Wasanii na Mitandao ya Wizi

majorbanks

JF-Expert Member
Feb 3, 2012
228
66
Wanajamii
Hivi karibuni kumeibuka wizi wa vifaa vya magari maeneo mbalimbali,especially jiji la Dar.Wizi huu umekuwa ukifanyika kwenya maeneo ya maegesho na hata majumbani nyakati tofauti tofauti.
Kuna jirani yangu aliibiwa vifaa vya gari yake usiku hivi karibuni na kwa kuwa jamaa anafahamiana na baadhi ya watu alifanya mawasiliano kiasi kwamba vifaa vyake vingefika popote Dar kwa ajili ya mauzo basi jamaa alikuwa na nafasi kubwa sana ya kujua.
Na ndivyo ilivyotokea,kwani kuna dada alienda kuuza huo mzigo mahali na ndipo jamaa akajulishwa na askari wakaenda mkamata dada huyo.Alipobanwa dada alitaja washirika wake ambapo miongoni mwao kulikuwa na wasanii maarufu nchini ambapo kwa sasa kama wamepoteza uelekeo katika kazi ya muziki.(to be specific mmojawapo ni Lord Eyez wa Nako 2 Nako)
Dada alifunguka zaidi na kusema pia wameshaiba mpaka silaha zilizokuwa zimeachwa kwenye magari kiasi kwamba mpaka muda huu dhamana hawajapewa kwa kuwa washaonekana ni watu hatari sana.
Wasanii mnapokuwa mnafanya kazi kwa mafanikio basi kumbukeni kuwekeza kwa maisha yenu ya mbeleni kwani muziki au sanaa zingine ni kazi zinazoendana na umri,ukishavuka umri fulani basi na wakati wako wa kung'aa nao unakwisha.
 
Mambo ya lord eyez yako mahakamani, haturuhusiwi kuingilia muhimili wa mahakama!
 
Back
Top Bottom