Wasafi: Media House iliyokosa ubunifu yakinifu

Gini

JF-Expert Member
Oct 11, 2018
398
385
Wasafi, Media House iliyokosa ubunifu yakinifu!

Na Mwl Sylvester, George Wambura
Twitter @PGGeorgeJr Instagram @pg_georgejr
+255716109169
georgesylvester35@yahoo.com

Ukiiongelea Wafasi Media hukosi kumfikiria Diamond Platinumz ambaye kimsingi ndiye ameibeba clue yote ya wasafi. Bila shaka ni media house iliyotarajiwa na watu wengi kufanya makubwa sana hasa katika tasnia ya burudani. Inawezekana inafanya vyema ila sio siri kuwa Wasafi imekosa ubunifu yakinifu katika programu ama contents zao ambazo zinaonekana kama ni copy & paste kutoka kule wanakowachua watangazaji wake

Ubunifu ikiwa ni nguzo namba moja ya kufanya vyema na kukupa mileage, ukikosekana inakuwa taabu kweli kweli. Yamkini wana wataalam wa hizo mambo lakini wanonekana kazi yao hawaijui, sipo hapa kuwafundisha cha kufanya bali kama miongoni mwa wasikilizaji na mtazamaji wa Wasafi Radio na Tv,naona kama hiki kingefanyika basi Wasafi Media ingepiga bao sana kama inavyopiga bao Wasafi Music Label.

Walipowachukua akina Maulid Kitenge kutoka
E-fm nilijua wangekuja na kitu tofauti badala yake wameileta Sports HeadQuarter ndani ya wasafi fm, ni kama wameyachukua naudhui yote ya E-fm ya michezo na kuyahamishia kwao yaani Copy & Paste.Hakuna kilichobadilika, modalities ni zile zile, walichokibadilisha ni jina tu na kukiita Sports Arena badala ya Sports HQ.

Maudhui ya Maulid Kitenge ya usomaji wa magazeti ni ule ule, yaani amehamisha huku na kupeleka huku. Dida wa Mchops amehamisha kipindi chake cha taarabu kama kilivyo kutoka Times Fm na kukipeleka Wasafi Radio. Kipindi cha The Story Book ni mfamo wa maudhui ya Ananias Edgar na Denis Mpagaze.

Refresh ni kipindi kizuri ila maudhui yake ni ya
E-news ya East Africa Tv, wamemchukua jamaa aliyekuwa EATV nyuma ya Camera akiwahoji wasanii au watu katika show. Yaani vile vile alikuwa anajifunika asionekane sura akiwa EATV ndiyo vivyo hivyo anavyofanya akiwa Wasafi Tv.

Bartender aliyokuwa anaitangaza Jonijoo, ni copy & paste ya #NowYouKnow aliyokuwa anaifanya Jonijoo katika YouTube channel yake, maswali yale yale ndiyo aliyahamishia wasafi. Japo idea ya Bartender ni ya msanii Baghad, nitaielezea baadae.

Ubaya ni kuyahuisha maudhui kwa kuyachukua yalivyo, nguvu ya pesa inaweza kukuweka sehemu kwa muda ila isipoambatana na maarifa na ubunifu inaweza kukuvunjia heshima na kukudharaulisha.

Msanii Baghdad aliwahi kusema kuwa wazo la kipindi cha The Bartender lilikuwa ni lake na mwanzo wazo lilikuwa #TheCounter au The Bartender na alilisajiri #Cosota na kubaki na hatimiliki yake. Alishangaa kuona kipindi kinatangazwa wakati makubaliano hayakuwa yametimizwa na kukubaliana. Baghdad anasema kuwa makubalialo yalikuwa ni apate 13% ya mapato yatokanayo na show na idea zote ambazo ataziweka pale Wasafi kuliko kuajiriwa yaani awe na life time contract na wasafi media.

Baghdad anaendelea kusema kuwa wakiwa katika mchakato wa kusaini mkataba ambao ilionekana kuwa 13% ni kubwa na ishuke hadi 5% ghafla akashangaa kuona promo ya The bartender, anasema aliamua kuwasiliana na Diamond, cha ajabu Diamond hakuwahi kupokea simu wala kujibu meseji zake. Anasema ilimstua na kuamua kumtafuta Babu Tale, Tale alimsihi sana Baghdad kuwa mtulivu wakati anaongea na Diamond juu ya hili. Alimsihi pia kutofanya chochote mathalani interview popote. Baada ya siku kadhaa Tale na Baghdad walichekiana na kumchana kuwa Diamond kasema fanya chocote unachoweza.

Baghdad aliamua kwenda Cosota kutafuta haki yake kwa maana hata wazo la Jogoo ni miongoni mwa madini aliyoyatoa Wasafi. Anazidi kusema kuwa, Cosota waliwaita ili kuwasuruhisha japo Diamond alikuwa akituma wawakilishi, mazungumzo yalifanyika kwa siku kadhaa bila mafanikio na Baghdad kuamua kwenda Mahakamani ili tu haki yake ipatikane.

Media inahitaji nidhamu yake ili iweze kukua na kubaki iko juu mawinguni, mambo kama haya yanashusha hadhi na kubomoa misingi yake. Hakuna anayejua kwa nini watangazaji wanaondoka Wasafi FM & TV katika kipindi kifupi sana, wengine wakidai kuwa ni makubaliano ya kimaslahi kukiukwa, wengine wakidai ni sheria zisizo fair kama kuzuia account binafsi za watangazi kama YouTube kutopandishwa content zao, mimi na wewe hatujui ukweli. Alipoondoka Mtiga Abdallah ilionekana ni utovu wa nidhamu, Jonijoo nae kasepa na amejiunga na TVE, inafikirisha sana kupata jibu sahihi.

Ulikuwa ni wakati wa Wasafi Media kuijenga na kuepuka watu kuwaona kama wababaishaji kwa kuwa ni wachanga. Contents ndizo zingebaki kama sababu ya watu kusikiliza au kuangalia Wasafi. Ilivyo sasa ni kama watu hufuatilia kwa sababu ya umaarufu wa Diamond. Yeye ndiyo ameibeba Wasafi Media begani mwake, ndiyo maana hata #WasafiFestival inaweza kuwa inan'ara kwa sababu ya uwepo wake. kesho akishuka kimuziki, kama Media House haikujengwa kinidhamu (kuheshimu mawazo ya watu, makubaliano, contents nzuri, ubunifu n.k) watu wataiona kawaida na kuipuuza. Umaarufu alionao utafifia siku moja.

Diamond anatakiwa kujua kuwa kati ya #Individualism Vs Society kila mmoja lazima amtegemee mwenzie, individualism haiwezi kufanikisha lengo bila Society, yes wewe ni maarufu, una hela, unaanzisha Media House, kifuatacho ni nini, ni kuungana na watu tofauti ili kama ni Radio, TV isimame. Kila mtu awe katika nafasi yake na atimize wajibu wake, iwe independent organ itakayokuwa na namna yake ya kazi.

MWISHO, nimpongeze Diamond na watu wake kwa kuona umuhimu wa kuanzisha Wasafi Media House, kama kuna tofauti za kimasilahi au kitabia ni kuzijadili na kuendelea kupiga kazi, kuwaacha akina Mtiga Abdallah, JoniJoo na wengine kwa muda mfupi sio sifa nzuri kwa mustakabali wao, Radio One & ITV zipo pale kwa kuwa wanavumiliana, kuvumiliana hakuji bila kuheshimiana. Kuheshimu wafanyakazi wako haimaanishi utapoteza U-Diamond wako, lazima ujue kuwa wao ndiyo wanaifanya Wasafi Media ku shine, kama kuna wazo mtu analo zungumza nae ili tuendelee kusikiliza na kutazama Wasafi, by the way, nina wazo kabambe sana la kipindi kizuri cha Tv, tunaweza kuchekiana pia.
Tchao! until next time.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mi nnachojua hakuna kipya chini ya jua




Ulitaka wcb waanzishe kipindi cha kwenda mwezini ndo uone upya na ubunifu??


Mtu unaponda halafu bado unafuatilia vipindi vyao maanake nini???
hakuna kipya chini ya jua??..ina maana iphone 11 pro ilikuwepo tokea zamani??..

Mfano,Millard alipoingia clouds na kuja na kipindi cha Amplifaya kuna redio bongo ilikuwa inafanya kitu kama hiki??..huu ndo ubunifu unaozungumza..

Kutengeneza characters..mfano soudy brown..japo umbea si ishu zangu ila huu ni ubunifu wa hali ya juu..

Diamond awekeze kwenye creativity,atafanikiwa sana,na sio kugombania tu presenters
 
hakuna kipya chini ya jua??..ina maana iphone 11 pro ilikuwepo tokea zamani??..

Mfano,Millard alipoingia clouds na kuja na kipindi cha Amplifaya kuna redio bongo ilikuwa inafanya kitu kama hiki??..huu ndo ubunifu unaozungumza..

Kutengeneza characters..mfano soudy brown..japo umbea si ishu zangu ila huu ni ubunifu wa hali ya juu..

Diamond awekeze kwenye creativity,atafanikiwa sana,na sio kugombania tu presenters

achana nao je waulize ile homa ya tvE ilikuwepo??


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom