CHADEMA mkitaka maandamano yafanikiwe fanyeni kwenye makundi na agenda maalumu

Matulanya Mputa

Senior Member
Aug 14, 2023
105
203
Natoa kongole kwa maandamano ya CHADEMA, maandamano yenu mmemaliza kwa kundi moja tu. Maandamano ni hatua, maandamano yenu leo ni hatua, hatua ya kwanza mmemaliza kuwakutanisha watu wa mijini hasa tabaka la chini na pia maandamano yenu leo yanachukuliwa kawaida kwakuwa wameona hayana sura mpya.

Ushauri wangu; maandamano kwakuwa ni njia ya kudai haki sasa nendeni katika makundi yafuatayo ili mfunge kazi, na maandamano yawe yenye tija na sura mpya;

(I) ITISHENI MAANDAMANO KUPINGA TATIZO LA AJIRA TU MSICHANGANYE NA MAMBO MENGINE (jifunzeni nchi za ulaya katika maandamano yao).

(II) ITISHENI MAANDAMANO YA KIKANDA KUHUSU CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI WAKULIMA NA WAFUGAJI (mfn; mkoa wa Ruvuma wanalia na bei ndogo ya mahindi, Mtwara korosho, Kanda ya ziwa pamba, pia angalieni changamoto zawafugai hasa wamasai na wasukuma).

(III) ITISHENI MAANDAMANO MKISHIRIKISHA WAFANYABIASHARA TU KUJUA CHANGAMOTO ZAO.

(III) NA MWISHO MARILIZENI NA WATUMISHI WA UMMA (hawa ndiyo usimama katika sanduku la kura japo hawezi kwenda barabarani lakini watasimama pamoha).

Kama kuna kundi nimesahau mtaongeza, kwa sisi wanahistoria ukirudi karne ya 16 bara la Ulaya utaona maandamano yao walivyoendesha kwa makundi na agenda maalumu na yakafanikiwa.

Kuna maeneo hamjagusa, mkigusa hayo maeneo hata katiba itakuja yenye.

MWENE: MATULANYA MPUTA
email:maggierozaria@gmail.com
 
Back
Top Bottom