Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 18,330
- 33,958
Tangu enzi za wizi wa Tangold na Meremeta, wizi wa fedha za Tegeta - Escrow na hata sasa wizi unaonekana kwenye Ripoti ya CAG, kila hatu ya wizi huo wahusika wakuu huwa ni wasomi wabobevu wa fani mbali mbali.
Swali linaloibuka ni kwamba wasomi wetu wanaisaliti nchi kwa kushindwa kutumia elimu waliyo nayo kwa maslahi ya nchi, au CCM ambao ndiyo wako madarakani wanawatumia wasomi wetu kuifilisi nchi?
Kuna kisa kimoja cha kweli cha mwanasiasa mmoja wa CCM mpenda kunyoa upara, kuwa wakati wa Kampeni za uchaguzi za Mwaka 2015 alikwenda kwenye chuo Kikuu kimojawapo cha Serikali na KUTAKA apewe shilingi milioni 60 kwa ajili ya Kampeni za CCM. Makamu wa Mkuu wa Chuo wakati huo aliomba apewe siku mbili awasiliane na wenzake, lakini bwana mkubwa huyo alitoa saa moja tu apewe hizo fedha.
Busar wa chuo alimwambia Makamu Mkuu wa chuo atoe hizo hela kwani akikataa hao jamaa wanao uwezo wa kumtoa yeye na kumteua mwingine ambaye atakuja kuwapa hizo hela. Mnyoa upara yule alipewa zile milioni 60 na kutokomea nazo. Mtaka hela msomi, mtoa hela msomi,lakini wote hawakufuata taratibu za fedha za chuo husika. Tatizo ni nini?