Wassira azidi kumng'ang'ania Bulaya Ubunge wa Bunda, Wafuasi wake wakata rufaa

Waendelee kukata rufaa mwisho watakatika wenyewe,Wassira amekataliwa na wananchi.
 
Mzee akalee wajukuu jamani,kipindi cha nyerere alikuwepo, kipindi cha mwinyi alikuwepo,kipindi cha kikwete alikuwepo ,na cha huyu ngosha anataka,jamani alizokusanya miaka hiyo yote hajatosheka???
 
Huyu mzee hafai hata kidogo,hapa amechungulia upepo wa mahakama na serilikali .Hapo nisawa na kugonga hodi kimyakimya aone jp atamfungulia?

Ni haibu sana kwake na familia yake.TOKA ENZI ZA NYERERE HADI LEO JPM BADO UNAN'GAN'GANIA UBUNGE?ACHA DAM CHANGA ZIFANYE KAZI.
 
Wapiga kura wanne wa Jimbo la Bunda waliofungua shauri kupinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliopita wameendelea kumng’ang’ania mbunge wa jimbo hilo, Ester Bulaya kwa kukata rufaa kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu wa kutupa maombi yao.

Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Francis Kabwe alisema Jumatano hii kuwa rufaa ya wapiga kura hao, Magambo Masato, Matwiga Matwiga, Janes Ezekiel na Acetic Malagila iliyosajiliwa kwa namba 199 ya mwaka 2016, itasikilizwa mfululizo kuanzia Februari 20.

Alisema rufaa hiyo itasikilizwa jijini Mwanza na jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufani, Salim Mbarouk, Augustine Mwarija na Shabani Lila.

Katika maombi ya msingi waliyofungua Mahakama Kuu, wapigakura hao wanaowakilishwa na Wakili Constantine Mutalemwa, wanaiomba Mahakama kutengua ushindi wa Bulaya dhidi ya aliyekuwa mgombea wa CCM, Stephen Wasira kwa madai kuwa uchaguzi wa Oktoba 25, mwaka 2015 haukuwa huru na wa haki.

Pamoja na madai mengine, Masato na wenzake wanadai kuwa mchakato wa kampeni, upigaji kura na utangazaji wa matokeo uligubikwa na ukiukwaji wa sheria na utaratibu wa uchaguzi, vikiwamo vitendo vya rushwa, msimamizi wa uchaguzi kumnyima haki Wasira kwa kukataa ombi lake la kura kuhesabiwa upya.

Novemba 17, mwaka jana, Jaji Noel Chocha wa Mahakama Kuu alimtangaza Bulaya kuwa mshindi halali wa uchaguzi huo baada ya kutupilia mbali maombi ya wapigakura hao.

Chanzo: Mwananchi
hakuna cha wapigakura wake wala washabiki wa huyo mzee yy mwenywe mzee wa usingiz na kufunga vishkizo sawasawa ndiye anayesimamia hiyo kesi sema anaona soo kujiweka front
 
Bulaya hamuwezi wassira kwa ligi.
Wassira kiboko yake warioba.Warioba aliweza kusimama na Wassira akitetewa na Proffessor Juan Mwaikusa,akamponda ponda Wassira,hadi akazuiwa na kugombea uongozi miaka 10.Huyu Bulaya sidhani kama pumzi hizo anazo
 
WanaJF tumtafute member mwenye hekima amtafute mzee Wassira amuombe apumzike.Tena aseme ametumwa na watanzania zaidi ya 300,000 waliopo JF.
 
Kuna Kila Dalili Za Wasiiira Kushinda, Anaweza Pindua Kiaina Si Unawajua Hawa Kijani Kwa Figisu Na Vile Dada Ester Anavyowaumbua, Wanaweza Kumsupport Wasiira kwenye figisu...MARK MY WORD!!
 
u
Wapiga kura wanne wa Jimbo la Bunda waliofungua shauri kupinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliopita wameendelea kumng’ang’ania mbunge wa jimbo hilo, Ester Bulaya kwa kukata rufaa kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu wa kutupa maombi yao.

Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Francis Kabwe alisema Jumatano hii kuwa rufaa ya wapiga kura hao, Magambo Masato, Matwiga Matwiga, Janes Ezekiel na Acetic Malagila iliyosajiliwa kwa namba 199 ya mwaka 2016, itasikilizwa mfululizo kuanzia Februari 20.

Alisema rufaa hiyo itasikilizwa jijini Mwanza na jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufani, Salim Mbarouk, Augustine Mwarija na Shabani Lila.

Katika maombi ya msingi waliyofungua Mahakama Kuu, wapigakura hao wanaowakilishwa na Wakili Constantine Mutalemwa, wanaiomba Mahakama kutengua ushindi wa Bulaya dhidi ya aliyekuwa mgombea wa CCM, Stephen Wasira kwa madai kuwa uchaguzi wa Oktoba 25, mwaka 2015 haukuwa huru na wa haki.

Pamoja na madai mengine, Masato na wenzake wanadai kuwa mchakato wa kampeni, upigaji kura na utangazaji wa matokeo uligubikwa na ukiukwaji wa sheria na utaratibu wa uchaguzi, vikiwamo vitendo vya rushwa, msimamizi wa uchaguzi kumnyima haki Wasira kwa kukataa ombi lake la kura kuhesabiwa upya.

Novemba 17, mwaka jana, Jaji Noel Chocha wa Mahakama Kuu alimtangaza Bulaya kuwa mshindi halali wa uchaguzi huo baada ya kutupilia mbali maombi ya wapigakura hao.

Chanzo: Mwananchi

mambo ya fainali uzeeni, Wasira hana cha kufanya kwa sasa, hana issue hana hela na umri unamtisha, tujipangeni na sie
 
Kwani mzee "Tyson" kulikoni alikua hajajiandaa vizuri kukipiga mtaan au kuna nini nyuma ya Pazia mana si kwa kukomaa namna hyo au kuna maelekezo nini? Faza tulia lea wajukuu ikiwezekana fungua kanisa uwe mchungaji bas maji yashakuacha hayo....
 
Back
Top Bottom