilimia 0.03 ndio tupo nyuma ya Mh. Makonda, kiongozi jembe haswa.

Makonda oyeeeeee
 
Kelele zote hizo zinatokana na mheshimiwa mwenyekiti wa chama cha kule kutajwa kuwa anauza ngada na hao wote wanaoshabikia porojo za Gwajima ni watu wa Chadema,toka lini Gwajima akawa mukweli?mtu anayedanganya umma kuwa anafufua misukule ,anayevunja ndoa za watu.Watu wa Chadema na sio Watanzania wote ndio wanashabikia ujinga huo,kwao wao mtu yeyote anayepinga upande wa serikali ni shujaa na yule anayepinga upinzani ni msaliti.Huyu Makonda akiamua kwenda Chadema utasikia wamepata jembe,lakini akiwa upande wa serikali anaonekana ovyo,wao kila kifanywacho na serikali kwao wao ni kibaya hata kama ni kwa manufaa ya wote,huko ndiko ilikofikia Chadema.Najua hapa watasema mbona nasema mambo ya Chadema wakati anazungumziwa Gwajima,najua kelele zote hizo chanzo ni wana Chadema,kisa wanakijua wao wenyewe.
Acha povu, mwambieni boss wenu Bashite aweke vyeti hapa!
 
Wasukuma wame take over ....Makonda ni msukuma ....Pasco ni msukuma ...Gwajima ni msukuma ....JPM ni msukuma ....kanda ya ziwa noma sana ...
 
  • Thanks
Reactions: 911
Sasa yeye Mkuu mwenyewe aache kulia aoneshe vyetu kuwanyamazisha hao unaowaita waongo. Ni kitambo hili suala kama mtajwa angelitoa vyeti aaaah lingekuwa limeisha.
 
Mchungaji wa mwenyezi mungu anatuma Mapepo yamuendee Makonda!!
huyu mchungaji wa mungu au shetani!!
Watanzania wanao Ipenda Tanzania na walio na uchungu na nchi yao Tanzania
hawawezi kumpinga na Kumkashfu Makonda,
hawa tunao waona leo ni kikundi cha Watu wasio na matendo mazuri walio amua kumchafua makonda
na kwavile wana mikono na nguvu za shetani lazima wasumbue japo hawata shinda wala kupenya.

Hii ni vita Na makonda anaijua kuwa ni vita ngumu
lakini kwakuwa Mungu husimama na watu wake Itakwisha vita hii.
Mungu yupi mkuu?? Labda Mungu aitwaye GSM.....
 
Back
Top Bottom