Wasifu wa ndani Mh. Catherine Magige na nia yake ya 2015

Status
Not open for further replies.

Saranda

Member
Jul 4, 2012
53
8
Wanajamvi nilikuwa Dodoma nilikutana na Mh. Catherine Magige. 2015 ana ndoto ya kuwa Vice-President.

Je nani anajua elimu yake CV yake na hata utendaji kazi wake.

=======
images.jpg

Hon. Catherine Valentine Magige

Member Type : Special Seats
Constituent : Special Seats
Political Party : CCM
Phone : +255754440444
P.O Box : P.O Box , Arusha
Email Address : c.magige@bunge.go.tz
Date of Birth : 1981-05-08



Education History :

Dar es Salaam School of Journalism Advance Certificate of Journalism 2003 2004 Certificate

College of Business Education Certificate of Business Administration 2005 2006 Certificate

Ngarenaro Girls Secondary School CSEE 1996 1999 Secondary School

Kimandolu Primary School CPEE 1989 1995 Primary School

Employment History :

Bank M Customer Service 2007 2008

Barclays Bank Customer Advisor 2007 2009

Diamond Trust Bank Cashier 2006 2007

Political Experience :

Parliament of Tanzania Member of the Parliament 2015-2020

Constitution Assembly Member 2014 2014

Public Accounts Committee of the Parliament Member of the Committee 2012-2015

Minerals and Energy Committee of the Parliament Member of the Committee 2010-2012

Parliament of Tanzania Member of the Parliament 2010 2015

Chama cha Mapinduzi Member of the General Council of CCM Youth Wing-Arusha 2009-2009
 
Hii haijakamilika, aulizwe Katibu wa Bunge kwanini iko nusu sidhani kama Mheshimiwa Cath anahusika na mapungufu ya kuingiza data
 
Huyu atakuwa na Degree ya Mapishi kama ya Mbunge wangu wa Nkenge. Ukiona hivyo ujue chini hamna kitu
 
Usiyoyajua Kuhusu Catherine Magige-5


Anawahusudu Zitto, January Makamba
Tunaendelea kutazama yale ambayo kwa maana moja au nyingine ulikuwa huyajui kuhusu Mbunge wa Viti Maalum (CCM) anayewakilisha vijana (UVCCM) Mkoa wa Arusha, Catherine Valentine Magige.

Huko nyuma tumeshaangalia maeneo kadhaa, sababu ya yeye kuingia kwenye siasa, wito alionao katika kusaidia makundi mbalimbali kwa sababu mpaka sasa, ameonekana ndiye mbunge anayeongoza kwa kusaidia watu mbalimbali ndani ya kipindi kifupi.

Ukiachana na hayo, hivi karibuni gazeti hili liliendesha shindano la mbunge anayedatisha. Shindano hilo lililenga kumpata mbunge kijana mwanamke mrembo, anayejituma kufanya kazi, hivyo kuigusa jamii kwa sehemu kubwa kutokana na huduma anayoitoa.

Kutokana na mvuto wake pamoja na namna alivyojitoa kuisaidia jamii ndani ya kipindi kifupi, Catherine aliweza kufika hatua ya tatu bora, huku mshindi wa jumla akiwa Mbunge wa Kawe kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Halima Mdee.

Catherine anazungumziaje ushindi huo wa Halima na hatua ambayo yeye amefikia? Anasema: “Kwanza nampongeza Halima Mdee kwa ushindi, waliokuwa wanapiga kura ni Watanzania kutoka maeneo mbalimbali ya nchi, kwa hiyo anakubalika na utendaji kazi wake unaonekana.

“Pili namshukuru Mungu kwa hatua ambayo nilifikia. Unajua wakati shindano linaanza sikutegemea, ukichukulia mimi ndiyo nilikuwa naingia bungeni kwa mara ya kwanza, kwa hiyo nafasi hiyo imeonekana Watanzania wananiona na wanakubali utendaji kazi wangu.

“Hapa namaanisha kuwa pale hatukuwa tunapigiwa kura kwa urembo, kulikuwa na kigezo cha namna mtu anavyojituma katika kazi yake. Kingine ni kwamba napongeza shindano kwa sababu limetuweka karibu na Watanzania ambao ndiyo wapiga kura wetu.”

Mwakani utafanyika Uchaguzi Mkuu ndani ya CCM, je, Magige ana mpango wowote wa kugombea? Anajibu: “Hapana, sina mpango. Nahitaji kutumia muda wangu kuwatumikia wananchi kupitia ubunge. Jukumu nililonalo ni jipya, hivyo sitakiwi kuchanganya mambo mengi kwa wakati mmoja.

“Angalau ningekuwa mbunge kwa kipindi kirefu na kuona kama ninaweza kujigawa, kukitumikia chama kama kiongozi wa chama na mbunge, pia wakati huo huo kuwatumikia wananchi kama mbunge, hapo bila shaka ningekuwa na uamuzi wa moja kwa moja.

“Kuna watu wananishauri kugombea ujumbe wa NEC (Halmashauri Kuu ya CCM), mimi naona bado. Sidhani kama natakiwa kujitwisha kofia nyingi kwa sasa, ila mpaka mwakani nitakuwa nimeshajipima kuona kama naweza kugombea NEC. Ni suala la kuangalia na kusubiri, muda utazungumza.”

Wanasiasa ni watu wenye maadui wengi, vipi upande wake? Catherine anasema: “Maadui hawakosekani. Hata kama siyo mbunge, bado kuna watu watakuchukia na mara nyingi mtu anayekuchukia siyo lazima awe na sababu za msingi. Anaamua tu kuchukia.

“Kama kuna watu wananichukia, hilo siyo tatizo kubwa kwangu. Mimi nawaheshimu, namheshimu kila mmoja kwa sababu sitaki kuishi kwa ubaya na watu. Ni vizuri kama kuna mtu anahisi simfurahisi, aje aniambie kuliko kukaa na chuki. Kumaliza tofauti na mwenzako ni jambo jema mno.

“Mimi ni kiongozi, ninawakilisha wananchi bungeni, kwa hiyo sitakiwi kuishi kwa uhasama. Endapo nitaonesha chuki na mtu, hiyo ni alama ya kuwabagua watu ambao natakiwa niwawakilishe bungeni. Hivyo sipendi chuki lakini bado nasisitiza kwamba huwezi kuzikwepa kwa sababu wengine wanakuchukia bila sababu.”

ANAWAHUSUDU ZITTO NA JANUARY
Mbunge wa KIgoma Kaskazini (CHADEMA), Zitto Kabwe na yule wa Bumbuli, January Makamba ndiyo wanamkuna vilivyo Cathaerine, anasema: “Kuna sifa ambazo zinanifanya nivutiwe na mwanasiasa. Kwanza ni lazima awe na upeo, uzalendo, uadilifu, ujasiri na msimamo usioyumba.”

Source: Global Publishers 7th May, 2011
 
Hata ikiwekwa hiyo iliyokamilika hutaona tofauti na hii tunayoiona hapa. Waulize barclays wenzie waliowahi fanya nae kazi!
 
..Hebu bwageni humu ka-CV kake basi.
au ndio walewale dizain ya 'Kwema chepetu,' Vi..kamata'
aise Body linalipa bwana.... anapozungukwa na mafisadi malimbukeni ..unaweza kucheka hadi ufe
 
MBUNGE wa Viti Maalumu, Catherine Magige, amewalilia vijana kwa kuitaka serikali kuwajiri
wanaohitimu vyuo vikuu kwenda kutumikia mahakama mbalimbali nchini badala ya kuwaacha
wakihangaika mitaani.


Akichangia katika Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria, bungeni
Dodoma, jana, Catherine alieleza kwamba vijana wengi wanaohitimu vyuo vikuu kutoka fani ya
sheria wamekuwa wakihangaika mitaani na matokeo yake wengine kujiingiza kwenye mambo
yasiyofaa.

Alisema ugumu wa maisha wanaokumbana nao baada ya masomo unawafanya baadhi yao
kushindwa kumudu gharama za maisha na matokeo yake kujiingiza kukata tama kimaisha.

Hivyo, aliitaka serikali kuweka mpango ambao utakuwa unawajiri moja kwa moja kutokana na
kuonekana uhaba mkubwa wa watumishi wa mahakama, hali itakayosaidia wengi wao kupata
ajira kuliko ilivyo sasa.

Ni muhimu serikali kulitazama hili ili kuwasaidia vijana ambao wanajituma kusoma kwa bidii lakini
wanapohitimu masomo yao huishia kuzurura mitaani wakitafuta ajira bila mafanikio,alieleza.

Aidha, aliitaka serikali kuhakikisha inapunguza msongamano wa wafungwa magerezani kwa
kuharakisha kesi kuliko ilivyo sasa ambapo kuna mlundikao mkubwa wa keshi katika mahakama
nchini.

Kuwekwe utaratibu maalumu wa kushughulikia kesi hizo ili kupunguza mlundikano wa kesi
mahakamani, maana watu wanakaa kwa muda mrefu sana magarezani bila kutendewa
haki,alisema.

Aidha, aliwataka wabunge kuacha kuingilia mhimili wa mahakama kwa kuujadili bungeni, kwani
kufanyua hivyo ni kuvuka mpika ya bunge na matokeo yake kuingilia mhimili mwingine wa dola.
Lazima tuheshimu mihimili mingine, vinginevyo tunawezakujikuta tukifanya mambo ambayo
hayahusiani na kazi za bunge , kitu ambacho kitaleta picha mbaya ya bunge kuingilia mihimili
mingine,alieleza.

Pia, aliwataka vijana kujitokeza kwa wingi katika kutoa maoni ya mchakato wa katiba, kwani hiyo
ndiyo fursa pekee kwa vijana kutambulika katika katiba hiyo kuliko ilivyo sasa.

Alisema kwamba kushindwa kwa vijana kutoa maoni yao katika mchakato huo ni kupoteza fursa
adhimu ambayo haitapatikana tena kwa miaka mingi ijayo, hivyo kuwaomba kushiriki kwa wingi
katika mchakato huo wa kutoa maoni.
 
Huyu atakuwa na Degree ya Mapishi kama ya Mbunge wangu wa Nkenge. Ukiona hivyo ujue chini hamna kitu

Huyu mh. sijamsikia hata siku moja bungeni anatoa mada yoyote zaidi ya kuweka make-up, wadau watujuze zaidi dukuduku la kumuelewa zaidi
 
Ndio anasoma sasa degree yake elimu yake na alivyopitia ni story ndefu ......sanaa na inasemekana amekulia kwenye shida sana sana!
 
uzi wako umeandika 'wasifu wa ndani"nikafungua uzi fasta kujua umejuaje moyo ,figo,maini,kongosho,nyongo,utumbo n.k vya ndani vya mhe catherine maige?kumbe sio ulivyoandika!HA HA HAHAAAAAA!
 
Hata kama,naona sasa wengi mmezama katika maisha yake binafsi wakati mleta mada alitaka tuone nafasi au matarajio ya huyu mwanamama 2015.maisha yake binafsi hayatusaidii ,tunataka ubora wake kama mbunge.other wise i QUIT

viongozi wa kitaifa katika karne ya 21 hawaangaliwi tu kwa vyeti na uzoefu wa kazi bali pia na tabia binafsi kama hizi wanazoziweka hapa hawa wachangiaji..Africa tujifunze kuchangua viongozi kwa kuangalia na maisha binafsi ya nje ya uongozi. otherwise tutapata MADHAIFU wengi tu huko mbeleni
 
Catheline alisoma CBE miaka minne au mitano imepita Certificate, ila sikumbuki kama aliendelea Diploma au hakuendelea. WaCBE Miaka hiyo wanamjua.
 
Oooh my god!! My country is the area where the most stupid in the world come from. Ok! But why me is the most clever in the world? Oooh becouse i hate the wickness leaders especiall those who come thithiem.ok join with me to spread our camp peoples poweeeeeeeeeeeeer
 
wewe bwana hapo juu wacha kutudanganya cbe ajawahi kutia mguu labda cbe hotely unachanganya mbona wewe ulishawahi kumuona mazungumzo yake ? bungeni akifika yeye ni kutuma vikaratasi na kuongea ujinga kuna siku kidogo nimuabishe niliombwa sana na mtu nimuache lakini wana nchi watajionea huu uzembe siku moja utakwisha people powerrrrrrrrrrrrrrr
 
kweli umenena mgeni wetu jf imeingiliwa watu tunaomjua huyu dada hana hizo tabia nanimtulivu sana au kosa la Mungu kumpa uzuri? yaelekea watu wakiwa nachuki zao binafsi wanazileta huku. wana jf tubadilike natuwe tunafikiria siyo kukurupuka kupost mambo yaajabu nayasiyo nafaida kwetu sote badilikeni. nimesoma kuanzia mwanzo hadi mwisho niuzandiki na fitna huyu dada namfahamu sana nimtulivu naanajiheshimu. jf yupunguze majungu kunamambo mengi yakupost siyo majungu
 
Huko bungeni kuna kazi kweli kweli na mimi mwaka 2020 nachukua form ya kupata ubunge binafsi sheria ikipitishwa:happy:
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom