DOKEZO Wastaafu wa TAZARA tunasotea stahiki zetu huu Mwaka wa 20, Rais Samia tusaidie

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Mzazi wangu ni mmoja wa Wazee ambao wamestaafu utumishi katika Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA), mzee wangu na wenzake wengi waliostaafu Mwaka 2004, 2005 na 2006 hawajalipwa stahiki zao licha ya kufanya jitihada kubwa ya kushughulikia.

Naandika andiko hili kwa maelekezo ya Mzee wangu ambapo anachokisema ndicho nakiandika...

Mimi na Wazee wenzangu tupo zaidi ya 180 tumefanya jitihada kubwa tangu wakati huo hadi leo ikiwa ni takribani miaka 20 bila mafanikio huku Serikali ikituzungusha.

Wazee wachache ambao wana ndugu kwenye nafasi za juu Serikalini wao walifanikiwa kupata msaada na wakalipwa.

Waliolipwa walikuwa na ndugu au jamaa katika nafasi za Uwaziri na nyinginezo lakini sisi huku ambao naweza kusema ‘hatujuani na Wakubwa’ tumeambulia patupu bado tunateseka kufuatilia.

Kuna wenzangu kadhaa wameshapoteza maisha bila kupata stahiki zao, familia zao zimepambana nazo hazijafanikiwa.

Uhakiki wa madai yetu ulishafanyika na Serikali ikathibitisha tangu kipindi cha Rais Jakaya Kikwete hadi cha hayati Magufuli, ambapo tulionana hadi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ikathibitishwa kuwa tunatakiwa kulipwa lakini hilo halijatekelezeka.

Suala letu lilifika hadi Mahakamani tukashinda shauri, baada ya hapo tukaonana na Waziri Mkuu kuwasilisha malalamiko yetu, akatusikiliza na akatukabidhi kwa maafisa wake washughulikie lakini tangu wakati huo danadana zimekuwa nyingi.

Wengi wetu wanaendelea kuteseka, wengine wanaumwa, jasho letu tulilolitoa kwa ajili ya Taifa linapotea, tunamasononeko, familia zetu zinamasononeko dhidi ya Serikali yetu kwa hiki kinachoendelea.

Mara kadhaa nimewashawishi wenzangu twenden kwenye Vyombo vya Habari kueleza changamoto zetu, hawataki kwa kuwa wengi wetu ni Wazee wa CCM na wakereketwa hasa, wenzangu wanaamini tukisema kwa Waandishi tunaweza kukiharibia chama, jambo ambalo mimi napingana nalo kwa kuwa ukimya wetu ndio anguko letu hadi tunakufa.

Taarifa zilizopo ni kuwa fedha tunazotakiwa kulipwa zipo Hazina na kuna wakati inadaiwa zimekuwa zikitoka na kurejea, kwa maana zinaingia katika matumizi mengine kisha zinarejeshwa.

Tumejuaje hilo? Harakati hizi za kwenda huku na huku zimetuwezesha kukutana na baadhi ya watu wa karibu na Mamlaka za juu wa Serikali ambao wanajua sakata hilo na wamekuwa wakitudokeza kuhusu hilo, kama ni kweli au la hilo sina uhakika.

Sisi Wastaafu wengi tuna hali mbaya sana kiuchumi, wengi tupo Dar na wengine wapo mikoa tofauti, tumeenda huku na huku bila mafanikio, yaani kwa ufupi tunatapatapa na imekuwa kawaida kuombaomba nauli kwa watu tofauti, ni aibu lakini hatuna jinsi.

Inaniuma sana kuona Watanzania tuliopambana kwa nguvu zetu zote kwa ajili ya Taifahiki haya ndio matunda.

Tumaini letu pekee limebaki kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwani kauli yake inaweza kuwa na nguvu ya kuweza kutusaidia kupata haki yetu.
 
Serikali ya CCM inafahamika vyema kihistoria kwa dhuluma dhidi ya hela za wastaafu. Ilianza tabia hii tokea enzi za utawala wa awamu ya kwanza.

Tulishuhudia kilio cha wazee wa iliyokuwa EAC ya awali. Wakati wenzao wa nchi za Kenya na Uganda wakilipwa mafao yao tena ndani ya wakati, wastaafu wa Tanzania wao waliambulia patupu. Licha ya kufuatilia kwa miaka nenda rudi waliishia kupewa porojo tu.

Angalia madeni yaliyokithiri na yasiyolipika ya serikali katika mifuko ya hifadhi za jamii. Mifuko hii imegeuzwa na serikali kuwa kama shamba la bibi pale inapokabiliwa na uhaba wa fedha za kuiendesha na kufanya anasa.

Angalia suala zima la kikokotoo. Wakati watawala wakijilipa mafao ya kukufuru, wastaafu wengine wanalipwa mafao kiduchu tena kupitia michakato iliyojaa mlolongo mkubwa.

Hawa wazee wanaolalamika hii leo, waliwahi kuwa vijana katika miaka yao ya kutesa. Walipita barabani huku wakiringa na kujidai kuwa wao na CCM ni damu damu, na tena wapo tayari kukilinda kwa gharama yoyote na hata kukifia chama chao.

Sasa leo kiko wapi! Walisaliti mapambano ya kutaka kuleta mageuzi, sasa hivi wanatafuta huruma kutoka kwa watesi wao walewale wa siku zote. Hali inajirudia hata katika nyakati za sasa, wakati watu makini wanapaza sauti zao, za kutaka katiba mpya, kuna watu wenye vichwa vigumu wakiwemo chawa maarufu ambao wanafahamika vyema hata ndani ya mitandao karibu yote ya kijamii, kwa makusudi wanajitoa ufahamu na kujifanya haelewi dhuluma inayofanywa na watawala, huku wakileta kejeli na dhihaka dhidi ya takwa hili nyeti na la wakati.

Wao pia ni wastaafu watarajiwa. Na itafika muda nao watakuja kuwa na kilio hiki hiki kama cha wenzao. Utakuja wakati ambapo watawala mafisi maji wa CCM watakuwa wakijilipa mabilioni ya fedha na wenzi wao, pamoja watoto wao, wao watakuwa wanalia na kusaga meno.

My friend, shetani hana rafiki. Tambua kuwa kila kitu kina gharama zake, iwe mbaya ama nzuri, Lakini uamuzi unao wewe mwenyewe ili kuweza kulipia hiyo gharama. Fanya uamuzi sahihi hii leo, mwaka huu wa 2024 ama mwaka kesho 2025, mchague shetani na mtesi wako ili muyajenge pamoja nae, ama la, chagua kesho yako iliyokuwa bora wewe mwenyewe pamoja na watoto zako
 
Kama Kweli.Raisi Awalipe hao watu yeye anasema ni mtu wa haki hapendi dhuluma.Kama aliwalipa wenye vyeti feki sababu japendi dhuluma awalipe hao wazee wa Tazara haki yao.Hao wana haki kuliko hao wa vyeti feki
 
Waende tu kwenye vyombo vya habari, na wamechelewa sana.

Bila hivyo hawawezi kupata kitu, danadana huwa haziishi nchi hii
 
Miaka ishirini iliyopita hata thamani ya hiyo pesa kwa sasa ni mitihani.

BTW:Na wastaafu wengi tu wa toka 2019 walilipwa pungufu nao wanasotea mapunjo huku serikali ikigharamia mashabiki wa Simba&Yanga kusafiri na timu zao.

Mchengerwa agiza Halmashauri zote zinazodai was na wastaafu walipe au DEDs watakaoshindwa wakae pembeni.
 
Mzazi wangu ni mmoja wa Wazee ambao wamestaafu utumishi katika Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA), mzee wangu na wenzake wengi waliostaafu Mwaka 2004, 2005 na 2006 hawajalipwa stahiki zao licha ya kufanya jitihada kubwa ya kushughulikia.

Naandika andiko hili kwa maelekezo ya Mzee wangu ambapo anachokisema ndicho nakiandika...

Mimi na Wazee wenzangu tupo zaidi ya 180 tumefanya jitihada kubwa tangu wakati huo hadi leo ikiwa ni takribani miaka 20 bila mafanikio huku Serikali ikituzungusha.

Wazee wachache ambao wana ndugu kwenye nafasi za juu Serikalini wao walifanikiwa kupata msaada na wakalipwa.

Waliolipwa walikuwa na ndugu au jamaa katika nafasi za Uwaziri na nyinginezo lakini sisi huku ambao naweza kusema ‘hatujuani na Wakubwa’ tumeambulia patupu bado tunateseka kufuatilia.

Kuna wenzangu kadhaa wameshapoteza maisha bila kupata stahiki zao, familia zao zimepambana nazo hazijafanikiwa.

Uhakiki wa madai yetu ulishafanyika na Serikali ikathibitisha tangu kipindi cha Rais Jakaya Kikwete hadi cha hayati Magufuli, ambapo tulionana hadi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ikathibitishwa kuwa tunatakiwa kulipwa lakini hilo halijatekelezeka.

Suala letu lilifika hadi Mahakamani tukashinda shauri, baada ya hapo tukaonana na Waziri Mkuu kuwasilisha malalamiko yetu, akatusikiliza na akatukabidhi kwa maafisa wake washughulikie lakini tangu wakati huo danadana zimekuwa nyingi.

Wengi wetu wanaendelea kuteseka, wengine wanaumwa, jasho letu tulilolitoa kwa ajili ya Taifa linapotea, tunamasononeko, familia zetu zinamasononeko dhidi ya Serikali yetu kwa hiki kinachoendelea.

Mara kadhaa nimewashawishi wenzangu twenden kwenye Vyombo vya Habari kueleza changamoto zetu, hawataki kwa kuwa wengi wetu ni Wazee wa CCM na wakereketwa hasa, wenzangu wanaamini tukisema kwa Waandishi tunaweza kukiharibia chama, jambo ambalo mimi napingana nalo kwa kuwa ukimya wetu ndio anguko letu hadi tunakufa.

Taarifa zilizopo ni kuwa fedha tunazotakiwa kulipwa zipo Hazina na kuna wakati inadaiwa zimekuwa zikitoka na kurejea, kwa maana zinaingia katika matumizi mengine kisha zinarejeshwa.

Tumejuaje hilo? Harakati hizi za kwenda huku na huku zimetuwezesha kukutana na baadhi ya watu wa karibu na Mamlaka za juu wa Serikali ambao wanajua sakata hilo na wamekuwa wakitudokeza kuhusu hilo, kama ni kweli au la hilo sina uhakika.

Sisi Wastaafu wengi tuna hali mbaya sana kiuchumi, wengi tupo Dar na wengine wapo mikoa tofauti, tumeenda huku na huku bila mafanikio, yaani kwa ufupi tunatapatapa na imekuwa kawaida kuombaomba nauli kwa watu tofauti, ni aibu lakini hatuna jinsi.

Inaniuma sana kuona Watanzania tuliopambana kwa nguvu zetu zote kwa ajili ya Taifahiki haya ndio matunda.

Tumaini letu pekee limebaki kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwani kauli yake inaweza kuwa na nguvu ya kuweza kutusaidia kupata haki yetu.
Nafurahia msaatfu kuteseka kwasababu ndo hao walisababishia vijana wao wa Leo khali ngumu ya Maisha,(ndo walikuwa watunga Sera, wala RUSHWA, Wapiga vigelegele usalama wa TAIFA, watunga Sera). Leo vijana wanakosa shukran kwao kwasaba nao hawakuona kesho ya TAIFA lao . Huu utaratib ndo M40 pekee utakapo ibua vinyongo Kwa JAMII nakuweka vizur TAIFA. Tunateswa na imana kuwa serikali iko kwa maslah ya watu wake kumbe sio kweli NI kwamaslahi ya familia zao na mabeberu walifaidi nchi hii..tufika hatua ya kuwa tunaumizwa na matatizo yaliyoko Kwa jirani /IDARA,ofisi kwa uzalendo bwa kweli TAIFA litasshinda.
 
Back
Top Bottom