Watangazaji hamnazo

Gama

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
13,266
4,716
Jamani, sasa hivi niko kwenye daladala natoka tazara to posta, kunamtangazaji anaendesha kipindi cha mitikisiko ya pwami(nadhani ni radio times fm) mda wote anasifia timu ya chelsi na kuiponda Man. Hiii inanishangaza sana: inamaana redio hii au mtangazaji huyu hana la kuzungumzia lenye manufaa kwa wa tz?
 
Eeh, we Gama unamlaumu huyo mtangazaji, unafahamu mwajiri wake ni shabiki wa timu gani kati ya hizo mbili? Na huyo mtangazi si yuko ofisini kwake na hajatukana mtu, hebu mwache aendeshe kipindi chake.
 
mimi asubuhi ya jana na leo kwenye gari imenilazimu kuzima redio, huwa na penda kusikiliza Power Breakfast Clouds ila Gerald ameanza kitabia kile cha Kibonde chakujipendekeza kwa watu Maana anazungumzia suala la Mh. Joseph Mbilinyi all the time as if hakuna jambo jingine lakusemea.
Mara viongozi wamelogwa....... wanalogana wanaporomosha mitusi..... Naona anataka fadhila za waliopondwa na Mh. Joseph Mbilinyi.
Kutokana na chuki zenu kwake hayo mnayo taka yatokee kwake hayoto tokea.........
KWELI WATANGAZAJI HAMNAZO............!!!!!!!!!!!!!!!!
 
clouds wenzio tushaacha kusikiliza, mi inanipa kichefu chefu
 
Eeh, we Gama unamlaumu huyo mtangazaji, unafahamu mwajiri wake ni shabiki wa timu gani kati ya hizo mbili? Na huyo mtangazi si yuko ofisini kwake na hajatukana mtu, hebu mwache aendeshe kipindi chake.

Sawa, tumuache aendelee kujaza upupu hewani huku nchi ikididimia katika dimbwi la matatizo: umaskini, mfumuko wa bei, magonjwa, huduma duni hospitali, mabomu, ukosefu wa umeme, utitiri wa bidhaa feki madukani, serikali isiyotimiza majukumu yake.................................................. Kwa haya machache unadhani ni haki radio kutumia saa nzima kuzungumzia chelsea + man?!, .
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom