Watanzania mnamuogopa sana Lowassa kuliko JK, wabunge mashahidi...

Hossam

JF-Expert Member
Feb 10, 2011
3,538
2,155
Nimejifunza usemi mmoja, 'in the company of mercenaries, they care about nothing but their own survival'. Watanzania mnamuogopa sana Lowassa na mnamtukuza kuliko kiumbe chochote Tanzania, jamaa ana power sana aisee naona. Hebu ona haya;-
  1. Jamaa siku anatoa hotuba bungeni kumbwambia rafiki yake ambaye 'hawakukutana barabarani' kuwa serikali yake inaumwa saratani ya uoga, haiwezi kutoa maamuzi magumu; wabunge karibu wote walipiga makofi hadi wengine jasho liliwatoka na jamaa hadi alikuwa anakatishakatisha hotuba kuwaacha wapambe wafanye shughuli yao, je waliwaomba wamuumbue JK?
  2. Juzi kati aliwaita waandishi akawapa mkwara hataki kuandikwa tena na Mwanahalisi, raia mwema wala Tanzania daima, wote shatap, hakuna cha maoni ya mhalili wa mtazamo wangu, wala jahazi la jumapili wala gumzo la wiki, wote shatap, atakayeniandika tena atakutana na pilato, meaning anataka awe na muda wa kujifanyia atakayo kwa nafasi. JK alishawahi kuandikwa kahingwa suti je alikaripia hilo zaidi ya blaablaa za akina Salva?
  3. Humuhumu JF, watu zaidi ya 20,000 walii review habari ya Lowassa baada ya mkwara na hii ni idadi kuwa ikionyesha wengi wana hamu nae sana huyu jamaa na wanataka sana kumsikia akitoa matamko mazitomazito kila mara ila basi tu.
  4. Kagoma kujiondoa CCM hiyo NEC yao oohh mara itakuwa baada ya kumpata mrithi wa Rostam, mpaka sasa sijui hata lini itakaa, imepoteza mwelekeo kwa sababu jamaa kakataa katakata na kasema anaumbua mtu, kila mtu kakaa masikio kama punda kusuburi Lowassa ataambiwa ama atafanya nini!!
  5. Hakuna mwandishi wa habari anayejaribu kuiparamia namba yake ya simu hovyo maana huwa wanajibiwa hadi nahisi wanabanwa na haja ndogo, 'no comment' 'sina muda wa kujibu hilo' 'sijui' 'wewe umepata wapi hilo, nenda kaulize zaidi' hayo ni baadhi tu.
Mimi huwa naamini kabisa moyoni mwangu, huyu jamaa atafika mbali sana na siasa za Tanzania, hata kama watu wana personal saga na jamaa lakini ukweli uko palepale jamaa ana nafasi kubwa sana ya kwenda magogoni na hakuna wa kumzuia. Mimi ni mwanaharakati, sipaswi kusema uongo ama kumpendelea mtu, namsema mawazo na mtazamo wangu. Kesho nitaandika upande wa pili wa Edo, nikisahau plz nipeni wake up call.
 
Mwache aendelee kudhani kuwa watanzania wanamwogopa. lakini akumbuke tu aliutema Uwaziri Mkuu bila ridhaa yake na mpaka leo bado jinamizi hilo linamwandama. Watanzania wa jana si wa leo
 
Nahisi alishajua urais wa 2015 uko kwa vijana, kwa hiyo anajitahidi kutaka kutukamata kwa nguvu zote lakini hatudanganyiki!! safari hii ni mapinduzi ndani ya kisanduku cha kura!!

Offcourse kwa upande mwingine, jamaa anatisha aise!! Ananguvu za ajabu.
 
Hamna nguvu za ajabu ni pesa tu! hata gadafi alikuwa nazo.
Kama mtu anawakodia ndege waandishi wa habari unategemea wangaandika nini kuhusu yeye?
Kama unataka kujua kwamba hana nguvu yoyote atoke nje ya chama halafu waandishi wampe ban!
 
Mpaka leo waziri Membe anasema bila kuficha na kwa ujasiri kwamba waziri mkuu (Lowassa) alifukuzwa na rais yaani he was told to go,do we need to say more?
Mwache aendelee kudhani kuwa watanzania wanamwogopa. lakini akumbuke tu aliutema Uwaziri Mkuu bila ridhaa yake na mpaka leo bado jinamizi hilo linamwandama. Watanzania wa jana si wa leo
 
Mashine ya kusaga au kukoboa? Tumekua na majabari na majemedari hodari wenye pesa kila kona ya dunia ,lakini wamepotea au kufa kama kuku wa mdondo e.g. Mubarrak,Ben Ali,Ghadaff,Saddam and the list goes on seuse Lowassa? Lowassa hana lolote nje ya mfumo wa kiserikali,he can't survive a year without government confer,hayo majumba,biashara vyote vinategemea uwepo wake serikalini.
Kuna jamaa yangu pale hazina (MoF) analalamika kwamba jamaa analazimisha kulipwa mafao stahili ya kila mwaka ya mawaziri wakuu wastaafuu wakati yeye ha-qualify because he was sucked(ask Membe,the minister).
Lowasa ni mashine bwana mpaka sasa watz tuanachanganyikiwa!!
 
ndio tunamuogopa ..ya nini kulifuatafuata jitu lina miguvu kama goriath
 
Kwani hata akisimamishwa na chama chake kugombea urais ndo kapita? Nadhani waTZ imefika kipindi sasa kubadili fikra zetu kwamba anaesimamishwa na ccm ndo anafaa kuwa rais lahasha bado kuna vyama vya upinzani bado wanawasimamisha watu ambao ni wasafi na wenye sera nzuri na wanauwezo mkubwa sana wakutuongoza. Sisi kama waTZ tuliangalie kwa makini sana hili
 
we unamjua Lowassa wewe au unasema tu...
 
Kwani hata akisimamishwa na chama chake kugombea urais ndo kapita? Nadhani waTZ imefika kipindi sasa kubadili fikra zetu kwamba anaesimamishwa na ccm ndo anafaa kuwa rais lahasha bado kuna vyama vya upinzani bado wanawasimamisha watu ambao ni wasafi na wenye sera nzuri na wanauwezo mkubwa sana wakutuongoza. Sisi kama waTZ tuliangalie kwa makini sana hili

Tuombe mungu ccm wasimpitishe

Akipitishwa hakuna mpinzani unaweza kumzuia wote walafi tu oops
 
Mashine ya kusaga au kukoboa? Tumekua na majabari na majemedari hodari wenye pesa kila kona ya dunia ,lakini wamepotea au kufa kama kuku wa mdondo e.g. Mubarrak,Ben Ali,Ghadaff,Saddam and the list goes on seuse Lowassa? Lowassa hana lolote nje ya mfumo wa kiserikali,he can't survive a year without government confer,hayo majumba,biashara vyote vinategemea uwepo wake serikalini.
Kuna jamaa yangu pale hazina (MoF) analalamika kwamba jamaa analazimisha kulipwa mafao stahili ya kila mwaka ya mawaziri wakuu wastaafuu wakati yeye ha-qualify because he was sucked(ask Membe,the minister).
......hii ni mashine kiuongozi, aulizwe nani membe? jamaake G.A.D.D.A.F. naye anaukodolea uras macho hana mpya, kinachowatesa watu kuhusu lowassa ni kwmba jamaa ni threat kwao wanaoutaka huo urais, shida yangu ni moja, jamaa yupo kwenye mfumo ambao hatatoka na jipya. si mmewaona akina mwakyembe (dk)nna sitta wameishia kuwa wanafiki tu.
 
Lowassa ni mtu makini na hata tuhuma zilizopelekwa kwake zilipelekwa sababu ya uadilifu wake,. ni vigumu kufanya kazi na mafisadi halafu ukaweka maslahi ya Taifa mbele,. I nawezekana kweli hakuwa mkamilifu lakini hakuna kama yeye kama tatizo ni Richmond mbona alivyoondoka yeye tena kwa kukashifiwa sana na media ikapamba na Mwakyembe aliongea kwa mbwembwe nyingi lakini Serikari haijachukua hatua ya manufaa yoyote, sana sana wakaipenyeza Dowans?

Aliyehusika kuileta Dowans nani? na kwanini hawajibishwi? walimzunguka Lowassa, naweza kuamini sababu yeye kama WM alikuwa na majukumu mengi lakini kosa la Lowassa eti kuhimiza mkataba usahiniwe haraka, hebu tujiulize kama Waziri Mkuu, baraza la mawaziri limekutana limejadili kazi imepewa Richmond taifa lipo gizani waziri analega lega na WM ni kiranja lakini pia anamajukumu zaidi ya kuwaangalia mawaziri mmoja mmoja, ni kosa kuhimiza uwajibikaji? lakini kwakuwa walimfahamu kwamba ni mchapakazi na aliifisha nyota ya JK sababu ya kiutendaji JK alikuwa hasikiki,.

History inajieleza wazi Tanzania ukijua sana makubwa yatakukuta, tulikuwa na Sokoine aliishia vipi? utata Lowassa naweza kusema hakujua nini kinasukwa kama alijua aliacha kisukwe ili aone na jiulize tangu Lowassa atoke hali ya maisha ikoje? Lowassa ana rekodi ya kuvunja mkataba na akashinda, City Water walijichimba Dar Es Salaam wakitanua tu! lakini Lowassa akiwa waziri wa Maji na maendeleo ya mifugo, aliwafukuza nchini, wakakimbilia The Hague, ICC lakini waliambulia patupu, lakini kama angefanya hivyo akina "Ngeleja" ungesikia tunadaiwa some Billions, halafu wanakwambia itabidi tulipe tu! hatuna jinsi ICC ndiyo wamwisho kwa maamuzi??? mfano ni hiyo Dowans, IPTL n.k
 
Nimejifunza usemi mmoja, 'in the company of mercenaries, they care about nothing but their own survival'. Watanzania mnamuogopa sana Lowassa na mnamtukuza kuliko kiumbe chochote Tanzania, jamaa ana power sana aisee naona. Hebu ona haya;-
  1. Jamaa siku anatoa hotuba bungeni kumbwambia rafiki yake ambaye 'hawakukutana barabarani' kuwa serikali yake inaumwa saratani ya uoga, haiwezi kutoa maamuzi magumu; wabunge karibu wote walipiga makofi hadi wengine jasho liliwatoka na jamaa hadi alikuwa anakatishakatisha hotuba kuwaacha wapambe wafanye shughuli yao, je waliwaomba wamuumbue JK?
  2. Juzi kati aliwaita waandishi akawapa mkwara hataki kuandikwa tena na Mwanahalisi, raia mwema wala Tanzania daima, wote shatap, hakuna cha maoni ya mhalili wa mtazamo wangu, wala jahazi la jumapili wala gumzo la wiki, wote shatap, atakayeniandika tena atakutana na pilato, meaning anataka awe na muda wa kujifanyia atakayo kwa nafasi. JK alishawahi kuandikwa kahingwa suti je alikaripia hilo zaidi ya blaablaa za akina Salva?
  3. Humuhumu JF, watu zaidi ya 20,000 walii review habari ya Lowassa baada ya mkwara na hii ni idadi kuwa ikionyesha wengi wana hamu nae sana huyu jamaa na wanataka sana kumsikia akitoa matamko mazitomazito kila mara ila basi tu.
  4. Kagoma kujiondoa CCM hiyo NEC yao oohh mara itakuwa baada ya kumpata mrithi wa Rostam, mpaka sasa sijui hata lini itakaa, imepoteza mwelekeo kwa sababu jamaa kakataa katakata na kasema anaumbua mtu, kila mtu kakaa masikio kama punda kusuburi Lowassa ataambiwa ama atafanya nini!!
  5. Hakuna mwandishi wa habari anayejaribu kuiparamia namba yake ya simu hovyo maana huwa wanajibiwa hadi nahisi wanabanwa na haja ndogo, 'no comment' 'sina muda wa kujibu hilo' 'sijui' 'wewe umepata wapi hilo, nenda kaulize zaidi' hayo ni baadhi tu.
Mimi huwa naamini kabisa moyoni mwangu, huyu jamaa atafika mbali sana na siasa za Tanzania, hata kama watu wana personal saga na jamaa lakini ukweli uko palepale jamaa ana nafasi kubwa sana ya kwenda magogoni na hakuna wa kumzuia. Mimi ni mwanaharakati, sipaswi kusema uongo ama kumpendelea mtu, namsema mawazo na mtazamo wangu. Kesho nitaandika upande wa pili wa Edo, nikisahau plz nipeni wake up call.
Sema ni waandishi wa habari wanamwogopa sio watanzania. nyie waandishi njaa mnaoishi kwa kulambalamba makombo ndio mnaomwogopa kwa sababu bila yeye mtakufa njaa, anaweza kuwageuza mbele nyuma kushoto kulia na mnafuata kwa kuogopa kumuudhi .....
 
Back
Top Bottom