Anselm
JF-Expert Member
- Nov 16, 2010
- 1,710
- 291
Najua kuna watakaoniita Mnafiki,lkn kama kuongelea kitu ambacho kwa mtazamo wa kawaida kabisa kinaonekana siyo cha kawaida wacha tu niendelee kuitwa hivyohivyo lkn sitaacha kusema.
Watani kupitia Msemaji wao Bwana Ezekiel Kimwaga wametangaza bei ya Super Striker wao Emanuel Okwi kuwa ni fedha za kitanzania Billioni mbili (2000,000,000/= In tarakimu). Jambo 1 ambalo limekuwa nikijiulizaga kila wakati ni kuwa kama Viongozi wa mabingwa hawa wa soka hapa Tanzania huwa wanajua wanachokizungumzaga au huwa wanazungumza tu kwasababu maneno hayalipiwi kodi,hii siyo mara ya kwanza kwa washika hatamu wa Club hiyo kongwe kuutangazia uma "utumbo"...sijui huwa wanafanya hivyo kwa faida ya nani hasa?
Bei ya 2 billion kwa Okwi wa kupanda na kushuka kiwango mechi 1 hadi nyingine haimsaidii mchezaji hata kidogo,hiyo ni sawasawa na kusema Okwi hauzwi kwa namna yeyote ile, kwasbabau ni Chizi tu anayeweza kuvunja benki kumsajili mchezaji wa kiwango cha Okwi kwa gharama hiyo. Hivi, mfano, leo hii ukiwaambia wale Al Ahly Shandy kuwa Okwi anauzwa kwa US$ 1,500,000 si watacheka mpaka wazimie.
Ushauri wangu (whether they take it or not);
Kama wana nia ya kumuuza Okwi kwa faida yao na ya mchezaji mwenyewe wa'set bei inayostahili kwa mchezaji wa kiwango chake then wa'add vipengele ambavyo vitakuwa vinawanufaisha hata wao ikiwa mchezaji atazidi kufanya vizuri ni kuuzwa kuelekea team kubwa za Ulaya,tofauti na hapo ataendelea kucheza pale kwenye uwanja wa Kinesi(Simba wanapofanyiaga mazoezi) mpaka siku atakapojanjaluka na kutokomea 1 kwa 1 asirudi.
Nawasilisha!