Elections 2010 Wasiwasi wangu kwa Chadema !! ??

MPadmire

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,928
3,225
Kwanza napenda kusema kuwa nimefurahishwa sana na DK Slaa kugombea Urais, yaani siwezi kuelezea furaha yangu.

Kwanza nimewaambia ndugu zangu wote kama kumi na zaidi KURA kwa Dr Slaa.

Ila nina wasiwasi na hila za ccm, wasije kusema ameanza kampeni- wakamchongea kwa Tendwa na NEC.

Pia naongelea kuhusu Mgombea Ubunge Jimbo La Arusha. Sijui kuna mgombea gani anaeaminika, asiyenunulika. Naogopa isije akawa kibaraka wa ccm, akaja kujitoa baadae ili kumuachia mmbunge wa ccm ashinde.

Naomba ufafanuzi wa kisheria ili hofu yangu iondoke
 
Mpadmire,
kinachotakiwa ni CHADEMA kupata mawakala wazalendo na waaminifu, Mimi na wewe tuna jukumu kubwa la kuhakikisha kura haziibiwi safari hii.
Kuna haja ya Chadema kuanza kufanya mipango ya kuwapata Mawakala waaminifu kuanzia sasa hivi. mimi niko tayari kufanya hivyo kwa kujitolea katika eneo langu, maana safari hii ushindi ni lazima.
 
Cha maana ni wananchi wote kuamka.
Tuendelea kuwaelimisha wananchi kazi ambayo naifanya kila siku; naibua mijadala mbalimbali kuhusu hali yetu ya maisha na namna ya kutoka katika utumwa huu wa umasikini. Njia mojawapo ni kushiriki katika kupiga kura. Pia kuwatafuta mawakala ambao ni waaminifu;
 
Back
Top Bottom