Watano mbaroni Dar wakihusishwa na mauaji ya RPC Barlow

hivi ukipanga nyumba ya mganga utauliza kwann nanuka uvumba? nitafufuka nazo 200 za kizungu, kiarabu, kiswahili na kihindi. pia nene, nyembembe, fupi kwa ndefu kubwa kwa ndogo. wewe mwenzangu je?
ahahahhahaahhahahhahahhahhahah mwalimu mwenzangu shtilo una balaaa wewe yani nimecheka mpaka napaliwa huku kha!
 
hivi ukipanga nyumba ya mganga utauliza kwann nanuka uvumba? nitafufuka nazo 200 za kizungu, kiarabu, kiswahili na kihindi. pia nene, nyembembe, fupi kwa ndefu kubwa kwa ndogo. wewe mwenzangu je?
Aisee! Kazi ipo. Manake unaweza chukulia masihara kumbe kweli lol

Mimi ni mtumishi wa Bwana, Natenda kama alivyoniagiza. Ntaibuka na ya mke wangu. Nyingine zimeshaoshwa kwa damu ya Yesu.
 
Hili polisi wanaliweza kwa kuwa ni la mwenzao na wanajua madhambi yao na wabaya wao.Lakini uchunguzi kwa vifo vya raia wengine siku zote unaendelea na kufutia mara tukio lingine linapotokea.

Tanzania kisiwa cha amani kwa wenye mamlaka, lakini sasa kinageuka kuwa kisiwa cha mauaji ya kila mtu bila kujali cheo au utajiri alionao mtu.

kaka nakubaliana na wewe kwamba hawa jamaa issue ikiwausu wao au wakubwa wenye mamlaka katika nchi yetu wanachakarika haraka sana lakini kwa wengine inakuwa tofauti hebu vikiria maslani issue ya ulimboka si walijidai hawahusiki na wakaahidi kuwatafuta wahusika na kuwafikisha mbele ya sheria lakini hadi leo kiko wapi wamekaa kimya hata ulimboka aliporejea akiwa mzima hawajaenda kumuhoji kujua ilikuwaje kama sehemu ya uchunguzi wa hilo tatizo sasa wanajeuri gani ya kudai kuwa hawakuhusika? mbona issue ya baro ambeye aliuwawa na watu wasiofahamika wameza kuifanyia kazi na kuwatia wahusika mbaroni ndani ya muda mfupi sana?
 
Kamanda Barlow keshakufa haya yanayotokea sasa hayamsaidii yeye bali sisi twaweza kupata mafundisho kadha wa kadha. mwandishi mzuri anaweza kuandika stori kuanzia kabla ya tukio wakati wa tukio na huo upelelezi. novel itauzika sana
 
Kwa issue kama hii me nasema IGP atakiwi kabisa kuwa kazin kwa kuendelea kuwepo kwake maovu mengi yanafichw kabisa japo hili limekuwa fundisho kwa viongozi mbalimbali wenye tabia kama hawa.
 
wana JF wenzangu, bila kusema uongo, mi nilikuwa naunganisha story kwenye hili tukio la mauaji ya kamanda, na sikumtoa hatiani marehemu kamwe, niliamini kuwa alikuwa na uhusiano na mwl. japo ninamfahamu ndugu wa damu wa insp., niliamini hivyo bila kujua undani wa tukio. hapo naomba Mungu anisamehe kwa dhambi hiyo ya dhana.
kweli kumbe ni bora ukajua kwanza jambo kabla hujaconclude au kabla hujajudge chochote. bwana yule hakuwa mshkaji wa huyo mwl hata kidogo, tena huyo mwl alikuwa mke wa marehemu ndugu yake insp. na kweli walikuwa kwenye kikao cha harusi kweli, na kati ya wanakamati huyo ndiye aliyejitolea kumpeleka mweka hazina wao hm (yaani mwl). na wauaji hawakumkusudia yeye insp, ila mwanamume mwingine tofauti ambae mwl alikuwa na mahusiano nae, kwa hiyo wakafikiri huyo ndio mwanamume mwenyewe, bila kujiuliza wakamuua.
kwa hiyo tusiwe na fikira mbaya juu ya polisi wa watu, tuache pengine katika uchunguzi wa polisi na kwa msaada wa mwl, wahusika wote huenda wakakamatwa. hata kama insp ana matatizo mengine lakini hili lililopelekea kifo chake, halikuwa la kweli, amedhulumiwa uhai.
 
Watakamatwa wengi,swala ni ukweli wa uhusika wa wanaokamatwa ambao wanaweza kuwa mahabusu kwa kipindi kisichopunguwa miaka 2,huku wengine wakiwa ni wahusikawa kusadikika tu.
Tuna tatizo na mfumo wetu wa uchunguzi wa matatizo ya mauaji,jeshi letu la polisi limepata wapi utaalam kiasi hiki ambapo limeweza kuwaweka mbaroni watuhumiwa hawa.
Nakumbuka kazi ya kufanya upelelezi kwa pupa ilisababisha vijana 11 wakae ndani miaka miwili kwa tuhumu za kuhusika na mauaji ya mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya RUNGWE ambaye pia alikuwa ni mwenyekiti wa CCM wilayani rungwe, then wameachiwa huru huku wakiwa wamepoteza bure karibia miaka miwili wakiwa mahabusu.
NI WENGI WATAKAMATWA ILI POLISI IDANGANYE KUONYESHA INAO UWEZO AMBAO IMESHINDWA KUONYESHA KWENYE MATUKIO KAMA HAYO YAWAPATAPO RAIA WENGINE...AIBU
 
wana JF wenzangu, bila kusema uongo, mi nilikuwa naunganisha story kwenye hili tukio la mauaji ya kamanda, na sikumtoa hatiani marehemu kamwe, niliamini kuwa alikuwa na uhusiano na mwl. japo ninamfahamu ndugu wa damu wa insp., niliamini hivyo bila kujua undani wa tukio. hapo naomba Mungu anisamehe kwa dhambi hiyo ya dhana.
kweli kumbe ni bora ukajua kwanza jambo kabla hujaconclude au kabla hujajudge chochote. bwana yule hakuwa mshkaji wa huyo mwl hata kidogo, tena huyo mwl alikuwa mke wa marehemu ndugu yake insp. na kweli walikuwa kwenye kikao cha harusi kweli, na kati ya wanakamati huyo ndiye aliyejitolea kumpeleka mweka hazina wao hm (yaani mwl). na wauaji hawakumkusudia yeye insp, ila mwanamume mwingine tofauti ambae mwl alikuwa na mahusiano nae, kwa hiyo wakafikiri huyo ndio mwanamume mwenyewe, bila kujiuliza wakamuua.
kwa hiyo tusiwe na fikira mbaya juu ya polisi wa watu, tuache pengine katika uchunguzi wa polisi na kwa msaada wa mwl, wahusika wote huenda wakakamatwa. hata kama insp ana matatizo mengine lakini hili lililopelekea kifo chake, halikuwa la kweli, amedhulumiwa uhai.

kwenye red. sijakuelewa,huyo mwalimu ni ndugu wa damu wa insp. then alikuwa mke wa marehem ndg yake insp. !!!??? naona nyota nyota
 
Nimesikia Kamanda alikuwa kwenye Zinaa shirikishi akakutana na walinzi shirikishi...kazi hapo ikatimia
 
Katika pitapita zangu nimekutana na hii:

KATUNEWS BLOG: POLISI YATAJA WALIONASWA KUMUUA KAMANDA BARLOW
Na Frederick Katulanda
JESHI la polisi, limetoa taarifa ya awali ya mauaji ya aliyekuwa kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Liberatus Barlow (53) na kubainisha idadi ya watuhumiwa 10 wanashikiliwa kwa mauaji hayo huku likitaja sababu mbili za kisasi cha mapenzi na ujambazi ndiyo zinaweza kuwa chanzo.
Taarifa hiyo ya kukamatwa kwa watuhumiwa hao wa mauaji imetolewa na Mkurugenzi wa Upelelezi wa makosa ya Jinai (DCI) Robert Manumba mbele ya Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Generali wa Polisi (IGP) Said Mwema na makamanda mbalimbali wa jeshi hili kutoka wilaya na vituo mbalimbali mkoani Mwanza.
Taarifa hiyo imetolewa jana jioni muda mfupi baada ya IGP Mwema kumaliza vikao viwili kimoja kikiwa ni Kamati ya Ulinzi na Usalama cha Mkoa kinachoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo, na baadaye kikao cha maofisa wa polisi ambavyo vyote waandishi wa habari hawakuudhuria.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoa wa Mwanza, Evarist Ndikilo akizungumza na Mwananchi alieleza kwamba jeshi hilo lilitoa taarifa hiyo katika kikao hicho awali na kwamba baada ya kuridhika nayo ndipo alikwenda kuzungumza na maofisa wake na kutoa kwa vyombo vya habari.
Uchunguzi ulivyoendeshwa:
Akizungumzia namna ambavyo jeshi hilo liliendesha uchunguzi huo, DCI Manumba alisema kuwa walipofika Mwanza yeye na kikosi chake kilichojulikana kama Kikosi kazi cha Upelelezi walilazimika kujigawa katika vikosi vitatu ambavyo ni Kikosi cha Ukamataji, Kikosi cha Mahojiano na kingine cha ufuatiliaji na ukusanyaji wa taarifa za Interejensia huku wakitumia njia za kisanyansi katika ufuatiliaji mitandao ya simu.
Alisema kuwa kikosi kazi cha ufuatiliaji kilijikita katika ufuatiliaji katika mikoa yote ya kanda ya ziwa ikiwemo Dar es Saalam kutoka na taarifa walizokuwa zikichambuliwa kinterejensia na kutoa majukumu kwa kikosi cha ukamataji na waliokamatwa walikabidhiwa kikosi cha mahojiano.
“Wakati tunafanya hivyo tayari wenzetu walikuwa wanamshikiria Mwalimu Doroth aliyekuwa na marehemu wakatia akiuwawa na majambazi hao huku wakimuhoji kutokana na tarifa mbalimbali zilizokuwa zinafaikia zikiwemo zile wivu wa mapenzi”alisema Manumba na kuongeza kuwa.
Sababu za Ujambazi:
Alisema katika ufuatiliaji wa pili baada ya kupatikana simu ya Mwalimu Dorothy Moses aliyekuwa na marehemu kamanda huyo usiku wa tukio, ambayo ilipatikana na kufanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa watano jijini Dar es salaam ambao wameonekana kuwa na rekodi ya kuhusika na mtukio kadhaa ya Ujambazi Mwanza na Dar es salaam.
DCI Manumba akisoma ripoti ya uchunguzi kwa Waandishi wa Habari
“Watu hawa ni majambazi, na kabla ya kumuua kamanda Mwanza inaonekana walihusika na matuko kadhaa ya ujambazi, na hata baada ya kukimbilia dar nako walihusika na matukio kadhaa na kufanikiwa kukamatwa ambapo wamekiri kuhusika na kutuwezesha kukamata siraha aina ya Shotgun pamoja na silaha nyingine aina ya Pumpaction,” alieleza DCI Manumba.
Aliwataja waliokamatwa katika tukio la Dar es salaam kuwa ni Muganyizi Marko Petro (36), Chacha Mwita (50), Magige Mwarwa(35), Edward Masota (33) pamoja na Bhoke Mwita (54) ambao wote wamekamatiwa jijini Dar es Saalm.
Kutokana na rekodi ya ujambazi na mmoja wao kubainika kuwa alitoka jela miezi minne kabla ya tukio hilo jeshi la polisi kwa watuhumiwa hawa limedai sababu inaweza kuwa ni tukio la ujambazi.
Sababu za kisasi cha Mapenzi:
Hata hivyo akielezea wakati wa maswali kwa waandishi wa habari, IGP Mwema alisema Waliokamatwa Dar ni watuhumiwa watano, lakini wapo watuhumiwa wengine wa Mwanza ambao ni pamoja na Dorothy Moses na mpenzi wake Feliex Felician na nduguye Fumo Felician pamoja na wengine wawili bado wanashikiliwa na jeshi hilo kutokana na dhana ya awali ya kisasi cha mapenzi ambao hawaajaachiwa.
Kwa sasa hatuwezi kueleza iwapo sababu ya mauaji ni nini hasa bado tunaendelea na kuunganisha sababu za makundi haya mawili na kile walichosema ili kupata sababu moja ya mauaji yao na pindi tutakapokamilisha tutaitangaza.



Wengine watatufwa:
Aidha IGP Mwema na DCI Manumba walieleza kuwa katika itadi hiyo ya watuhumiwa 10 bado jeshi lake linaendelea kuwasaka watu wengine wawili ambao wametajwa kuhusika na tukio hilo na kundi la watuhumiwa waliokamatwa Dar es salaam.
IGP Mwema alisema kuwa tukio la mauwaji ya kamanda Barlow halijawavuja moyo na badala yake wamejifunza na kuongeza ulinzi zaidi ili kuzuia matukio kama hayo yasitokee tena.
Alisema kuwa Jeshi la Polis linajipanga kuwapatia mafunzo askali wake ili kuhakikisha analinda hali ya usalama wa Taifa hili.
“Hata hivyo tumeweza kufanya kazi nzuri katika kipindi hiki kwa kuhakikisha mkoa wa Mwanza unakuwa na amani na utulivu baada ya kifo cha kamanda Barlow”alisema IGP Mwema.
Aliendelea kwa kusema kuwa Jeshi la Polisi halitasita kumchukulia hatua mtu yeyote ambayo atakuwa nataka kuvuja amania ya nchi hii iwe uchambazi au uchochozi.
Aliwaasa wananchi kuwa na siri binafsi,ya umma na yakijamii ili kujikinga na kuharibu amani ya Taifa hilo ambayo imekuwepo kwa muda mrefu.
Kamanda Barlow aliuawa Oktoba 13 mwaka huu majira ya saa 8 usiku wakati akitoka kwenye kikao cha maandalizi ya arusi ya mtoto wa dada yake Sembuli Moleto kilichofanyika Hotel Florida wakati akimsindikiza mwalimu wa shule ya Msingi Nyamagana B, Dorothy Moses eneo la Minazi mitatu Kitangiri.
 
na kila zinaa mtu aifanyayo lazima aje kuilipia tu.manake quran inasema siku mzinzi akifa atafufliwa akiwa na nyuchi zote alizo tumikia akiwa hai na hizi zitaota usoni mwake sasa sijui itakuwaje iyo siku lol!

siitamani hata kidogo manake...................mmmh!

Ujumbe wako umefika lakini katika Quran hakuna aya inayosema hivyo...labda utusaidie
 
kumbe polisi mnajua kuchunguza chunguzeni na mauwaji mengine au mpaka achinjwe rpc mwingine
 
.......................... hiii mada imeanza vingene inaishia vingine. ................ ni mchanganyiko... juu ya mkanganyiko
 
Haya tusubiri stori yao yasije kuwa ya kuletewa Wakenya walioenda tena kujisalimisha kwa mchungaji fulani...

Eti mzee mwana kijiji mbona katika utekaji wa dr. Ulimboka Juhudi hazikuwa kubwa kama hizi, na kuna ushahidi umetolewa na vyombo vya habari pamoja na yeye mwenyewe mtekwaji kupitia wakili wake lakini hawamkamati huyo bw.Ramadhani Ighondu aka ABEID wanamficha hebu tumia busara zako unisadie niweze kujua huu utendaji wa jeshi la polisi au ndio kutumia mbwa kwenda kukamata simba?
 
Back
Top Bottom