Wataalam ebu mtujuze je, serikali inaweza kutumia Sh 98 bilioni bila idhini ya bunge?

Gosbertgoodluck

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
2,855
401
Wandugu,
Wengi wenu mmesikia kauli ya 'mtoto wa mkulima' kuhusu dowans. Siju kama nimemweleza vizuri, ni kama amesema suala la dowans kamwe halitarudi bungeni. Kwamba litaachwa lifuate mkondo wa sheria na mbaya zaidi inaonekana kama yupo tayari hela ilipwe. Ninachojiuliza, in case serikali imeamua kulipa kiasi hicho cha fedha, je, italipa dowans moja kwa moja au itabidi iitishe kikao cha bunge ipate idhini ya kutumia kiasi hicho fedha ambacho hakikuwepo kwenye bajeti?

Karibuni wataalam wa masuala haya mtujuze.
 
Back
Top Bottom