Wasioishiwa pumzi ya kuupinga ufisadi tunakutana hapa!

meningitis

JF-Expert Member
Nov 17, 2010
8,349
4,674
Hii ni thread maalum ya wale wote wanaoukataa ufisadi katika mavazi yake yote.

Ni thread ya mashujaa wa kweli wanaopambana dhidi ya ufisadi hata pale unapojipa majina mapya!

Ni thread ya mashujaa na kwa ajili ya mashujaa wote waliosimama,wanaosimama na watakaoendelea kusimama dhidi ya mafisadi!

Ni thread ya waliopiga kelele na kuendelea kupiga kelele na watakaoendelea kupiga kelele dhidi ya mafisadi na ufisadi nchini Tanzania.

Ni thread kwa ajili ya waliowahi kuibuka,wanaoibuka na wayakaoibuka kuupinga ufisadi!

Ni thread ya kuunda umoja dhidi ya ufisadi uwe unatoka kwa CCM,CHADEMA,CUF au chama chochote au mwanasiasa yoyote anayesimama ipande wa ufisadi kwa nia yoyote ile.

Ni thread inayotambulisha maadui wakuu wa ufisadi Tanzania ili ikibidi historia iwahukumu katika hilo.

Ni katika thread hii ndio itatupasa kukumbushia aina ya ufisadi na mafisadi.

Ni katika thread hii tutatakiwa kuwataja na kuweka kumbukumbu na hukumu za kijamii dhidi ya mafisadi...yaani ukitajwa hapa ndio utakuwa umehukumiwa

Ni katika thread hii mtuhumiwa wa ufisadi ataweza kujitetea au kujisafisha.

Ni katika thread hii ushahidi wa ufisadi uyawekwa baada ya uthibitisho ukiwa na baraka za TCRA..

Hii iwe thread maalum ya mahakama ya kijamii ya mafisadi kwani sio serikali au vyama vya kisiasa vinavyoweza kuhukumu kwa haki na kutoa majibu ya nani hasa ni fisadi bali ni sisi pekee kama wana jamii forums ndio wenye mamlaka ya haki na huru na ya kimantiki ya kuhukumu mafisadi.

Thread hii iwe mwiba na eneo hatari kwa kiongozi kitajwa kwenye ufisadi.

Thread hii itumike kama laana ya kiongozi au yoyote yule awaye mtanzania kuhusishwa na ufisadi.

Orodha ya kweli na haki ya aibu (list of shame) iwekwe hapa.

Mods wawe na mandate ya kumfuta yule ambaye atasingiziwa ili tu aingizwe kwenye list yetu mpya ya ufisadi.

Thread hii isibebe Chama au mtu flani bali ibebe maslahi mapana ya nchi..!

Watu muhimu wenye michango yenye kura ya veto kwenye thread hii wawe kina ...

MzeeMwanakijiji Susuviri @Dr W.P Slaa Invisible na wengine ambao robot la JF litaona inafaa...

Let JF get back to its roots...!

Ni thread ya vizazi vyote vitakavyojiunga JF isiyoathiriwa na mihemko!

Thread hii iwe na gia moja tu isiwe na gia za angani au majini au ardhini..!!
 
Bila shaka wote tunapinga ufisadi na uovu mwingine wote unaowafanya watanzania wasisonge mbele kama taifa
 
Umeeleweka Mkuu na kazi ndiyo ianze sasa. Nadhani ni muhimu kutofautisha wale mafisadi walio nje ya siasa rasmi lakini indirectly they influence vyama na processes. Pili wanasiasa mafisadi
Tatu petty corrupt businessmen wanaofaidika na kutumiwa na wanasiasa.
 
Bila shaka wote tunapinga ufisadi na uovu mwingine wote unaowafanya watanzania wasisonge mbele kama taifa

Ufisadi ni zao la ccm na maraisi wake kama 2 walopita, na pia huyu ambaye anaomba ridhaa ya wananchi. Ufisadi si kupiga kelele jukwaani, ufisadi ni vitendo, na kama magufuli ataanza na mheshimiwa ambaye yuko sasa madarakani, ndo nitajua anapambana na ufisadi, otherwise ni bla bla tulizooea
 
Nashauri Mh Freeman Mbowe achukue fursa hii kukanusha tuhuma zilizozagaa kila kona ya nchi kuwa alipokea tsh 12 billioni kama gharama ya "kiingilio/registration fee" ya Lowassa chadema. Akishindwa kukanusha tuhuma hizo mbele ya jamii hii, nadhani tutakuwa tumetenda haki kama tukiifanyia amendment list of shame na kumuongeza Mh Freeman Mbowe
 
Wataongea sana sis hatudanganywi na maneno yapitao kama hewa ufisadi ccm ndo mama yake imeshachoka chagua mabadiliko
 
Kampeni yako nzuri ila umeianzisha kwenye kipindi kibaya sana.

Hizi kampeni za UFISADI zilishakufa hadi Lowassa alipohama kwenda UKAWA ndiyo zikaibuka na yeye kubebeshwa mzigo wote wa UFISADI kuanzia Escrow hadi ufisadi wa Bokhe Munanka (RIP) ambao ulijadiliwa sana hapa JF.

Wewe na Mzee Mwanakijiji ilitakiwa tuungane na Lowassa kwa sasa tuwaondoe CCM na baadaye ndiyo tuanza kusafisha zaidi ufisadi hata ule mdogo ingawa hata hivyo hatutaumaliza. Kumbuka The Great Helmut Kohl wa German na sifa zote alizojipatia, bado aliondolewa kwa UFISADI.

Sasa hivi kampeni zozote za kumpinga LOWASSA maana yake unamtaka Magufuli awe Rais.

Kama upo kwa Magufuli maana yake upo CCM na usituletee wimbo wa KUPINGA UFISADI wakati upo CCM.

attachment.php

Itakuwa vema hizi kampeni zikianza mwezi wa kwanza mwakani. Mwaweza kuungana na Zitto mkaleta Azimio la Tabora.
 
Nashauri Mh Freeman Mbowe achukue fursa hii kukanusha tuhuma zilizozagaa kila kona ya nchi kuwa alipokea tsh 12 billioni kama gharama ya "kiingilio/registration fee" ya Lowassa chadema. Akishindwa kukanusha tuhuma hizo mbele ya jamii hii, nadhani tutakuwa tumetenda haki kama tukiifanyia amendment list of shame na kumuongeza Mh Freeman Mbowe

Kumbe ni 12 Billioni?? Mimi nilikuwa najua ni 10 Billioni! Oh my God! kweli CHADEMA wanafiki sana.
 
Kampeni yako nzuri ila umeianzisha kwenye kipindi kibaya sana.

Hizi kampeni za UFISADI zilishakufa hadi Lowassa alipohama kwenda UKAWA ndiyo zikaibuka na yeye kubebeshwa mzigo wote wa UFISADI kuanzia Escrow hadi ufisadi wa Bokhe Munanka (RIP) ambao ulijadiliwa sana hapa JF.

Wewe na Mzee Mwanakijiji ilitakiwa tuungane na Lowassa kwa sasa tuwaondoe CCM na baadaye ndiyo tuanza kusafisha zaidi ufisadi hata ule mdogo ingawa hata hivyo hatutaumaliza. Kumbuka The Great Helmut Kohl wa German na sifa zote alizojipatia, bado aliondolewa kwa UFISADI.

Sasa hivi kampeni zozote za kumpinga LOWASSA maana yake unamtaka Magufuli awe Rais.

Kama upo kwa Magufuli maana yake upo CCM na usituletee wimbo wa KUPINGA UFISADI wakati upo CCM.

attachment.php

Itakuwa vema hizi kampeni zikianza mwezi wa kwanza mwakani. Mwaweza kuungana na Zitto mkaleta Azimio la Tabora.

Wewe unakubali wazi kabisa kuwa lowassa ni fisadi, lakini kwa akili zako za kimsukule unataka aende Ikulu halafu utapambana na mtu ambaye atakuwa tayari Ikulu wakati huo analindwa na katiba. Wakati huo yeye atakuwa anajua kuwa mtapambana naye halafu atawaacha tu mpambane naye kwa kuwapa nyenzo za kumuangamiza, kama vile katiba mpya???? Kama hivyo ndivyo mnavyofikiri, hakika ninyi UKAWA ni WAPUMBAVU wakubwa. So pathetic.
 
Pia sijaona mantiki ya kusema eti lazima kumsapoti Lowassa vinginevyo unamsapoti Magufuli! What a twisted logic! Wanataka kulazimisha jambo kwa nguvu?
Mi binafsi siwezi kumpa sapoti mtu kama Lowassa kamwe! Ni fisadi na wote hata Mbowe anajua!
Ajenda ya kupambana na ufisadi haikufa bali Mbowe tokea 2011 yuko na Lowassa kujaribu kuiua hoja hii. Ndiyo maana 2011-2015, Chadema ilijikuta inafuata matukio tu: mara kesi ya Zitto, Katiba mpya kisha Ukawa, nk
Lakini agenda ya ufisadi bado ina mashiko na inahitaji kusimamiwa ila siyo na Fisadi papa Lowassa!
 
Kwa hiyo tumpe nani ambaye siyo FISADI? Kama ni Magufuli, sioni tofauti yake na Lowassa na bado Magufuli alishasema "HATAWAANGUSHA...." Unategemea Magufuli amfunge Mkapa na au Kikwete? Keep dreaming.

11357011_509186502571148_1708925223_n.jpg

Dovutwa ni NANI? Hivi unasema ukweli au unatania? Hata Mzee Slaa anasema Magufuli ana afadhali ila siyo msafi pia.

Sasa kama pia si msafi, kwa nini kweli asiwe Dovutwa au Mama wa ACT? Mnaposema Hapana Magufuli au Lowassa, tuambieini sasa tumchague nani. Hii kusema tu hapana Lowassa kama MMM maana yake kwa wengi ni kuwa mchagueni Magufuli. Msimame kama WANAUME wa kweli na mseme mnamtaka nani na mtangaze waziwazi kama mnavyosema kwa Lowassa kuwa Magufuli pia ni Fisadi. Vinginevyo nyie ni team Magufuli au team Lowassa.

Ziku zimekwisha, mwakani Rais ni Magufuli au Lowassa tupende tusipende. Hii kuzunguka kujibaraguza eti Dovutwa sijui nani, ni kazi ya Wanawake au Mashoga. Wanaume choreni mstari na muhesabike mko wapi.

Mie sipo kwenye team yeyote ile hadi leo ingawa sifichi hisia kuwa SIIPENDI CCM. Ila kuanzia mwezi November, nitampa heshima zote yeyote aliyechaguliwa kuwa Rais wa Tanzania na ntakuwa tayari kumrarua Mkenya akija na kusema Lowassa aliji.... au Magufuli alikwenda kwa Babu wa Loliondo. Ntauwa mtu kumtetea Rais wangu wangu hata kama ni Dovutwa.

BTW: Usiku huu hamjalala, nyie mko wapi kweli? teteteteee......

Kama umechoka kweli basi bora umchague Dovutwa lakini siyo Lowassa ambaye ni part of problem not the solution!
 
Kwa hiyo tumpe nani ambaye siyo FISADI? Kama ni Magufuli, sioni tofauti yake na Lowassa na bado Magufuli alishasema "HATAWAANGUSHA...." Unategemea Magufuli amfunge Mkapa na au Kikwete? Keep dreaming.

11357011_509186502571148_1708925223_n.jpg

Hivi unataka maendeleo na kukomesha ufisadi au unataka kulipiza visasi na kufunga marais waliopita jela?
Sikubaliani na hoja ya kuwafunga marais jela ndiyo suluhu kwa ufisadi.
Lakini kujibu swali lako, labda niulize kati ya Mkapa na Lowassa nani fisadi mkubwa zaidi aliyetumia nafasi yake serikalini kujitajirisha sana? Jibu: Lowassa
Kati ya JK na Lowassa? Jibu: Lowassa
Huwezi kumweka Magufuli hata kwa mbali ligi mmoja na hawa wote, ye hana kashfa.
Tunahitaji mtu aliyejipambanua kuwa ameweza kuhimili vishawishi vya ufisadi. Ila kiukweli si mkamilifu. Lakini inapokuja ishu ya ufisadi na kuwa msafi Lowassa can never win! Hasafishiki hata kwa jiki!
 
Kwa hiyo tumpe nani ambaye siyo FISADI? Kama ni Magufuli, sioni tofauti yake na Lowassa na bado Magufuli alishasema "HATAWAANGUSHA...." Unategemea Magufuli amfunge Mkapa na au Kikwete? Keep dreaming.

11357011_509186502571148_1708925223_n.jpg
Kama ni kweli Magufuli alimuuzia mdogo wake nyumba ya serikali halafu hiyo pesa akaiweka mfukoni mwake au ilienda serikalini??? Magufuli alijitajirisha kwa mradi huu wa uuzwaji nyumba za serikali??? Acheni kudandia treni kwa mbele ninyi vilaza. Niambie wewe, utajiri alionao lowassa ambao unakaribia trilion 3 kwa mujibu wa mtoa mada mmoja hapa hapa JF, aliupata wapi utajiri huo??? Lowassa alipata wapi mali alizonazo leo hii hasa tukiangalia historia yake, baba yake hakuwa tajiri, yeye kapata wapi mali wakati alikuwa tu ni mtumishi wa umma????

Inakera sana kuona mijitu mizima inajiondoa ufahamu. Tutamchagua MAGUFULI sababu yeye ana afadhali mara milioni kuliko lowassa. CHAGUA MAGUFULI #HapaKaziTu
 
Nashauri Mh Freeman Mbowe achukue fursa hii kukanusha tuhuma zilizozagaa kila kona ya nchi kuwa alipokea tsh 12 billioni kama gharama ya "kiingilio/registration fee" ya Lowassa chadema. Akishindwa kukanusha tuhuma hizo mbele ya jamii hii, nadhani tutakuwa tumetenda haki kama tukiifanyia amendment list of shame na kumuongeza Mh Freeman Mbowe
Iko siku ushahidi utashushwa humu...nasikia hata jamaa zetu kina lissu na Mnyika na Msigwa pia.
 
Back
Top Bottom