Warning: Kwa mnaouza gesi za Oryx na Mihan, wajanja wamerudi mjini

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
51,132
22,384
Watanzania kadhaa wasiowaaminifu wamekuwa wakiuza gesi isiyo halali nikimaanisha gesi ilio chini ya uzito wake

Zoezi hili limeanza miezi minne iliopita kuna watu wasiowaaminifu wananunua mtungi mkubwa mrefu, wanachukuaa mitungi midogo na kujaza na pipes majumbani mwao,seal wanashirikiana na watu wasio waaminifu kufunika pale juu.

Unaponunua mnunuaji mkuu n ngumu kujua unless kama utaanza kupima mzigo mmoja baada ya mwingine
mbaya zaidi baadhi ya mitungi huwa wanaweka maji ndani via pipes, ili mtungi uweze kujaa/ndio maana kuna baadhi ukiwasha jiko, jiko aliwaki ila mtungi ukitikisa unasikia bado kuna kitu ndani.

Vijana hawa wamekuwa wakifanyia shuhuli hizi kwenye nyumba zao moja iko kimara mwisho na nyingine iko karibia na kituo kikuu cha mbezi mwisho, nisingependa kuweka wazi maana wako kwenye uchunguzi ila kukusaidia wewe unaenunua mzigo wa jumla namba zao zinaishia na 042,072.

Huwa wanatembeelea na hivi vigari vya mizigio vidogo vyeupe vikiwa na chuma kwa nyuma.

Matumaini utakuwa muangalifu kwa hili kukusaidia kuondokana na makeelele ya wateja..wazo tu akikisha anaekultea anakuletea toka kituo cha gesi kinachojulikana hili litakusaidia ikiwa kuna shida yoyote ni rahisi sana kukubadilishia.

Nawatakia biashara njema ya gesi wote.
 
Asante kwa taarifa ndugu,hivi naomba kujua mtungi mkubwa wa kilo 15 naweza tumia kwa muda gani kwa matumizi ya kupika mara3 kwa siku,nataka kujua kama nimepigwa ama la!
 
Asante sana kwa taarifa hii muhimu...
Hapo hata mtumiaji wa gesi anaumizwa moja kwa moja na uharamia huu unaofanya na hao wauza gesi. Kuna siku nilisema Natamani sana mitungi ya gesi ingekuwa mfano wa kioo inaonesha ujazo wa gesi waziwazi, kuliko kutegemea eti Kg tu. Mteja uone jinsi ilivyojaa,inavyoshuka na hadi inavyoisha.
Binadamu wafanyabiashara WENGI siyo waaminifu kibiashara wanachojali wao ni Kupata faida hata kama upatikanaji wake ni wa KUMUUMIZA MLAJI/ MTUMIAJI.
 
Asante sasa mkuu,
hata mimi nimekutana na hilo janga last month mtungi umeisha sijui wiki tatu wakati siko na familia??
Kwa hasira nikafuata mjini kwa dealer wa Oryxy ..
 
Mm niliwai nunua kwenye kituo kbs nilipaki juu kwa juu foleni nikafungua faster waniletee na nimezoea mlinzi akaniletea mpya akuchuka wazamani kwa buti nikampa hela.yake nafika.nyumbani washa washa na ww unatoa maji.cjui nn asubui nikabeba ni mzito kama kawaida naika pale nawaeleza wananiambia risiti ipo wp yani icho ndo chakwanza nikajua nimepigwa tyr wakaupima.uzito sawa ila aitoi gesi wakaniambia.no way ninunue mwingine roho iliniuma.sana
 
Na hiyo wengi hatuombagi rist na kwa vile nao sio waaminifu wanauchuna tu, hapa umakini unahitajika
 
Watu km nyie mngekuwa kumi tu Tanzania plus Magufuli ingekuwa kisiwa kizuuri cha kuishi. Thanx thanx .......
 
Duh nimepigwa kabisa nimenunua kama wiki ivi na jiko linawaka kwa tabu sana nikajua tatizo jiko kumbe ni mimaji itakua nyambafuuu zao.
 
Asante kwa taarifa ndugu,hivi naomba kujua mtungi mkubwa wa kilo 15 naweza tumia kwa muda gani kwa matumizi ya kupika mara3 kwa siku,nataka kujua kama nimepigwa ama la!

Miezi mitano mpaka sita inategemea unachopika.
 
Asante kwa taarifa ndugu,hivi naomba kujua mtungi mkubwa wa kilo 15 naweza tumia kwa muda gani kwa matumizi ya kupika mara3 kwa siku,nataka kujua kama nimepigwa ama la!

Itategemea na aina ya chakula, mfano atakaetumia kupiga ugali mara 3 kwa siku hatakuwa sawa na atakae chemcha makongoro mara 1 kwa siku, huyu wa kongoro atatumia gas nyingi zaidi ingawa kapika mara moja
 
Kuna "Pressure gauge" unafunga pale kwenye kichwa inakuonyesha ujazo uliomo ndani ya tanki,
Na ni rahisi kujua kama gesi imekaribia kwisha coz gauge "Gage" inaonyesha


Kama Bongo hakuna hizo gauge, kwa mnaokwenda China changamkieni hiyo fursa najua China zitapatikana tu..
 
Nasmaapesa mwezi unakaa.kama hutopikia maharage walakuchemchia maji
 
Back
Top Bottom