Washika Mipini Mnawaisha Mazishi ya CCM!

Omutwale

JF-Expert Member
Feb 4, 2008
1,429
1,045
Bado najiuliza kwa nini "washika mipini" (Spika, Majaji, Mwanasheria Mkuu, Mawaziri, n.k) kwa maksudi wanachukua maamuzi ya kusiliba kaburi la ccm? Hakuna hata mmoja anajifunza kutokana na makosa yake ya awali au ya mtangulizi wake!

Tuliona la Dr. Slaa na EPA Bungeni mwaka 2007, CDM wakashinda kesi Mahakama ya Wananchi na bado wanazidi kuvuna riba ya makosa yalitokana na udhaifu wa Bunge la wakati ule. Ikaja mwaka 2008 Zitto akafukuzwa Ubunge, wimbi la ushindi wa kuungwa mkono na wananchi likaendelea kusimama upande cha CDM. Bunge jipya 2011 tumewabeza CDM na Katiba, leo hii tunafakamia matapishi yetu tukiwa chooni kwa wapinzani. Juzi juzi tu Jaji wa Mahakama katika kesi ya Uchaguzi wa Arusha, kwa kufikiri amefanya kazi ya kusifiwa na chama, kaleta balaa uraiani kwa kumuacha Godbless Lema alande lande nchi nzima. Sasa badala ya watu wa Arusha wavue magamba, nchi nzima hata watoto wanavaa magwanda. Bado tu hatujajifunza wala kuwafunza au kuwaeleza watoa maamuzi kwamba; chonde chonde kujipendekeza kwenu kwa nia ya kukinusuru Chama Tawala, serikali na Taasisi zake (Bunge, Uraisi, Mahakama) havisaidii bali ndo vinamwaga petrol kwenye tanuru la kuni kavu za zinazoiteketeza serikali! Wananchi wa Tanzania ya leo, si wa Tanganyika ya Mwaka 1947! Wana maamuzi rohoni mwao tayari kwa kiama cha serikali yao hapo mwaka 2015.

Ukiyatazama haya yote huwezi kuja na uamamuzi kama wa leo juu ya JJ Mnyika. Watoa maamuzi wa serikali yetu ya ccm lazima wajue kuwa hawa CDM wakati mwingine wanachezea sharubu za simba maksudi kwa sababu wanajua Simba mwenyewe ni wa plastiki. Na akibahatika kuwa na betri zenye chaji inayomwezesha kuunguruma basi ni furaha zaidi Maana watoto wa wana CDM wanafaidi muungurumo wake!

Hivi kuna upya gani katika neno "UDHAIFU" lililosemwa na Mnyika leo Bungeni? Mbona watu wengi sana ikiwemo viongozi wa Dini na Vyama vya Siasa wamelisema na kulirudia neno hili na wakilihusisha na Taasisi ile ile (Rais Kikwete) bila kuchukuliwa hatua yoyote?

Juzi Prof. Lipumba kasema wazi Rais JK ni dhaifu na kaenda mbali zaidi kumsifia Mkapa na utawala wake. Mh. Sitta akiwa Spika aliwahi kusema "kiutu uzima" kuwa "wewe rais umekuwa mpole mno" Hapa kwa wenye kung'amua Sitta alitumia uungwana tu kukwepa kutumia neno DHAIFU. Angeweza kusema "wewe rais umekuwa DHAIFU mno". Pia mwandishi Kondo Tutindaga – katika MwanaHalisi ya tarehe 01 June 2011 iliyobeba kichwa cha mada "Ni ubaya wa Lowassa au udhaifu wa JK?" alitumia neno "UDHAIFU" kama kisifa cha Rais JK si chini ya mara 15. Upya uko wapi mpaka huyo Spika anampa Mnyika kupiga penalti kwenye goli lisilo na golikipa?!

Hapa chini ni baadhi ya waandishi wachache tu miongoni mwa Watanzania lukuki waliosema hadharani UDHAIFU wa Rais Kikwete

Kondo Tutindaga
………..Hali ya nchi kwa sasa ni tete kisiasa, kiuchumi na hata kijamii. Wale wanaojipendekeza kwa Rais Kikwete ni wepesi kumshauri kuwa anayesababisha haya ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Na wengine wanamwambia sababu ni mapacha watatu. Hakuna anayemwambia rais kuwa udhaifu wake ndicho chanzo cha utete wa taifa…………

Nimemkumbuka Nyerere, angekuwepo, tusingefika hapa!. Tukiwaambia JK is a weak president, watu hawataki kukubali!. Hao masheikh wa kukundi cha Uamsho, wanakuwa tolerated under pretex ya religious tolerance hivyo kutenda vitendo vya jinai ya uhaini kwa muda mrefu na kuachwa hivi hivi wakiangaluwa!. Lakini wafuasi wao walipofanya jinai ya violence, ndipo wakakamatwa!. Kwa huu udhaifu wa JK, sasa sio tena CCM itamfia mikononi

Kondo Tutindaga
….. Lakini upo upande wa pili unaowakilishwa na udhaifu wa Kikwete kama Rais na mwenyekiti wa chama chetu. Rais na mwenyekiti mwenye udhaifu wa kiuongozi husababisha makundi ya watu wanaojipendekeza kwake au kujituma kufanya mambo ambayo yeye angefanya……..

…….Kwamba, udhaifu wa Kikwete ambao wakati mwingine unaitwa "uungwana wake" kwa vile unatendwa na mkuu wa nchi, ndio unaosababisha makada wachinjane, wauane, wakamiane, wasingiziane, na hatimaye waangamizane kisiasa……..

………Udhaifu wa Kikwete umelifikisha taifa mahali pagumu sana. Ili kurekebisha hali hii, gharama kubwa kisiasa na kiuchumi itatumika. Rais kwa hofu na aibu ya kusemwa sana na watu, anaweza kuzinduka na kuchukua hatua kwa jazba na hasira na kufanya makosa yanayoweza kuligharimu taifa kwa muda mrefu……….

Saed Kubenea
MwanaHalisi 30 November 2011
Kikwete, Lowassa hapatoshi


Baadhi ya wachambuzi wa mambo wanasema kauli ya Lowassa ambayo ilitolewa mbele ya viongozi wake wakuu, akiwamo rais mstaafu, Benjamin Mkapa, ililenga kuonyesha udhaifu wa Kikwete ndani ya CCM kwa kuasisi falsafa ya kujivua gamba na kuikimbiza moja kwa moja kwenye CC na NEC, kinyume cha taratibu na kanuni za chama chake.
 
Mkuu, Kikwete si kiongozi DHAIFU tu bali pia ni GOIGOI, kwa sababu hana uwezo au ni muoga wa kuchukua maamuzi kwa wakati. Wala huhitaji kusumbuka kutafuta references kwa ajili ya kuthibitisha hilo, maana hata mke wake na watoto wake wanalitambua hilo.
 
Na tunaomba waendelee kuzishika hizo mipini ili waendelee kuwaudhi watanzania.
Nimeona wabunge wengi baadhi wa ccm kila waliposimama waliiponda hotuba ya Zitto, kana kwamba ina kasoro, eti chadema wanawadanganya watanzania.
wamesahau kuwa bajeti ya upinzani haitaishia bungeni, itaenda kusomwa kwa wananchi ili wajue kuwa ccm ni wasanii, rais ni mdaifu, CCM ni wapuuzi nk.
Mbunge anapewa dk. 10 kuchangia, badala ya kuijadili bajeti kwa maslahi ya wananchi anabaki kuiponda chadema mpaka dk.10 zinaisha.
Mungu aendelee kuwafumba macho mpaka kieleweke!
 
Last edited by a moderator:
Omutwale Kuna vitabu vya hadithi wakati tukiwa lower school std i -iv kulikuwa na mfalme mmoja ambaye alitaka ashonewe suti ya kipekee isio na mfano kwa yoyote, kitu ambacho kiliwashinda mafundi wakamwacha mtupu na kumwambia suti yako tayari mwilini. Mfalme alizunguka mitaani akiwa mtupu ili kuonyesha suti yake mpya, na kwa woga wa raia hakuna aliethubutu kumwambia kuwa uko mtupu mpaka mtoto mdogo alipopiga kelele mbona mfalme hakuvaa nguo? Sasa basi nafikiri alichofanya Mnyika ni kumkumbusha mfalme kuwa hajavaa nguo na si zaidi ya hivyo maana kama mabvyo umeweka baadhi ya nukuu hapo juu watu wanajipendekeza hawawezi kumweleza kuwa udhaifu .
 
Last edited by a moderator:
Imewapasa wafanye hivyo kama walivyoagizwa na mkuu wa kaya kuwatoa nje wale wote watakao onekana kupinga na ole wao waingize neno ambalo litaweza kubadilishwa na jamii ikaamini kuwa ni tusi...

Sishangai kwani ndugu na jamaa wa marehemu wamekwishawasiri (CUF, TLP, UMD na sasa Mbatia wamemleta ili awe mshika chetezo kwa tiketi ya NCCR) kama ni kaburi tayari limekwisha chimbwa....:pray: MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI ALIPOJICHAGULIA, AMMMMEEEEEENNNN!!!!!!!
 
Omutwale Kuna vitabu vya hadithi wakati tukiwa lower school std i -iv kulikuwa na mfalme mmoja ambaye alitaka ashonewe suti ya kipekee isio na mfano kwa yoyote, kitu ambacho kiliwashinda mafundi wakamwacha mtupu na kumwambia suti yako tayari mwilini. Mfalme alizunguka mitaani akiwa mtupu ili kuonyesha suti yake mpya, na kwa woga wa raia hakuna aliethubutu kumwambia kuwa uko mtupu mpaka mtoto mdogo alipopiga kelele mbona mfalme hakuvaa nguo? Sasa basi nafikiri alichofanya Mnyika ni kumkumbusha mfalme kuwa hajavaa nguo na si zaidi ya hivyo maana kama mabvyo umeweka baadhi ya nukuu hapo juu watu wanajipendekeza hawawezi kumweleza kuwa udhaifu .

MANI

Umenikumbusha enzi za Zama za "Uwazi na Ukweli" Jenerali Ulimwengu aliamua kumweleza Che Nkapa kuwa "Mfalme uko uchi" adhabu yake akaambiwa "wewe si raia"

Ndiyo...tunahitaji watu wa kumueleza Mfalme jinsi sura yake ilivyo, maumbile yake na muonekano wake kwa watu wake. Inaniuma sana kila nikiongea na East Africana "wananisifia" eti Watanzania tuna Rais Handsome! Aibu iliyoje badala ya tusifiwe kwa kutumia vema utajiri wa rasilimali tulio jaaliwa kukuza uchumi, tunapakwa lipsticks na cosmetics kwa sababu ya udhaifu wa Wakuu wetu.
 
Last edited by a moderator:
Wajifunze Kenya ambako katiba yao inawataka waombe upya kazi zao kwenye tume huru, na wote waliojihusisha na matumizi mabaya ya madaraka na wizi mwingine, Tufike mahala tuwe waadilifu kwa manufaa ya nchi yetu
 
Angalia mh alivyotolewa chini ulinzi wa masajenti wa bunge
 

Attachments

  • 5.JPG
    5.JPG
    106 KB · Views: 54
  • 10.JPG
    10.JPG
    67.1 KB · Views: 50
Omutwale, well said mkuu. upinzani unapelekwa makida makida na chama tawala. Lakini huu ushabiki wa kinyambaf una mwisho wake.
Haya magamba yamekaa vikao mapema ili kutetea hiyo budget bila ya kuangalia masilahi ya Taifa. Matokeo yake akina Komba (mnyama anaepiga mnazi) anakurupuka na kuunga mkono bajeti 100% huku akisema jimbo lake ni masikini sana asaidiwe!!
unaunga mkono mavi!!! Wako brain washed kama members wa Mirembe!
B....shit!
Mnyika apige mawe kama kawa, after all, yupo ktk kibanda cha makuti, hakuna vioo!
 
Omutwale well said sir Maspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano,Wabunge wa CCM na Mawaziri hawajitambui jinsi wanavyoipaisha CDM
 
Power

Today 15:16
#3 JF Premium Member
premium.png
Array


Join Date : 20th April 2011
Location : Msoga Kijijini
Posts : 1,898
Rep Power : 740
Likes Received537
Likes Given37


[h=2]
icon1.png
Re: Washika Mipini Mnawaisha Mazishi ya CCM![/h]
Mkuu, Kikwete si kiongozi DHAIFU tu bali pia ni GOIGOI, kwa sababu hana uwezo au ni muoga wa kuchukua maamuzi kwa wakati. Wala huhitaji kusumbuka kutafuta references kwa ajili ya kuthibitisha hilo, maana hata mke wake na watoto wake wanalitambua hilo. (HATA MKE WAKE NA WATOTO?):llama:​
 
najiuliza ni aibu sana kushindwa kutoa tofasiri maalumu ya ya neno "dhaifu" ina maana ni tusi naomba wataalamu wa lugha tusaidiane
 
Watu wengi ni Dhaifu na viongozi wengi ni dhaifu But Sija wahi kumwona rais wa nchi DHAIFU kama Kikwete, Amefanya Nafasi ya urais itamaniwe na hata mazezeta wanaona wanaweza kuliko yeye. haku faa hata kuwa balozi wa nyumba 10
 
KIPOFU HAWEZI KUMUONGOZA KIPOFU MWENZIE MWISHO WA SIKU WOTE WATATUMBUKIA SHIMONI...
bubge limeamua kuizika ciciem makusudi kabisaaaaaaaaaaaa
 
Back
Top Bottom