Watanzania mtaacha lini kulalamika?

Chawa wa lumumbashi

JF-Expert Member
Nov 19, 2022
789
1,750
Je, walimu wa serikali wanaumizwa na mpango wa mikataba na wakuu wao?

Ofisi ya Haki ya Askofu Mwamakula imepata malalamiko kutoka kwa baadhi ya walimu wa Shule katika Mkoa wa Dar es Salaam na pia tumegundua kuwa walimu kadhaa wako katika msongo mkubwa sana wa mawazo kufuatia 'mikataba mipya' ya walimu na wakuu wa shule ambapo baadhi ya Shule zimeanza kutekeleza.

Katika programu hiyo mpya, mwalimu huingia mkataba na Mwalimu Mkuu au Mkuu wa Shule wenye kipengere cha kumkandamiza mwalimu kuwa asipotekeleza basi 'majukimu' yake hayo mapya, basi mkuu wake atachukua hatua ye yote dhidi yake.

Katika Manispaa ya Ilala zoezi hilo linaendelea lakini walimu ambao ndio walengwa wanaona kuwa programu hii inawapa stress sana katika mazingira ya kazi na wameanza kutokufurahia kazi.

Baadhi ya walimu walioelezaea hisia zao, wameeleza kuwa viongozi wao wanawachosha na programu nyingi zinazochukua muda wao mwingi na kuwaongezea majukumu wakati hata mazingira ya posho zao, mishahara yao na hata marupurupu yao hayajaboreshwa.

Ushauri wetu kwa serikali ni kwamba, ingeanza kuwekeza katika kuinua maslahi ya walimu na kuwajengea mazingira mazuri ya kazi kuliko kuanza kuwatisha kwa mikataba au programu zisizo shirikishi.

Je, wewe ni mwalimu? Je, unatoka Manispaa gani na katika Mkoa gani? Je, umekutana na programu hiyo katika shule yako? Je, imepokelewaje na walimu? Je, kuna malipo ye yote ya ziada kutokana na programu hiyo kuchukua muda mwingi na kuwaongezea majukumu? Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?
 
Back
Top Bottom