Watanzania mnamuogopa sana Lowassa kuliko JK, wabunge mashahidi...

nimejifunza usemi mmoja, 'in the company of mercenaries, they care about nothing but their own survival'. Watanzania mnamuogopa sana lowassa na mnamtukuza kuliko kiumbe chochote tanzania, jamaa ana power sana aisee naona. Hebu ona haya;-
  1. jamaa siku anatoa hotuba bungeni kumbwambia rafiki yake ambaye 'hawakukutana barabarani' kuwa serikali yake inaumwa saratani ya uoga, haiwezi kutoa maamuzi magumu; wabunge karibu wote walipiga makofi hadi wengine jasho liliwatoka na jamaa hadi alikuwa anakatishakatisha hotuba kuwaacha wapambe wafanye shughuli yao, je waliwaomba wamuumbue jk?
  2. juzi kati aliwaita waandishi akawapa mkwara hataki kuandikwa tena na mwanahalisi, raia mwema wala tanzania daima, wote shatap, hakuna cha maoni ya mhalili wa mtazamo wangu, wala jahazi la jumapili wala gumzo la wiki, wote shatap, atakayeniandika tena atakutana na pilato, meaning anataka awe na muda wa kujifanyia atakayo kwa nafasi. Jk alishawahi kuandikwa kahingwa suti je alikaripia hilo zaidi ya blaablaa za akina salva?
  3. humuhumu jf, watu zaidi ya 20,000 walii review habari ya lowassa baada ya mkwara na hii ni idadi kuwa ikionyesha wengi wana hamu nae sana huyu jamaa na wanataka sana kumsikia akitoa matamko mazitomazito kila mara ila basi tu.
  4. kagoma kujiondoa ccm hiyo nec yao oohh mara itakuwa baada ya kumpata mrithi wa rostam, mpaka sasa sijui hata lini itakaa, imepoteza mwelekeo kwa sababu jamaa kakataa katakata na kasema anaumbua mtu, kila mtu kakaa masikio kama punda kusuburi lowassa ataambiwa ama atafanya nini!!
  5. hakuna mwandishi wa habari anayejaribu kuiparamia namba yake ya simu hovyo maana huwa wanajibiwa hadi nahisi wanabanwa na haja ndogo, 'no comment' 'sina muda wa kujibu hilo' 'sijui' 'wewe umepata wapi hilo, nenda kaulize zaidi' hayo ni baadhi tu.
mimi huwa naamini kabisa moyoni mwangu, huyu jamaa atafika mbali sana na siasa za tanzania, hata kama watu wana personal saga na jamaa lakini ukweli uko palepale jamaa ana nafasi kubwa sana ya kwenda magogoni na hakuna wa kumzuia. Mimi ni mwanaharakati, sipaswi kusema uongo ama kumpendelea mtu, namsema mawazo na mtazamo wangu. Kesho nitaandika upande wa pili wa edo, nikisahau plz nipeni wake up call.

mimi naamini jamaa kaanza mapema kupiganan na vyombo vya habari kwani hawa anawahitaji kesho kama ameanza kuwa mkali mapema je siyo kwamba akipata kiti tutapata shida sana
 
Si muungi mkono huyu bwana kuwa next Tz president,lakini natambua fika kuwa ana nguvu na convicing ya ajabu,namuunga mkono mia mia mpost mada.
 
Lowassa is totally confused/frustrated. Yani amechoka mwili na akili, siku ukikutana nae wala hutaamini kama ndo huyo unaemuona kwenye televisheni. Kwa ufupi Lowassa hana lolote wala haogopeshi wala hatishi, wala hawezi kuwa raisi.
 
Back
Top Bottom