Wasiovaa pete za ndoa kunyimwa komunio

Fidel80

JF-Expert Member
May 3, 2008
21,947
4,445
WAUMINI wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mpanda waliofunga ndoa kanisani wametakiwa kuvaa pete zao za ndoa muda wote, ili kuendeleza kiapo cha Agano Takatifu la Ndoa, la sivyo hawataruhusiwa kupokea Komunio Takatifu kanisani humo.

Uamuzi huo umetolewa na Paroko Msaidizi wa Kanisa hilo, Padri Cletus Bafumeko, wakati akitoa mahubiri yake katika Ibada ya Jumapili iliyopita.

Huku akishangiliwa kwa vigelegele na waumini waliofurika kanisani humo, Padri Bafumeko alitoa karipio kuwa atahakikisha katika kila ibada, wanandoa wote wasio na pete zao za ndoa vidoleni, wanazuiwa kushiriki Sakramenti Takatifu.

Alisema amelazimika kutoa karipio hilo, kutokana na tabia ya waumini wengi wenye ndoa, kuzoea kuacha pete zao za ndoa wanapokuwa mitaani. Kwa mujibu wa Padri Bafumeko, lengo la waumini hao ni kuonekana mbele za watu kuwa hawana wenzi waliofunga nao ndoa kwa lengo la kujitafutia ‘nyumba ndogo’.

“Sasa tabia hiyo imeendelea kukomaa katika jamii ya waumini wengi wa Kanisa hili na hata wa makanisa mengine, kushindwa kushika kiapo cha Agano Takatifu la Ndoa, kwa kukwepa kuvaa pete za ndoa vidoleni na kusababisha maadili ya ndoa kuporomoka katika jamii.

“Imekuwa sasa kama ni tabia ya waumini wa Kanisa hili, hususani wanandoa, kuvaa pete za ndoa wanapokuwa majumbani, lakini wanapotoka nje ya nyumba, pete huvuliwa na kuwekwa mifukoni au mikobani.

“Nimechunguza sana vidole vyenu ninapokutana nanyi wanandoa mitaani, nikaamua kuangalia hata mnapokuja hapa kanisani, hamvai pete zenu za ndoa kabisa, licha ya kuwa zimebarikiwa kabla ya kukabidhiwa kanisani, ni ishara ya kukosa uaminifu,” alisema Padri Bafumeko.

Alisema katika jamii nyingine, ishara ya kuvunjika ndoa ni kuvua pete na tendo la kuvua pete hiyo huwa ni mwisho wa uhusiano baina ya wanandoa hao.

Hivi karibuni, Kanisa Katoliki limekuwa likibuni mbinu mbalimbali za kurejesha maadili ya waumini wake, ikiwamo ya kuwavisha kaniki wanaokwenda kanisani na vimini, mavazi ya kuacha matiti nje na milegezo.

Parokia kadhaa za Kanisa Katoliki zilitangaza kuandaa mpango wa kuwavisha vazi la kaniki waumini hao ili kukomesha uvaaji mbovu unaokwenda kinyume cha maadili.

Paroko wa Msewe, Dar es Salaam, Padri Piero Clavero na viongozi wa Baraza la Walei katika Parokia hiyo ndio waliotoa tangazo hilo siku chache zilizopita.

Mwenyekiti Msaidizi wa Parokia, Benedict Fungo, alikiri kutolewa kwa tangazo hilo na kudai kuwa halina lengo la kumfukuza mtu kanisani, bali kurejesha nidhamu.

“Ni kweli tulitangaza, lakini hatukulenga kufukuza watu kanisani, lengo ni kurejesha maadili kwa waumini hasa vijana, unajua kanisani ni nyumba ya ibada, mtu anakwenda kupokea Ekaristi, ameacha matiti nje, wamevaa nguo zinaitwa za kupiga jeki, tukumbuke na mapadri ni binadamu jamani,” alisema Fungo.

Fungo, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Liturjia ya Parokia yenye dhamana ya kusimamia maadili, alisema baada ya tangazo hilo, yametokea mabadiliko makubwa na hakuna aliyevishwa kaniki hadi sasa.

Source:HabariLeo | Wasiovaa pete za ndoa kunyimwa komunio
 
Mpwa hapo nina mashaka kama wanaweza kulitekeleza hilo....sijaona uhusiano wa kuvaa pete na utayari wa kukomunika....hivi hapo anatumia sheria namba ngapi ya kanisa?
 
lol! wasiovaa pete utawajua tu!

Well, kweli its possible Mpanda na Mfaranyaki tu, manake inabidi umjue muumini na mkewe. Si ajabu ni senior bachelor ( boss wangu alifariki at 59 yrs old single and still searching!).

Haya mambo kanisa inabidi liyaangalie kwa mapana laweza kujipotezea mvuto watu wakatimukia kwenye ulokole.
Hivi pete inauhusianno gani na upendo wa mtu moyoni?
 
Dahhh kwa hiyo ukifika hapo mbele unapigwa maswali kwanza ..
Ni udhalilishaji kwa kweli.
 
Dahhh kwa hiyo ukifika hapo mbele unapigwa maswali kwanza ..
Ni udhalilishaji kwa kweli.

Hili linalishusha hadhi kanisa katoliki maaskofu waliangalie kwa mapana hakuna msafi duniani hapa
 
mchungaji kachemka,angetafuta njia nyingine si hiyo,watu wanavaa pete na bado wananyumba ndogo za kumwaga,bahati mbaya sana nyumba ndogo nyingi zinapenda wavaa pete.....
 
Wewe, hili haliwezi shusha hadhi
Akchwali linapandisha hadhi.

Sasa unataka upokee sakrament na mawaa?
Ni wajibu wa mapadri kujaribu kurudishwa wanakondoo wao kundini kadiri wawezavyo

Na hii ni kuwasisitiza waumini wavae pete zao za ndoa
Mbona kunyimwa kukomunika kwa kanisa katoliki ni kawaida kabisa?
Mfano, kama ukiongeza mke wa pili au pamanent small hausi

Hili linalishusha hadhi kanisa katoliki maaskofu waliangalie kwa mapana hakuna msafi duniani hapa
 
Wewe, hili haliwezi shusha hadhi
Akchwali linapandisha hadhi.

Sasa unataka upokee sakrament na mawaa?
Ni wajibu wa mapadri kujaribu kurudishwa wanakondoo wao kundini kadiri wawezavyo

Na hii ni kuwasisitiza waumini wavae pete zao za ndoa
Mbona kunyimwa kukomunika kwa kanisa katoliki ni kawaida kabisa?
Mfano, kama ukiongeza mke wa pili au pamanent small hausi

Nacho amini chini ya jua hakuna msafi hii ni ubaguzi wa kiroho kwani sote ni binadamu na ni wadhaifu
 
lol! wasiovaa pete utawajua tu!

Well, kweli its possible Mpanda na Mfaranyaki tu, manake inabidi umjue muumini na mkewe. Si ajabu ni senior bachelor ( boss wangu alifariki at 59 yrs old single and still searching!).

Halafu Mugglin, mbona sikujui/kufahamu hapa barazani? LOL

Mi nimeisikia asubuhi kwen gazeti mojawapo, nikashangaa sana. Ati Paroko msaidizi 'anakutana nao mitaani' ..hizi enzi ya mapadri kukaa parokiani haipo tena....wanarenda mitaani kuangalia 'nani amevaa pete, nani hajavaa, nani mwanandoa, nani sio' kisha jumapili 'wanakagua' kanisani 'kama huna pete, usikomunike'......hili linawezekana huko mpanda ndo maana nikauliza kwa sheria gani?

jambo jingine, wanawafilter vipi wenye pete lakini wanakomunika na huku wana nyumba ndogo...

whatever
 
wapendwa,

mi naona huyo paroko msaidizi hayuko mbali sana na ukweli.

pete ni ishara tu ya upendo na uaminifu wa mmoja wa wanandoa kwa mwezake hadi kufa. wakati wa kufunga ndoa, mchungaji anapompa mwanandoa pete husema maneno kama:

"pete hii iwe ukumbusho wa ahadi ya ndoa yako na pete hii iwe alama kwako ya kuwa mwaminifu kwa ndoa yako mpaka kufa"

na bwana/bibi harusi anapoipokea humwambia mwenzake maneno kama:

"pokea pete hii iwe ukumbusho wa alama ya ahadi ya ndoa hii na mimi na kuwa mwaminifu kwa ndoa hii mpaka kufa"

najua zipo sababu mbalimbali za baadhi ya wanandoa kutozivaa pete zao. baadhi ya sababu zinazokubalika ni pamoja na:

1.
allergy ya madini yaliyotengeneza pete hiyo,

2.
kunenepa kunakosababisha pete kubana mno kidoleni,

3.
kukonda kunakosababisha pete kulegea na hata kudondoka na kupotea,

4.
jeraha au kidonda kidoleni,

5.
kazi mbalimbali kama kufua nguo kwa mikono, kutandika kitanda (hasa wakati wa kuchomekea mashuka kwenye mifumbati na vitakizo) n.k. zinaweza kusababisha pete ikakukata na kukusababishia jeraha au kidonda

6. kupoteza ama kuibiwa

7.
sababu nyinginezo

kwa maoni yangu, imani na uaminifu wa mtu uko moyoni mwake na si kwenye kidole chake wala kwenye ile pete. ile pete ni alama tu na ishara ya nje. pete inaweza kuleta hamasa na kuchochea mapenzi zaidi kwa wanandoa kwa kuwa inaonyesha mwezio karidhika na wewe na hahangaiki huko nje, lakini bado si hakikisho la hayo. kuna watu wamezivua hizo pete siku nyingi sana lakini wamebaki waaminifu kwa wenzao. bila kutetereka

pia pete yaweza kuwa unafiki kwa wazinzi na watu wasio na heshima wala maadili kuivaa ili wapate kuheshimiwa na jamii kuwa wana familia ili watimize hila zao, huku ukweli ukiwa kinyume chake. mfano kuna wazazi wake kwa waume wana mapete makubwa ya gharama kubwa sana vidoleni huku hawana heshima kwa ndoa zaowala watoto wao, na wengine wamezitelekeza kabisa familia zao!

suala la kuivua pete ya ndoa bila sababu za msingi, ni sawa na kuivua alama ya uaminifu wako na hivyo ni sawa na gari kutolewa plate number kisha likaingia barabarani. gari kama hilo hata wewe ukikutana nalo barabarani unaweza kulitilia shaka, hivyo naona paroko ana haki ya kusema aliyoyasema, ila kwa kuwanyima hiyo komunio kwa hilo pekee naona kama linaleta changamoto kubwa hata kwa huyo paroko mwenyewe.

wapendwa, tujitahidi kuwa waaminifu kwa ndoa zetu hadi kifo kitutenganishe.

mbarikiwe sana

Glory to God!
 
Good Ms Judith, hapo ndipo na sisi tunasimamia kwamba pana mashiko kiasi gani? ndo maana naulizia namna ya utekelezaji wa hilo, na legitimacy yake kikanisa!
 
Hili linalishusha hadhi kanisa katoliki maaskofu waliangalie kwa mapana hakuna msafi duniani hapa
Hii imepitiliza sasa. Upate wale wenye imani finyu wanahama kanisa. Hata sikumoja Siamini kiongozi yeyote yule wa dini alazimishe watu kufanya Wao watakavyo ..
Zingatia hapo ni watu wazima sasa si watoto wa Sunday school. Hii imekaa vibaya sana.
 
Hakuna uhusiano kati ya pete na ndoa, mtu anaweza kuwa anavaa pete lakini ni mzinzi mkubw atu, ndiyo maana kanisani kwetu huwa hatuvalishani pete kabisa
 
Kuna waumini ambao wamekusudiwa katika azimio hili - vinginevyo ni "ubatili mtupu na kujilisha upepo.."
 
Hapo watachemka tu. Kwanza hakuna uhusiano wowote kati ya pete na ndoa, mtu anaweza kuwa anavaa pete na akafanya uzinzi akiwa na pete yake kidoleni. Mimi enzi hizo kabla sijampokea Yesu kwa kumaanisha niliwahi kufanya uzinzi na mwanamke akiwa amevaa pete, na wala alikuwa hashutuki. Yaani mpaka sasa unaniuma sana. Lakini namshukuru Mungu alinitoa katika shimo hilo la maangamizi.

Cha kufanya hilo kanisa liwafundishe vizuri watu kuhusu kuheshimu ndoa zao hata kama hawavai pete. Ila wokovu halisi ndani ya Yesu ndio suluhisho murua; hata mimi wakati huo nilikuwa Mkatiliki tena ex candidate for priesthood. Thank you my JESUS
 
Back
Top Bottom