Inanambo
JF-Expert Member
- Jun 26, 2011
- 3,985
- 2,770
Huyu mzee anatumia defense Mechanism ya kulaumu Gazeti la Mwananchi ili waonekana wabaya. Awali alitakiwa kulipongeza gazeti hili kwa kutumia TAFSIDA kuficha kipindi chake cha Usingizi Bungeni. sisi tulimuona kwenye TV akiwa amesinzia kabisa wala hana taarifa na mchango uliokuwa unaendelea. Pili angepaswa kukiri kusinzia labda sababu ya UCHOVU na si kutumia wenzake na yeye mwenyewe kulaumu chombo hiki cha habari wakati alikuwa kweli anasinzia. wanaCCM bungeni hupenda sana kutetea hata mambo ambayo wananchi wanayaona si sahihi. Mzee Wasira acha hizo sisi tulikuona kwa macho kabla hata Mwananchi hajakuripoti. Siku mambo Utandawazi watu wamefunguka macho.