Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 13,505
- 51,109
Ni dhahiri ndani ya CHADEMA watu wanachekeana usoni ila mioyoni mwao watu wanapiga mahesabu ya 2025.
Baada ya uchaguzi wa 2020, Kamati kuu ya chama hicho ilitoa msimamo kuwa hakuna kushiriki uchaguzi wowote ujao bila uwepo wa Katiba mpya yenye Tume huru ya Uchaguzi.
Mwanzoni kabisa, msimamo huu ulitetewa kwa nguvu zote na makada na viongozi wa juu wa chama hiki. Lakini kadri siku zinavyosogea, Sura halisi ya viongozi hawa imeanza kuonekana. Wameanza kama kawaida yao kubadili msimamo huo taratiiib kwa kutuma meseji kuwa watashiriki ktk uchaguzi huo bila hata ya uwepo wa Katiba Mpya.
Hili limedhihirika katika ziara ambazo viongozi hawa wakubwa wa CHADEMA wataka ubunge wanazofanya mikoani. Sasa hivi hawaongei tena suala la kupatikana kwa Katiba Mpya kwanza ili kushiriki uchaguzi, Sasa hivi wanaongea namna watakavyorudi Bungeni mwaka 2025!
Hapo awali katika kutetea uamuzi wa kamati kuu wa kutoshiriki uchaguzi mkuu bila Katiba Mpya, walisema kuwa practically katika nchi hii haiwezekani kufanya uchaguzi huru na haki bila katiba mpya iliyobora kuliko ya sasa. Lakini cha ajabu ni kwamba CHADEMA sasa inadhani raia wamesahau "elimu" hii waliyoitoa, wanadhani raia mwaka 2025 wanaweza kuwachagua achilia mbali kujitokeza kwa wingi kushiriki uchaguzi ambao wameshaambiwa na haohao CHADEMA kuwa hauwezi kuwa huru na haki.
Kiongozi mkubwa wa CHADEMA aliyeshiriki kutoa elimu ya ubovu wa katiba ya sasa na kutofaa kwake katikauchaguzi ni Tundu Lissu, alifanya kazi hiyo kwa moyo mmoja na kwa weledi kabisa, Lakini inavyoonekana ni kwamba kuna kundi la viongozi wenzie ndani ya CHADEMA wanaona kuwa mwaka 2025 wana nafasi ya kurudi bungeni, na hawa ndo wanachombezachombeza kama siyo kushinikiza chama kiingie katika uchaguzi ili wapate ubunge tena ili wakalambe asali kama wenzao wa CCM.
CHADEMA inajulikana vyema kwenye kubadili gia angani, pale inapokana misimamo thabiti yenye maana na kukumbatia vitu vya kupita vyenye manufaa ya muda mfupi kwa nchi na chama chao. Walifanya hivyo pale walipoikana ajenda yao ya Ufisadi pale walipomkabidhi kijiti mtu waliyemuita fisadi kwa miaka zaidi ya Nane kuwa mgombea urais wa chama chao. Wao walikuwa wanawaza kutwaa madaraka tu kwa udi na uvumba bila kujali wanayetaka kumuweka madarani ni nani hata kama Chadema wanajua wazi kuwa ni fisadi na pia waliutangazia umma wao wenyewe hilo suala.
Leo wanatambua kabisa kuwa bila uwepo wa katiba mpya uchaguzi ujao bado utakuwa feki lakini wao kwa sababu wanadhani kuwa wana chance ya kurudi bungeni kula baada ya JPM kufariki, hata hizo conditions za kutoshiriki uchaguzi mpaka ipatikane katiba mpya yenye tume huru ya uchaguzi hawana mpango nazo tena.
Leo CHADEMA inasound kama chama cha ACT, viongozi wake wanasema kuwa ili washiriki uchaguzi "Mchakato" wa katiba uanze lakini Tuanze na Tume huru ya uchaguzi kwanza. Ningependa kuwauliza viongozi wa CHADEMA hasa Tundu Lissu, ni nani alimwambia kuwa "Mchakato wa katiba" ndo katiba mpya yenyewe?.
Pili nani kawawmbia CHADEMA kuwa uwepo wa mchakato wa katiba bila katiba mpya ndo guarantee ya Uchaguzi Huru na haki mwaka 2025?
Mimi ningewaona CHADEMA wako serious na wana nia njema kabisa ya kusimamia kile walichokitangaza kwa umma baada ya uchaguzi wa hovyo wa 2020 kwa kusema kuwa ni heri katiba ya sasa ibadilishwe, Uchaguzi wa 2025 usogezwe mbele, ili tutafute katiba mpya kwanza halafu sote tuje tushiriki uchaguzi chini ya Katiba Mpya iliyobora.
Lakini hizi habari za kuuambia umma kuwa bila katiba mpya uchaguzi hauwezi kuwa huru na haki halafu baadae baada ya Rais Samia kuanza kuwapetipeti wanakuja kutwambia jinsi Samia alivyo raisi mzuri na hivyo basi kubadili gia angani na kusema uchaguzi unawezekana chini ya katiba hii mbovu ni kuwacheza shere wananchi, kudharau wanachama wake na kutokujua unapigania nini.
CHADEMA imekuwa ikisema kuwa hata kama una tume huru ya uchaguzi lakini as long as hakuna mahakama huru, Jeshi la Polisi huru huwezi kupata uchaguzi huru na haki chini ya katiba hii. Nashangaa sasa wazee wa kubadili gia angani wameshasahau nondo walizokuwa wakishusha kuelimisha watu juu ya hili.
Watanzania makini tunasema, bila Katiba Mpya Uchaguzi wowote ujao ni feki.