"Watangazaji Bora wa mpira Tanzania...."

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
23,914
23,077
Hawa ndio watangazaji wa mpira bora watatu Tanzania kati ya 1985-2011.
1.Sued Mwinyi
2.Jesse John
3.Hamed Jongo

Vigezo nilivyotumia
1. Kutochosha wasikilizaji.
2. kutokuonyesha upendeleo wa timu wakati wa kuzijadili kipindi cha mapumziko.
3.Kuonyesha uzalendo wa hali ya juu wakati wa mechi za kimataifa kwa vilabu au timu za taifa za Tanzania.

Ni maoni yangu binafsi. Wewe orodha yako ikoje?
 
Charles Hillary, Omar Jongo, the late Dominic Chillambo(huyu aliweza kutangaza mara kadhaa dk.90 mwenyewe)
 
Wewe ndio mfuatiliaji wa Matangazo ya mpira.
Sio huyo mpayukaji aliyeanzisha thread.

Mpira bila Charles Hillary na Marehemu Omari Jongo haukusikilizika sheikh kwa watu wenye utimamu kichwani.

Wakati huo fundi mitambo kwenye caravan alikuwa Obi Mwambungu

Msimamizi wa matangazo Nadhir Mayoka

Tukirudishwa studio tunapokelewa na Bujaga Izengo Kadago...

puumbav hakuna swedi mwinyi wala sijui maulid kitenge
 
mechi ya Simba na Villa mtangazaji alikuwa Charles Hillary na alipoanza kutaja kikosi cha Villa ilikuwa balaa kwani kabla hajafika kwa sentahafu kule mpira ulikuwa umeshaanza na ghafla akakatiza kutaja kikosi cha Villa kisha akapiga yowe la Goooooooooooooooo....halafu akasema ''namna gani pale...ni goal Kick...alikwenda vizuri sana pale Majid Musisi, lakini Frank Kasanga Bwalaya alisimama imara pale...namna gani pale Jamhuri kihwelu Mrema alikuwa kazubaa''....halafu akaendelea kutaja kikosi
 
respect mkuu
 
Mtanisamehe wakuu kama nitakuwa nimechanganya madawa!!! Nilikuwa toto tundu tu wakati huo kaka zangu hawakosi kusikiliza mpira.. Charles Hilary, Salim Mbonde, Ahmed sijui nani vile, Sekioni Kitojo... Dah, wazee wakitangaza hao mpira kama unauona live vile!
 
mechi ya Simba na Villa mtangazaji alikuwa Charles Hillary na alipoanza kutaja kikosi cha Villa ilikuwa balaa kwani kabla hajafika kwa sentahafu kule mpira ulikuwa umeshaanza na ghafla akakatiza kutaja kikosi cha Villa kisha akapiga yowe la Goooooooooooooooo....halafu akasema ''namna gani pale...ni goal Kick...alikwenda vizuri sana pale Majid Musisi, lakini Frank Kasanga Bwalaya alisimama imara pale...namna gani pale Jamhuri kihwelu Mrema alikuwa kazubaa''....halafu akaendelea kutaja kikosi

Safi sana Chomba '..Orodha na ushahidi kama huu'

Lengo la thread ni kuwaamsha watangazaji wa mpira kuboresha mbinu zao za utangazaji kwa ajili ya jamii.

Nitaomba mwongozo wa msimamizi wa forum hii namna anavyoweza kunisaidia kumpa zawadi Mtangazaji au mwakilishi wake atakayekuwa ametajwa zaidi ya wengine kupitia JF.
 
Brother MIKIDADI MAHMOOD, DUSTAN TIDO MUHANDO, AHMED JONGO, Hwa walikuwa kibboko cha utangazaji mpira enzi hizo za 70s Bila kumsahau ABDUL OMAR MASUD JAWEWA
 
Hawa ndio watangazaji wa mpira bora watatu Tanzania kati ya 1985-2011.
1.Sued Mwinyi
2.Jesse John
3.Hamed Jongo

Vigezo nilivyotumia
1. Kutochosha wasikilizaji.
2. kutokuonyesha upendeleo wa timu wakati wa kuzijadili kipindi cha mapumziko.
3.Kuonyesha uzalendo wa hali ya juu wakati wa mechi za kimataifa kwa vilabu au timu za taifa za Tanzania.

Ni maoni yangu binafsi. Wewe orodha yako ikoje?

Lengo ni kuboresha sasa ni " Watangazaji bora wa mpira Tanzania toka kuwepo fani ya utangazaji nchi hadi sasa"
 
Chacha Maginga wa TBC sema yeye ni mnazi wa Yanga...watangazaji wa zamani ilikuwa sio rahisi kujua wao ni timu gani.
 
ohhhhhhhh Dominic chilambo RIP alikuwa akikitangazia mpira ni kama msikilizaji unakuwa uwanajani.

Tena miaka hiyo ukizingatia wanatupwisa lindanda wana kawekamo yaani pamba walikuwa wanatandaza soka hasa. Timu nyingine ilikuwa inatandaza soka amabyo Chilambo likuwa anasema zinafanana na pamba ilikuwa Mecco na Ushirika Moshi.

Chilambo mwenyewe aliwai kusema kuwa mechi kati ya pamba na Mecco ndo zilikuwa zinamvutia.

Ahmed kipozi ingawa hakuwa akitangza sana sauti yake ilikuwa nzuri sana huyu alikuwa akitangaza kutoka dodoma
 
Wewe ndio mfuatiliaji wa Matangazo ya mpira.
Sio huyo mpayukaji aliyeanzisha thread.

Mpira bila Charles Hillary na Marehemu Omari Jongo haukusikilizika sheikh kwa watu wenye utimamu kichwani.

Wakati huo fundi mitambo kwenye caravan alikuwa Obi Mwambungu

Msimamizi wa matangazo Nadhir Mayoka

Tukirudishwa studio tunapokelewa na Bujaga Izengo Kadago...

puumbav hakuna swedi mwinyi wala sijui maulid kitenge

Yah Mkuu, hapo ni Charles Hillary, Ahmed Jongo, Salim Mbonde, Dominic Chilambo (huyu alikuwa balaa sana wakati anakupa kikosi kaMili cha wana kawekamo TP Lindanda-Pamba ya Mwanza, madata Lubigisa, na wenzie)

hapo fundi mitambo pia alikuwepo Noel Namaloe, Steven Kujumu na fundi Juma Kengele wakiwa kwenye gali lao la matangazo ile "Unimog"
 
mkuu unanikumbumbusha mtu mmoja anaitwa Fumo Felician Ferdinand. Leo nimeamini maisha bila jf haiwezekani
 
Mshindo Mkeyenge, mmoja katika watangazaji wazuri sana wa zamani. Enzi ambazo $pir tunausikiliza bila tv kama sasa, lakini, jinsi watangazaji walivyokuwa wazuri, hata uwanjani watu wakienda na redio ili wapate kuwasikia.
 
samahani tumesahau kosa kubwa la kifani ya uandishi wa habari hasa utangazaji wa mpira kuwa hutakiwi kuwa biased wala kumlead msikilizaji..pale wewe ni jicho na sikio la mtazamaji unatakiwa kumweka shamba la bibi msikilizaji aliye tandahimba huko....watangazaji wa siku hizi hakuna kitu hasa wa luninga..wanamdanganya mtazamaji wakati naye anatazama live,kukosea majina,namba wanazocheza wachezaji,hali ya hewa ya uwanja,idadi ya watazamaji,key players,rekodi za wachezaji hasa mchezaji akiwa kaumia au kafunga goli na hawawajui kwa kina wachezaji.....comments please
 
mechi ya Simba na Villa mtangazaji alikuwa Charles Hillary na alipoanza kutaja kikosi cha Villa ilikuwa balaa kwani kabla hajafika kwa sentahafu kule mpira ulikuwa umeshaanza na ghafla akakatiza kutaja kikosi cha Villa kisha akapiga yowe la Goooooooooooooooo....halafu akasema ''namna gani pale...ni goal Kick...alikwenda vizuri sana pale Majid Musisi, lakini Frank Kasanga Bwalaya alisimama imara pale...namna gani pale Jamhuri kihwelu Mrema alikuwa kazubaa''....halafu akaendelea kutaja kikosi

1993 kama sijakosea
 
nakumbuka mechi ya yanga na sigara ....early 1990s...sigara ikapigaa 3 dakika za mwisho...mtangazji akasema ...WAO TATU SISI BILA
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom