Wassira: Mnataka serikali za majimbo mnafahamu zilivyo na gharama au mnaigiza tu

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
6,273
6,637
Hoja ya serikari za majimbo inayopigiwa chapuo na CHADEMA haina tija.Tanzania ina ukubwa sawa na jimbo la Texas. Kuwa na majimbo yenye magavana, mabunge na mabaraza ya mawaziri ni kuongeza gharama za utawala. Bunge moja tunalalamika sembuse mabunge 20. Tuache kuigiza"

1677575854636.png

1677575691461.png

Huo msumari wa moto kweli, tunaposema wazee ni hazina tuelewane tu palipo na wazee haliharibiki jambo.

CHADEMA ni weupe sana kichwani, unapouzungumzia serikali unazungumzia mamlaka kamili yenye kila kitu ndani yake. Sasa wanajiokotezea vitu impractical mitandaoni wanataka ku practice kwetu
 
Ngoja nikae kwa kutulia nisome komenti zilizoenda skuli yaani za uchambuzi kulingana point ya mzee Masatu au nisome porojo hapa zinazotokana na hasira!.
 
Serikali za majimbo ni cheap zaidi kuliko muundo wa sasa.

Chadema inachosema ni kwamba hizi kanda za hivi Sasa ndiyo ziwe majimbo (mfano kanda ya ziwa yenye mikoa zaidi ya 5 ) iwe Jimbo moja.

Chukua hiyo mikoa 5 Ina wakuu wa mikoa 5, wakuu wa wilaya zaidi ya 40, maRAS 5 , maDAS 40, maDED 40, maDEO 40, maREO 5, maRPC 5, maOCD 40, wabunge 60, n.k

Serikali ya Jimbo ni cheap mno kuliko ilivyo hivi Sasa. Huyu mzee Wasira akili ishazeeka mwambieni apumzike.
 
Huo msumari wa moto kweli, tunaposema wazee ni hazina tuelewane tu palipo na wazee haliharibiki jambo.

CHADEMA ni weupe sana kichwani, unapouzungumzia serikali unazungumzia mamlaka kamili yenye kila kitu ndani yake. Sasa wanajiokotezea vitu impractical mitandaoni wanataka ku practice kwetu
Kenya vipi mbona kiduchu na bado ina majimbo
 
Huwa hata sisomi hoja za huyu mzee kwani alishapitwa na wakati muda mrefu sana! Sijui hana wajukuu wa kucheza nao!
 
Hoja ya serikari za majimbo inayopigiwa chapuo na CHADEMA haina tija.Tanzania ina ukubwa sawa na jimbo la Texas. Kuwa na majimbo yenye magavana, mabunge na mabaraza ya mawaziri ni kuongeza gharama za utawala. Bunge moja tunalalamika sembuse mabunge 20. Tuache kuigiza"

Hapo ndipo akili za CCM zilipoishia,
Wanataka watu wote wafikiri kama wao.
Wakubali kuwa CCM imeshagonga mwamba kuleta mawazo mapya kwao ni shida kwa vile Misingi yao inawakataza .CCm ni serikali 2 kuelekea 1
Wapinzani wanathani 2 kuelekea 3 zenye mamlaka kamili.
 
Huo msumari wa moto kweli, tunaposema wazee ni hazina tuelewane tu palipo na wazee haliharibiki jambo.

CHADEMA ni weupe sana kichwani, unapouzungumzia serikali unazungumzia mamlaka kamili yenye kila kitu ndani yake. Sasa wanajiokotezea vitu impractical mitandaoni wanataka ku practice kwetu
Kwani hili la serikali 3 au Mifumo ya Majimbo hakuna nchi zinazo practise duniani?
Wacheni kuwaziba watu macho.
Kama Nyinyi hamuoni wengine wanaona.
CCM Imefeli kuboresha Muungano wao wenyewe wataweza kutowa maoni kuhusu Majimbo?
 
Serikali za majimbo ni cheap zaidi kuliko muundo wa sasa.

Chadema inachosema ni kwamba hizi kanda za hivi Sasa ndiyo ziwe majimbo (mfano kanda ya ziwa yenye mikoa zaidi ya 5 ) iwe Jimbo moja.

Chukua hiyo mikoa 5 Ina wakuu wa mikoa 5, wakuu wa wilaya zaidi ya 40, maRAS 5 , maDAS 40, maDED 40, maDEO 40, maREO 5, maRPC 5, maOCD 40, wabunge 60, n.k

Serikali ya Jimbo ni cheap mno kuliko ilivyo hivi Sasa. Huyu mzee Wasira akili ishazeeka mwambieni apumzike.
Wassira ni wa kumwonea huruma tuu, mtu mwenyewe anakokotwa kama Plau.
 
Hoja ya serikari za majimbo inayopigiwa chapuo na CHADEMA haina tija.Tanzania ina ukubwa sawa na jimbo la Texas. Kuwa na majimbo yenye magavana, mabunge na mabaraza ya mawaziri ni kuongeza gharama za utawala. Bunge moja tunalalamika sembuse mabunge 20. Tuache kuigiza"

Majimbo yatasababisha mgawanyiko na hata kutaka kujitenga. Tumeona Ethiopia vita kali ya kutaka kujitenga jimbo la tigray kaskazini ya nchi hiyo. Pia Nigeria hakuna usalama wala utawala bora kutokana na majimbo. Huku mashariki majimbo yaliyowahi kupigana vita ili kujitenga na kuunda nchi ya biafra kwenye miaka ya 60 leo yameanza tena kupigana kutaka kujitenga.
 
Back
Top Bottom