"Watangazaji Bora wa mpira Tanzania...."

Mimi 10 bora wangu ni hawa:

1.Mshindo Mkeyenge
2.Omary Jongo
3.Dominick Chilambo
4.Charles Martin Hilary
5.Barthlomeo Komba
6.Ahmed Jongo
7.Salim Mbonde
8.Abdallah Idrisa Majura
9.Mikidad Mahmoud 'Brother Mick" na
10.Abdul Ngarawa
 
naikumbuka hii ya Omari Jongo na Charles H. "wasikilizaji ni kipindi cha pili cha pili hapa" au ile ya D.Chillambo mtangazaji aliyetangaza magoli mengi kuliko mwingine yeyote kwenye mechi moja
 
Wewe ndio mfuatiliaji wa Matangazo ya mpira.
Sio huyo mpayukaji aliyeanzisha thread.

Mpira bila Charles Hillary na Marehemu Omari Jongo haukusikilizika sheikh kwa watu wenye utimamu kichwani.

Wakati huo fundi mitambo kwenye caravan alikuwa Obi Mwambungu

Msimamizi wa matangazo Nadhir Mayoka

Tukirudishwa studio tunapokelewa na Bujaga Izengo Kadago...

puumbav hakuna swedi mwinyi wala sijui maulid kitenge

Umenikumbusha mbali sanaaaa mkuu! Wakati ule Ahmed Jongo alikua akitangaza Gooooooooooooooooooo! hata kabla mpra haujamfikia Zamoyoni Mogella, akishaona amejipanga kwenye position nzuri kupokea pasi ya mwisho na kweli anapoke pasi toka kwa Hussein Marsha nae hafanyi ajizi.

Usiombe Dominick chillambo atangaze mechi ya Pamba ya Mwanza atakavyoipamba.... Wana T.P Lindanda, Kawekamo.
Kwa sasa watangazaji wa kiwango cha Charles, Chillambo Dominick, Ahmed Jongo, na Omary Jongo ni ngumu kuwapata. Ila Jesse anajitahidi.
 
Dominick CHilambo:Jongo, nafikiriri unanipata?
Jongo: Ndio Chilambo.
Chilambo: Huku Mwanza vijana wa Tuit Puissant Lindanda wanafungua kitabu, mpira ulianzia kwa Nico Bambaga akafungua chumba kwa ball dancer Mao Mkami ambae bila ajizi alimsogea Hamza Mponda na kumpeleka shule kipa wa Ushirika Bahatisha Ndulute, mpaka sasa Pamba 3, UShirika 1, kwako Jongo na Chaaarles......
 
Charles H: Namna gani hapa Jumanne Shengo anarudisha mpira kiduchu na unanaswa na double R...Pilsner 1 sisi 0.
 
Kina mheshimiwa mmoja Juma Nkamia alishindwa kabisa kuficha mapenzi yake wakati wa kutangaza mpira bora amekuwa mbunge labda nitasililiza tena mpira TBC lakini bado wanahitaji mabadiliko makubwa
 
Ahmed na Omary Jongo,Charles Hilary,Sued Mwinyi,Juma Nkamia,Dominic Chilambo,wapo wengi lakini hawa wanawazidi kiufundi.
 
Wewe ndio mfuatiliaji wa Matangazo ya mpira.
Sio huyo mpayukaji aliyeanzisha thread.

Mpira bila Charles Hillary na Marehemu Omari Jongo haukusikilizika sheikh kwa watu wenye utimamu kichwani.

Wakati huo fundi mitambo kwenye caravan alikuwa Obi Mwambungu

Msimamizi wa matangazo Nadhir Mayoka

Tukirudishwa studio tunapokelewa na Bujaga Izengo Kadago...

puumbav hakuna swedi mwinyi wala sijui maulid kitenge


...Asante Mkuu! Hapa ungeongeza pia Salim Mbonde na kwenye OB Van au Studio kwenye mitambo, Noel Namaloe.
Kwangu mimi Watangazaji wa mpira walikuwa wawili tu:
Charles Hilary.....na Pasi za Giza!!
Salim Mbonde.
 
Mimi 10 bora wangu ni hawa:

1.Mshindo Mkeyenge
2.Omary Jongo
3.Dominick Chilambo
4.Charles Martin Hilary
5.Barthlomeo Komba
6.Ahmed Jongo
7.Salim Mbonde
8.Abdallah Idrisa Majura
9.Mikidad Mahmoud 'Brother Mick" na
10.Abdul Ngarawa

Nimesikitika kutowaona wafuatao:
1. Ahmed Kipozi; huyu alikuwa nanifurahisha sana kwa pozi zake.
2. Salim Seif Nkamba
 
Gomba usitake kukonka jukwaa na kujifanya wewe ndo unawajua sana watangazaji na tuamini kuwa list yako ndio sahihi.Wewe panga list yako tulia watu waichambue sio kuponda list za wengine!!!kama mtangazaji anataja list na akitangaza goli ndio ujiko???Ile siku walichelewa kujiunga uwanjani na kosakosa zilianza mapema sasa presenter afanyaje???Hayo ni maoni yako tu na watakao kuunga mkono.Mimi yangu iko hivi:
1.charles hillal
2.Dominic Chilambo
3.JESSE JOHN
4.Omary jongo
5.Ahmed jongo
 
Safi sana Chomba '..Orodha na ushahidi kama huu'

Lengo la thread ni kuwaamsha watangazaji wa mpira kuboresha mbinu zao za utangazaji kwa ajili ya jamii.

Nitaomba mwongozo wa msimamizi wa forum hii namna anavyoweza kunisaidia kumpa zawadi Mtangazaji au mwakilishi wake atakayekuwa ametajwa zaidi ya wengine kupitia JF.

Du! kweli wazee mna vichwa!
 
Mimi namfagilia sana Sekioni Kitojo, huyu alitangaza mechi ya fainali ya klabu bingwa ya A. Mashariki na Kati (wakati ule - 1986), pale shamba la bibi, ilikuwa kati ya Yanga na El-Merreikh ya Sudan. Hadi dk. ya 88 Yanga walikuwa nyuma kwa 2-0! Ndipo Sure Boy, Abubakar Salum alipoisawazishia Yanga na kupelekea dk.30 hatimaye Yanga walitota kwa penalty 4-2. Sekioni alipaza sauti na kushangilia kwa nguvu zooote......"Amini Usiamini, amini usiamini, amini usiamini........."alirudia mara kadhaa kabla ya kusema Sure Boy, anaisawazishia Yanga! Pia enzi zile tulikuwa tunarekodi matangazo ya mpira hasa mechi za Yanga na Simba. Siku mpinzani wako uliyemfunga akikuchokoza tu unamuwekea kumkumbushia yale mabao, yaani ilikuwa raha sana!
 
umesahau, mikidad mahmood and nadhir mayoka. Ilinoda wakiwamo uwanjani Zamoyoni mogella, juma mkambi, makumbi juma, abeid mziba
...Mikidadi Mahmood hakuwahi kuwa mtangazaji mzuri wa mpira RTD wakati huo alijaribu lakini hakuwa na mvuto. Hii pia ilikuwa kwa Julius Nyaisanga alijaribu kutangaza mechi kati ya Simba Vs Coastal Union uwanja wa Taifa mwaka 89 lakini hakurudi tena. Lakini ninaowakumbuka ni Charles Hilary (mwanzilishi wa neno majalo akimaanisha cross na darizi mchezaji akipigwa kanzu na sauti yake husikika pia kwenye kiashirio cha kuanza kwa kipindi cha Sports Leo Radio One ile ilikuwa mechi ya Simba Vs Sports Club Villa ya Uganda 1990 goli lilofungwa na aliyekuwa kocha mchezaji wa Simba Hassan Hafif) , Ahmed Jongo (aliyeanzisha msemo wa maguu 12 ya mtu mzima kunapokuwa na kupigwa penati), Salim Mbonde (Kumbuka Mechi ya Simba Vs National Al- Ahari 1984) , Dominick Chilambo (aliyeibatiza timu ya Pamba ya Mwanza wakati ule jina la TP Lindada), baadaye wakaja akina Sued bin Mwinyi,Halima Mchuka,Jesse John,sasa wamo pia akina Maulid Kitenge na Issac Gamba (Radio One), Tom Chilala (RFA) na wengineo
 
WanaJF,mmetosheka na kuridhika kuwa hawa waliotajwa ni watangazaji bora wa mpira Tanzania?
 
Kwa hao hakuna ubishi hata senti moja.Kwa viwango vya miaka hii yule ustaadhi Sued Mwinyi alijitahidi kuburudisha kunako matangazo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom