Waraka wangu mfupi kwa Kikwete, na washauri wa Kikwete.

Status
Not open for further replies.

Mcheza Karate

JF-Expert Member
Jun 30, 2011
690
350
Mpendwa rais wangu, je unakumbuka kuwa ulivyoingia madarakani mwaka 2005 watu tulikuamini sana na ukawa kama "mwenzetu?"

unakumbuka ulikuwa maarufu kuliko hata chama chetu(CCM) kwa wakati ule?

Je unakumbuka vizuri ulituahidi nini waTANZANIA?

Je unakumbuka uliwaahidi nini waislamu?

Unakumbuka wewe na tema member wako kinana uliwaahidi waislamu Kupitia BAKWATA kuwa utawapatia waislamu Mahakama ya kadhi na na Tanzania kujiunga na OIC?

Je si unakumbuka uliahidi kuwapa nafasi nyingi waislamu ktk uongozi? Umesahau?

Je unakumbuka kuwa uliahidi kukipanua chuo kikuu cha kiislamu Morogoro? Vipi tayari umeshapanua?

Rais wangu mpendwa wewe ni mdini na naomba ujue hivyo. Umetupandia mbegu mbaya sana na hadi sasa binafsi nina mashaka sana na wewe.

Kumbuka mwaka 2010 ktk kampeni zako za uchaguzi (ulieneza kwa maksudi au kushawishiwa na kinana) propaganda ya udini.

Si ulituambia waislamu kuwa tusichague Chama ambacho mgombea wake ni padri kwani wana lao jambo? Tukuchague wewe ambaye ni muislamu "MWENZETU"?

Umeona mbegu uliyopanda BAKWATA wakaipalilia, wakaeneza ujumbe huu misikitini? Au hukuwatuma wewe? Walijitungia kwa vile nayo BAKWATA ni TAASISI ya serikali?

Mpendwa rais wangu unakumbuka mara baada ya uchaguzi ulisema udini ulishamiri sana. Je ulivyowaita mashehe na maaskofu ndo basi? Mbona wote wapo uraiani na kinyongo? Kila mmoja wao anasema lake la kukulaumu?

Mpendwa rais, je una habari kuwa radio iman imefungiwa? Unajua shehe ponda yuko mahabusu na amenyimwa dhamana?

Mbona uko kimya? "UMETUSALITI"? Si uliahidi utakuwa bega kwa bega na sisi?

Hivi umewahi kusikiliza malalamiko ya wakristu kuwa bwana mkubwa unaongoza kwa upendeleo na ushabiki wa kidini? Umewahi kuwaita maaskofu ikulu ukanywa nao chai huku wakikueleza unapoteleza?

Mpendwa rais wangu, je huogopi hali ilivyo hivi sasa? Je wakristu hawatatupiga mapanga waislamu na waislamu hatutawachoma visu wakristu?

Je kwa ahadi ulizoahidi kuwatekelezea waislamu na ulivyo mgumu kuzitekeleza huoni ipo siku TUTACHOKA?

Mpendwa rais, kwanini wasaidizi wako wanakuogopa sana kukuambia ukweli? Au unawachagua ambao watakuridhisha ktk kauli zao tu?

Kwa nini unamtumia wassira kumaliza migogoro ya udini huku ukijua fika "WASSIRA ANAKUOGOPA?" Na si unajua Wassira huwa hakubali kushindwa anapotatua mizozo au migogoro?

Si unajua Wassira huwa anajiona mnyonge pale anaposhindwa na kuona kushindwa kwake ni kushindwa kwa serikali?

Kwa nini usiwatumie watu makini kumaliza tatizo la udini? Kwani suluhu inatafutwa na mawaziri tu? Kwa nini usiunde tume ikaja na majibu na mapendekezo juu ya mtafaruku huu baina yetu waislamu na wakristu?

Au kwako hili ni dogo tu na kama UPEPO WA SIASA UNAOPITA? Hivi ni nani huwa anakushauri ktk mambo yanayohitaji maamuzi magumu?

Mpendwa rais, unajua kikundi cha Boko haram kilianzaje? Unajua historia ya Alqaida au alshaabab? Punguza presha rais wangu. Kaa chini tulia jipange, tatua huu mzozo mapema.

Kama wasaidizi wako wanakudanganya kuwa tatizo la udini ni dogo hivi sasa na halina madhara basi amini wanaogopa kukuambia ukweli kwa vile wewe mwenyewe ndio mpandaji wa mbegu hii.

mpendwa rais, nakusihi kuwa macho na chuki za udini. Tunaipenda Tanzania, hatutaki tuipoteze.

Unafanya juhudi gani kuondoa udini huu? Na je UTAWEZA?

"wahadha assalam alleykum, wabilah taufiq"

Tafakari!!!!
 
Huo ndo ukweli na uzalendo. Mungu akubariki. Hopes wasaidizi wake wata take note.
 
Natumaini unastahili kuwa mshauri wa Rais, nyeusi waiita nyeusi na hiyo ndo lugha sahihi, hakika weye ni mkweli na mzalendo kwa Taifa lako.
Rais wako atakusoma tu au idara yake ya habari ya akina Nshomile Salva itaisoma article yako ila usitarajie matekelezo coz inasemekana kuwa Rais wako hashauriki. Kama raia, umetimiza wajibu wako kwa nchi yako kwa kusema ukweli daima.
 
Natumaini unastahili kuwa mshauri wa Rais, nyeusi waiita nyeusi na hiyo ndo lugha sahihi, hakika weye ni mkweli na mzalendo kwa Taifa lako.
Rais wako atakusoma tu au idara yake ya habari ya akina Nshomile Salva itaisoma article yako ila usitarajie matekelezo coz inasemekana kuwa Rais wako hashauriki. Kama raia, umetimiza wajibu wako kwa nchi yako kwa kusema ukweli daima.

nashukuru. Tuwe na upendo tu wakati nchi ikiwa imepoteza umoja wa kitaifa
 
Alichochea ila hakujua kama mambo yatafika hapa yalipo.

Hata yeye kwa sasa hajui suluhu, kwa hiyo inabidi amwachie hili tatizo mrithi wake anayekuja ataalitatua.
 
Huo ndo ukweli na uzalendo. Mungu akubariki. Hopes wasaidizi wake wata take note.
Yani mpaka inaliza kwani watu makini kama jamaa wasiwe washauri wa rais,.... eti wasira ndio mshauri wakati akili yake ime diminish to 0.00009%... KAMA MWANZA WAMESALI MKESHA WA PASAKA JION BAADA YA USIKU kisa ni waslamu Hali ni mbaya sanaaaaaaaaaaaa
 
Huo ndo ukweli na uzalendo. Mungu akubariki. Hopes wasaidizi wake wata take note.

kwanza uliyeleta mada hii wala siyo muuislam we pimbi tu,rais kikwete ni rais wa tanzania wala siyo rais wa waislam kama unataka udini ni hukohuko wewe na wazazi wako tena koma kutuletea hoja za udini humu pimbi mkubwa wewe.
 
Huo ndo ukweli na uzalendo. Mungu akubariki. Hopes wasaidizi wake wata take note.[/QUOTE ]

Kikwete huwa hana confidence na ndio maana anachagua washauri weak ambao wanaogopa kumwambia ukweli!! Hebu chunguza ni nani mshsuri wake wa mambo ya uchumi na ana uzoefu gani!!!! Weak input leads to weak output!!!
 
Yani mpaka inaliza kwani watu makini kama jamaa wasiwe washauri wa rais,.... eti wasira ndio mshauri wakati akili yake ime diminish to 0.00009%... KAMA MWANZA WAMESALI MKESHA WA PASAKA JION BAADA YA USIKU kisa ni waslamu Hali ni mbaya sanaaaaaaaaaaaa
Neno la Mungu linasema hivi "Heri wapatanishi maana ufalme wa Mungu ni wao" Kinyume chake Wassira atajiju. Upatanishi kinyume chake ni Uchonganishi.
 
Wajinga tu ndo watakusifu. Lakini sisi wajanja tayari tumenusa kitu. Hutupati ng'o kwa kuwa tunajua aliyekutuma.

huenda nikawa nimetumwa. Na kweli nimetumwa na dhamiri yangu. Tena imenituma ninene nilichoandika hapa. Ila nadhani wewe unaweza ukawa unatumika bila kujijua. Ila sio mbaya sana ndo mjadala lazima pawepo watu wa aina yenu.
 
kwanza uliyeleta mada hii wala siyo muuislam we pimbi tu,rais kikwete ni rais wa tanzania wala siyo rais wa waislam kama unataka udini ni hukohuko wewe na wazazi wako tena koma kutuletea hoja za udini humu pimbi mkubwa wewe.

unajaribu kuficha uso kwa viganja mkubwa. Mimi ni muislamu kama wewe unavyojionesha. Ila sema kosa langu ni kusema ukweli ndo nimeonekana mkosaji kwako. Ila jadili hoja tu. Kama nimegusa ukweli samahani.
 
Hii Islamophobia itawaua kabla ya siku zenu. Na kama mna base criticism kwa rais wa nchi kwa vigezo vya dini basi mjue hamtakuja kusimamisha rais kwa chama chenu maana CCM wanasoma mchezo mzima. Come 2015 CCM itawapa mnachotaka na chama chenu kwishne.
 
Ukitaka kujua jamaa ni mdini na CCM ndio wa kulaumiwa kwa haya yanayotokea,katiba ya Tanzania inatamka wazi kuwa Serikali haina dini,ila kwenye Ilani ya CCM wameahidi kushughulikia swala la Mahakama ya Kadhi sasa hapa watajinasua vipi kwenye kitanzi walichojivika wao?
 
Hizi ni bia za pasaka tu hamna kingine.

usijali. Tukana lakini lakini sitokaa nikwepe kivuli changu. Simwogopi awaye yoyote ktk ukweli labla allah! Lakini mwenyezi mungu akukirimu busara na maarifa wakati unachangia hoja.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom