Wasifu: Huyu ndiye Dkt. Bashiru Ally

Wasifu wa Dakta Bashiru kwa hisani ya gazeti la Mwananchi.

=====

Huyu ndiye Dk Bashiru Ally​

Dar es Salaam. Miongoni mwa mambo yaliyoibua mjadala ni uteuzi wa aliyekuwa katibu mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally kuwa balozi na katibu mkuu kiongozi.

Ni uteuzi ambao haukutarajiwa uliokwenda sambamba na msomi huyo kuteuliwa kuwa balozi, wengi wanajadili uzoefu wake wakiamini anaweza kuitumikia vyema nafasi hiyo.

Uteuzi wa Dk Bashiru ulitangazwa jana Ijumaa Februari 26, 2021 na mapema leo Rais John Magufuli amemuapisha kwa mujibu wa katiba ya nchi na kuanza kutumikia upya wadhifa wake huo mpya.

Dk Bashiru Ally alizaliwa Januari mosi, 1968 katika Wilaya ya Bukoba vijijini Mkoa wa Kagera na kupata elimu ya msingi katika shule ya msingi ya Katerero wilayani humo kati ya mwaka 1980-86.

Mwaka 1987 alijiunga na shule ya sekondari ya Kilosa mkoani Morogoro alikosoma kidato cha kwanza hadi cha nne mwaka 1990 kabla ya kujiunga na shule ya sekondari ya Ihungo iliyopo Bukoba alikosoma kidato cha tano na sita na kumaliza mwaka 1993.

Mwaka 1997/98 alijiunga na Chuo kikuu cha Dar es salaam akisomea shahada ya kwanza sayansi ya siasa na kumaliza mwaka 2000 ambapo aliunganisha na kusoma shahada ya uzamili aliyomaliza mwaka 2002.

Mwaka 2003 aliajiriwa na taasisi ya Haki Elimu lakini mwaka huohuo alihamia Chuo kikuu cha Mzumbe ambako alifundisha kwa mwaka mmoja kabla ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kama mhadhiri msaidizi.

Akiwa chuoni hapo aliendelea na kusoma akichukua shahada ya uzamivu kuanzia mwaka 2011 hadi 2015.

Amewahi kuwa makamu mwenyekiti na kaimu mwenyekiti wa Chama cha kitaaluma cha UDSM (Udasa), makamu Mwenyekiti wa chama cha wanataaluma nchini.

Kabla ya kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM Mei, 2018 Dk Bashiru akiwa mhadhiri mwandamizi katika idara ya sayansi ya siasa UDSM vilevile alikuwa akiongoza kurugenzi ya mijadala na makongamano.

Ni mtafiti na mwandishi wa makala mbalimbali zilizochapishwa kwenye matoleo ya machapisho mbalimbali na kiitikadi amejipambanua kama mjamaa na mfuasi wa sera za hayati Mwalimu Julius Nyerere hata kabla ya kuweka wazi kuwa yeye ni mwanaCCM.

Kuhusu familia Dk Bashiru alioa kabla hata hajaanza kusoma chuo kikuu mwaka 1994. Yeye na mkewe Zulaika Hashim walijaliwa kupata watoto wawili wa kike, Halima na Hasanat.

Chanzo: Mwananchi
Yaani! Miaka yote hiyo mke mmoja tu. Huyu jamaa ana uzembe wa aina fulani eti. Watoto wenyewe ameshindwa kuwatengeneza! Yaani ubingwa wake ni mdomoni tu!
Mwambie awe na tabia nyingine, sisi ni waafrika, askali wa Magufuli.
 
Kwanini alichelewa sana kuanza darasa la kwanza? Miaka 12! At this age mimi ndiyo nilikuwa namaliza darasa la 7.
Ni kawaida, labda alikuwa na degedege. Pia alikaa miaka kadhaa kabla ya kujiunga na chuo kikuu. Lakini jiulize kwa nini aemwahi sana kufika hapo alipo leo hii! Just life roadway.
 
Kwanini alichelewa sana kuanza darasa la kwanza? Miaka 12! At this age mimi ndiyo nilikuwa namaliza darasa la 7.
Hao ndiyo zile design za enzi zile waliitwa repeaters. Wanarudia mara kibao mpaka wanafaulu. Inawezekana hata hilo Jina Siyo Jina lake halisi kama Jamaa yetu Mwigulu.
 
Wasifu wa Dakta Bashiru kwa hisani ya gazeti la Mwananchi.

=====

Huyu ndiye Dk Bashiru Ally​

Dar es Salaam. Miongoni mwa mambo yaliyoibua mjadala ni uteuzi wa aliyekuwa katibu mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally kuwa balozi na katibu mkuu kiongozi.

Ni uteuzi ambao haukutarajiwa uliokwenda sambamba na msomi huyo kuteuliwa kuwa balozi, wengi wanajadili uzoefu wake wakiamini anaweza kuitumikia vyema nafasi hiyo.

Uteuzi wa Dk Bashiru ulitangazwa jana Ijumaa Februari 26, 2021 na mapema leo Rais John Magufuli amemuapisha kwa mujibu wa katiba ya nchi na kuanza kutumikia upya wadhifa wake huo mpya.

Dk Bashiru Ally alizaliwa Januari mosi, 1968 katika Wilaya ya Bukoba vijijini Mkoa wa Kagera na kupata elimu ya msingi katika shule ya msingi ya Katerero wilayani humo kati ya mwaka 1980-86.

Mwaka 1987 alijiunga na shule ya sekondari ya Kilosa mkoani Morogoro alikosoma kidato cha kwanza hadi cha nne mwaka 1990 kabla ya kujiunga na shule ya sekondari ya Ihungo iliyopo Bukoba alikosoma kidato cha tano na sita na kumaliza mwaka 1993.

Mwaka 1997/98 alijiunga na Chuo kikuu cha Dar es salaam akisomea shahada ya kwanza sayansi ya siasa na kumaliza mwaka 2000 ambapo aliunganisha na kusoma shahada ya uzamili aliyomaliza mwaka 2002.

Mwaka 2003 aliajiriwa na taasisi ya Haki Elimu lakini mwaka huohuo alihamia Chuo kikuu cha Mzumbe ambako alifundisha kwa mwaka mmoja kabla ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kama mhadhiri msaidizi.

Akiwa chuoni hapo aliendelea na kusoma akichukua shahada ya uzamivu kuanzia mwaka 2011 hadi 2015.

Amewahi kuwa makamu mwenyekiti na kaimu mwenyekiti wa Chama cha kitaaluma cha UDSM (Udasa), makamu Mwenyekiti wa chama cha wanataaluma nchini.

Kabla ya kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM Mei, 2018 Dk Bashiru akiwa mhadhiri mwandamizi katika idara ya sayansi ya siasa UDSM vilevile alikuwa akiongoza kurugenzi ya mijadala na makongamano.

Ni mtafiti na mwandishi wa makala mbalimbali zilizochapishwa kwenye matoleo ya machapisho mbalimbali na kiitikadi amejipambanua kama mjamaa na mfuasi wa sera za hayati Mwalimu Julius Nyerere hata kabla ya kuweka wazi kuwa yeye ni mwanaCCM.

Kuhusu familia Dk Bashiru alioa kabla hata hajaanza kusoma chuo kikuu mwaka 1994. Yeye na mkewe Zulaika Hashim walijaliwa kupata watoto wawili wa kike, Halima na Hasanat.

Chanzo: Mwananchi
Tangazo tangazo kama wewe unatoka kanda ya ziwa kama
Bashiru, siro, magu, Biteko, mabeyo n.k
Karibu PM kunauteuzi niwafikirie
 
Miaka ile ili mtoto aweze kuingia darasa la Kwanza sharti mkono uguse sikio kupitia juu ya kichwa,ukiwa mfupi ndo Bas tena waweza Anza at 15,Miaka yenu hii hata miaka 3 mnaanza shule ndo maana kichwani ni shida tupu

Kwanini alichelewa sana kuanza darasa la kwanza? Miaka 12! At this age mimi ndiyo nilikuwa namaliza darasa la 7.
 
Ana bahati Sana cv yake ya kawaida Sana, hana hata experience ya kimataifa
Siku hizi Watanzania tulio wengi hatuwataki Viongozi wenye experience ya kimatifa, maana wengi wao wanaishia kua vibaraka wa Mabeberu na kuuza Rasilimali zetu kwa bei Chee kupitia Mikataba yao mibovu!!
 
Historia feki kabisa..
Mbona umaskip kua alikua mwalimu wa shule ya msingi?
Mbona umeskip kua ukoo wake wametokea huko kwenye vita...AWRNDA
Kabla ya kuwa Mkaguzi wa Mali za Chama na akazunguka Nchi nzima na kwenye matawi hivi hakutokea upinzani
watu wanajua kweli kutengeneza CV na kuziminya
 
Kwa hiyo ameteuliwa pia kuwa Balozi wa nini? /Nchi gani? Mnazidi kupeana tu ulaji huku wahitimu lukuki wakiwa wanahangaika tu mtaani.
Uchaguzi 2025 soon.. Jipangeni mshinde mfanye mnalo liona lina tija! Sasa tulieni na msitingishe kwani mkitingisha sindano itakatika tena..
 
Back
Top Bottom