Watanzania lioneni hili

Eliphaz the Temanite

JF-Expert Member
Jan 19, 2010
3,018
1,147
Maeneo ya Tabata Mangumi karibu na garage ya Saibaba kuna kiwanda cha kutengeneza Rasta za kina mama kinaitwa Prima. Kiwanda hiki kinamilikiwa na raia wa kigeni kutoka China …!
Hawa jamaa wanatumikisha vijana wetu kwa wastani wa masaa 10 kwa siku, kuelekea sikukuuu hivi watato wanatoka hadi saa tatu za usiku. Ujira wanalipa ni sh 5000 kwa siku
Mazingira ya kiwanda hayafai hata kidogo hakuna ventilation hakuna AC wala feni kuna vidilisha vidogo viko juu, watoto wanaanguka kila siku …Actually wiki mbili zilizopita kuna mfanyakazi wa kike alifariki dunia ghafla
Machines wanazotumia hawajamaaa ni manual wanapump kwa manually na imagine kazi wanayofanya kwa siku hawa vijana. Kwa wastani wanazalisha rasta hadi mia 3 kwa mtu 1 kwa siku, bei ya reja reja ni sh 7000 kwa bunda 1
Jamani hii ni overexploitation ya vijana wetu, ujira wanapewa hauendani na hali halisi ya maisha ya mtanzania. Kiufupi wanashinda njaaa kila siku ili waweze ku save angalau nauli ya kuwarudisha makwao Wizara ya Kazi, Vyama vya kutetea hak za wafanyakazi tena Mgaya anakaaa karibu huku kabisa okoeni maisha ya vijana wetu
Halafu uki mis-behave kule ndani unachezea makofi toka kwa mchina…….! Vijana wanaogopa bala
 
Shukrani kwa huruma yako. Je wewe una mpango gani wa kuwapa hao vijana ajira mbadala?
 
Watanzania tuzinduke tusitegemee mgeni aje ndio atatutetea haki zetu hivi hao wafanyakazi wakijitambua wanachofanyiwa kisha wakachukua hatua hao wachina hizo rasta watatengeneza wao?...wabongo tumezidi ujinga haki unataka mtu mwingine ndo akutetee...Tuamke Tuchukue Hatua..ni mm mzee wenu pangu pakavu tia mchuzi panoge Desouza kutoka Mbuzi kalamba Reli.::mad:
 
Watanzania tuzinduke
tusitegemee mgeni aje ndio atatutetea haki zetu hivi hao wafanyakazi
wakijitambua wanachofanyiwa kisha wakachukua hatua hao wachina hizo
rasta watatengeneza wao?...wabongo tumezidi ujinga haki unataka mtu
mwingine ndo akutetee...Tuamke Tuchukue Hatua..ni mm mzee wenu pangu
pakavu tia mchuzi panoge Desouza kutoka Mbuzi kalamba
Reli.::mad:

Kwa nini ujasiri huo usitumike kwa sisi wenyewe kuwekeza viwanda kama hicho ili kutoa ajira zenye maslahi bora zaidi kwa vijana wetu?
 
hii ndiyo tanganyika unashangaa hao khali ikoje kwa wafanyakz wa makampuni ya ulinz ucku kucha masaa zaidi ya 12 150000 per mwz
 
Huu ni unyannyasaji ndani ya nchi huru....! Kwani wakiboresha mazingira na wakawapa ujira kwa haki nani atawafuata fuata
 
Sioni kosa kwa hao Wawekezaji, tambueni kuwa kima cha chini kilichoidhinishwa na serikali yetu kwa sekta binafsi ni sh 3800 kwa siku, (8hrs) au 115,000= kwa mwezi. Kama Mchina anawalipa 5000= kwa siku, amevuka kiwango kilichowekwa na serikali, anastahili shukurani, kwa ku create ajira na kulipa zaidi..
 
Watumwa ndani ya Tanzania....Chezeya Serikali dhalimu weye!!!! Sehemu kama hii ni kuiwasha moto tu ili kukomesha udhalimu unaofanywa na haya machina dhidi ya Watanzania wenzetu.
 
Watumwa ndani ya Tanzania....Chezeya Serikali dhalimu weye!!!! Sehemu kama hii ni kuiwasha moto tu ili kukomesha udhalimu unaofanywa na haya machina dhidi ya Watanzania wenzetu.
Hahahahahahahahahahaha duh kuiwasha tena hapana haifai. Yaani umeongea kwa machungu kweli nadhani unatamani kuwawasha makofi hawa .
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mimi kwangu ni karibu kabisa na hicho kiwanda mbona nilikuwa naonaga watu kibao wanakaa pale kwenye mti wa muarubaini wakigombea kazi kwamba wanalipa vizuri eti elfu 2000 ya chakula na elf 5 ya kazi? Nani kakata ule mti wa muarubaini?
 
Tafuta nafasi Ablessed ukaione Mandela ila andaa handkerchiefs nyingi za kufutia machozi. Inaudhi sana kunyanyaswa nchini mwenu kiasi hiki

Hahahahahahahahahahaha duh kuiwasha tena hapana haifai. Yaani umeongea kwa machungu kweli nadhani unatamani kuwawasha makofi hawa .
 
Last edited by a moderator:
Tafuta nafasi Ablessed ukaione Mandela ila andaa handkerchiefs nyingi za kufutia machozi. Inaudhi sana kunyanyaswa nchini mwenu kiasi hiki
Ndugu yangu BAK haya mbona yanatendeka sana ukianzia huko kwa wahindi ndio usiombe bado migodini kuna mengi huko. Hebu njuze mandela nini hiyo mbona hapa umeniacha kwenye mataa.
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom