Waraka wa wazi juu ya Mahusiano ya Wakristo na Waislam kujenga amani ...

Dini
Ni mfumo wa maisha ambao mwanadamu wamejiwekea kuhisi kupitia mfumo huo.Katika dini kunahusisha imani ya mtu pia.
Historia ya dini:
Islam
Uliletwa na waarabu katika pwani ya africa mashariki na baadhi ya maeneo wakiwa na lengo moja kusambaza mfumo wao wa kuishi pia kupata bidhaa kutoka kwa machief wetu waarabu hawa ndo waliendesha slave trade kuuza mababu kwenda ulaya kufanya kazi zenye ujira mdogo na mateso makubwa.
Ukistro:
Ulianza kuenea africa mashiriki baada ya kuingia kwa wa missionaries ambao walingia ndani zaidi ya nchi nyingi za Africa mashariki.hawa pia walikuja kufanya biashara na kutafuta madini

Kwahiyo tunaona kila dini ililetwa kwa malengo fulani dini ilikua kama sababu tu kukutanisha watu fulani.

Udini Tanzania:
Udini tanzania upo na tusijidanganye haupo kuna dini moja inalalamika kua kuna mfumo unaibeba dini nyingine toka kitambo sana.
Mfumo kristo:
Baadhi ya waislam wanadai kuna mfumo huu tanzania wanalalamika hawajapewa fursa kwenye Elimu,Afya,Uongozi,Utawala.
Lakini suala la kujiuliza je ni kweli tanzania kuna mfumo kristo na je kama upo tunafanyaje kuuondoa ili sehemu nyingine wasilalamike.

Suala la Kuchomwa kwa makanisa:
Mimi sikusahangazwa sana na suala la kuchomwa kwa makanisa hii chuki imepandikizwa siku na daima kuna baadahi ya waislam wanaona wakristo ndo wabaya wao kwahiyo tatizo linapotokea wengi wanakimbilia kufanya kitu fulani sababu ya chuki.

Suala la sheikh ponda:
Kwanza tuwe wakweli Ponda hahusiki vurugu za mbagala.Ponda anaendesha harakati za kuutoa uongozi wa bakwata ambao baadhi ya waislam unaona ni uongozi mbaya sana unachezea hela za waislam wengine.
Lakini suala la kujiuliza kwanini serikali inamshikilia sheikh Issa Simba na uongozi wa bakwata kuna maslai gani pale bakwata.
Nasikia ndo taasisi yenye pesa kuliko zote Tanzania
Je bakwata wamefanya nn mpaka sasa
Wameshajenga chuo hata kimoja
Nasikia shule walizokua wanaendesha zote zimekufa
Wameshajenga hospital ngap mpaka sasa
Ponda anaendesha harakati za kuitoa bakwata tuache propaganda hapa.

Uamsho:
Toka zanzibar ipate mafuta chokochoko za kujitenga zilianza na hizi zinaongozwa na kikundi cha uamsho na kufadhiliwa na viongozi wa serikali na umoja zanzibar tusiume maneno hapa.

Juzi kiongozi wao alitekwa kama wanavyodai maelezo ya dereva wake alijipeleka mwenyewe kwa watekaji hao akaingia kwenye gari.
Hivi uchukulue na usalama wa taifa wakakuulize maswali urudi vile vile na tabasamu angalia zile picha utaniamba.

Either uamsho walificha kiongozi wao wajionyeshe wana nguvu kubwa.Maana serikali ilikataa kuwa naye.
Uamsho ni hatari sana tukiangalie hiki kikundi

Maadili yetu yamekwisha sasa
Tumezoea kuwadanganya watoto kwamba ukichana bibilia au koran utakufa watoto wetu wa siku wanachunguza kweli mtoto watacheza wakianza kuleta utani wa kitoto tu ndo mambo ya mbagala yakatokea.

Watoto wetu hawana maadili
Taifa zima maadili yamekwisha kabisa humu ndani ya jamiiforums mnadhikiana kwa udini
Katika mitandao ya kijamii inayoongoza kwa mijadla ya kidini ni humu.

Yakufanya kuondoa hizi kadhia:
Mijadala ya kidini. Kujadili tatizo
Kuboresha elimu kwa watoto wetu ya maadili
Kutengeneza fursa ya elimu kwa ndugu zetu waislam waipate kwa sawa
Kuipitia upya bakwata
Sote ni ndugu dini zilikuja

Vyama vya siasa viache kutumia dini kutafuta kura;
CUF ilifanya
CCM ilifanya 2010 kueneza udini na propaganda za ajabu
CHADEMA sikusikia makanisi tukiambiwa tuichague I stand to be corrected.
Turudie msingi ya baba wa taifa kuunda taifa hili.
Tuache chokochoko za kidini kwenye mitandao kwenye radio(radio imaan)
Tushirikiane kwenye maendeleo kama Mh mengi anavyojitoa hata kwa waislam

Kumbuka dini zililetwa tu zisitugombanishe sisi ni ndugu

N:B
Taifa letu lilijengwa kwa nguvu nyingi sana litaboboka kwa nguvu ndogo na itakuwa ngumu kujenga taifa imara kama Tanzania

Tulinde Amani yeru,Muungano wetu

Mungu ibariki Tanzania

Fred Kavishe

Sasa mods mnaweza kunibadilisha jina langu la nick name kuwa hilo hakuna haja ya kujificha tena
 
mkuu kavishe maneno yako kuntu. kabla dini hazijaletwa na wakoloni wazungu na waarabu, tulikuwa tunaabudu nini na tulikuwa tunaishije kama jamii?
 
Kweny hichi kipengele mkuu ndo umegusa kabishasa hasa kwenye Red.
Watoto wetu hawana maadili
Taifa zima maadili yamekwisha kabisa humu ndani ya jamiiforums mnadhikiana kwa udini
Katika mitandao ya kijamii inayoongoza kwa mijadla ya kidini ni humu.
 
Mi naona mpuuzi ni wewe...kwanza definition yako ya dini haiendani na definition ya dini kwa mujibu wa uislam, so kulazimisha kujenga mada kwa definition hiyo ni upuuzi.

Pili muungano umewekwa na watu na utavunjwa na watu...ikiwa sehemu moja ya waliouweka muungano huo wanasema basi, wee unaelazimisha ndie mpuuuzi.
 
Na hizi ndo tunazipeleka mtaani
 
Wewe nani kakuambia hiyo ni definition ya dini kila mtu anajenga hoja yake dini ina maana nyingi ndugu uliyosoma ww sio niliyosoma mimi.

Muungano hautakufa kwa matwaka ya watu wachache pale tu wanzibar wote wakiamua hawataki muungano
 
Kwanza jifunze ustaarabu, wanaotofautiana na wewe kimawazo si wapuuzi...na kupitia Katiba mpya ndipo wazanzibar watakapo kupa jibu kama wanautaka muungano au hawautaki. Muulize warioba atakupa hints kwa kinachoendela so far!

Pili sababu definition ya dini zinatofautina ukome kuwaita wengine wapuuzi sababu ya misimamo yao katika dini kwani misimamo hiyo inatokana na definition yao. Katika uislam DINI ni mfumo kamili wa maisha uliowekwa na Mwenyezi Mungu kwa waja wake ili waufuate.
 
ukichunguza kwa makini,sio waarabu wote ni waleta noma,angalia wale wa Oman,Yemen,Brunei,Kuwait na Qatar walivyotulia,wale uislamu kwao umeanza siku nyingi mno lakini hawana mambo ya ajabu ajabu,huku kwetu KULIKONI?
hawa wafuasi wa waarabu wanaleta noma daily
 
Nashukuru kama bado tuna wenzetu kwenye jamii hii wapo wazi na wakweli kwenye suala la amani ya nchi hii.
Mara zote sisi binadamu huwa tuna vionjo vyetu na moja ya vionjo hivyo ni ile hali ya kuwa na amani si moyoni tu bali hata ya kifikra hasa unapo kuwa karibu na mwenzako wa labda dini moja au kabila moja hizi ndo hulka za kibinadamu huwezi kushindana na ukweli.Wazazi wetu mbadilike kizazi hiki ni tofauti sana na kizazi chetu watoto hawa ni wadadisi kwa kila jambo mie napata taabu sana kutoa ufafanuzi kwa wajomba zangu wanapo bishana kuhusu mambo ya msingi kabisa kwenye maisha tofauti na zama zetu ambazo tualiambiwa mama ameenda kununua mtoto sokoni kumbe kaenda hospital kujifungua. Hii ni sawa na watoto wa kule Mbagala hadithi kama hizo hazina nafasi tena kwenye jamii yetu ni budi tukawafundisha heshima na maadili mema yatokanayo na vitabu vyetu vitakatifu na si vitisho ambavyo mwisho wa siku vinatuumbua.
Suala la wengine kuwa wanapendelewa kwenye masuala ya uongozi, utawala na mambo mengine inabidi tuwe wakweli kutoka ndani ya mioyo yetu. Mambo mengi wanayo lalamikia yamezungukwa na elimu dunia na si elimu ahera kama ambavyo wenzetu wanasisitizia, la msingi ni wao kujipanga na kutengeneza mikakati ya kuinua suala la elimu kuwa na taasisi zenye nia ya dhati kuwakomboa waumini wao ambao wamezama kwenye kadhi hii ya kutokuwa na elimu dunia na ufahamu mdogo kwenye masuala ya msingi katika ustawi wa maisha ya binadamu. Hamuwezi kukaa na kusubiri serikali iwafanyie hicho mnacho taka maana iko wazi kuwa hawawezi kuwajengea shule kwa ajili yenu tu hii nchi ni yetu sote na wote tunalipa kodi JIPANGENI. Msikubali kutumiwa na vyama vya siasa ambavyo vinakimbilia kwenye mlango wa udini kutimiza malengo yao. Mlihitaji muda mfupi tu wa tafakuri kuweza kutambua changa la macho 2010 kwenye hekaheka za uchaguzi kuwekewa suala la mahakama ya kadhi kwenye ilani yao, mngesoma katiba kwanza kabla ya kuwaamini walicho waambia(Serukamba bungeni alilalamikia suala hili)Tulipofika hapa wa kulaumiwa ni serikali maana watu walisha andika na kuonya juu ya watu hawa wanaopandikiza chuki za kidini lakini sikio la kufa halisikii dawa walinufaika nao hawawezi kuwatenga sasa. Ushauri wangu ni kuwa fundisheni na muhubiri mazuri yatokanayo na imani yenu na si mapungufu ya dini zingine maana mwawasema vibaya lakini waumini wanaongezeka mwisho wa siku watoto wa kizazi hiki wanatafakari na kusema ni MAJUNGU NA UNAFIKI KWANI HAKUNA ALIYE MKAMILIFU CHINI YA JUA WOTE TU WADHAMBI NA WAPITAJI
 
Kwanza jifunze ustaarabu, wanaotofautiana na wewe kimawazo si wapuuzi...na kupitia Katiba mpya ndipo wazanzibar watakapo kupa jibu kama wanautaka muungano au hawautaki. Muulize warioba atakupa hints kwa kinachoendela so far!

Pili sababu definition ya dini zinatofautina ukome kuwaita wengine wapuuzi sababu ya misimamo yao katika dini kwani misimamo hiyo inatokana na definition yao. Katika uislam DINI ni mfumo kamili wa maisha uliowekwa na Mwenyezi Mungu kwa waja wake ili waufuate.

Mm nimechambua dini kwa jinsi yavyoona mimi na ww chambua jinsi unavyoona ww
 
Sisi hatutaki chochote tunachotaka zanzibar huru na muungano hatuutakiiiiiiiiiiiii hapo tena fitna zote Zitaisha
 
Serikali ya Tanzania haina dini [maneno na msistizo wa hayati Baba wa Taifa, mwalimu Julius Nyerere-wakati wa uhai wake], bali watu wake wana haki ya kuwa na dini. Dini zisitugawe watanzania. Tusichanganye dini na siasa, na pia tusichanganye siasa na dini.

Tatizo la udini limetokana na udhaifu wa viongozi wetu wengi wa kisiasa kutafuta kuungwa mkono na viongozi wa dini kwa maslahi yao binafsi ya kisiasa. Inawezaekana viongozi hawa wa kisiasa hawakutambua madhara ya kutumia dini kutimiza utashi wao wa kisiasa.

Viongozi wa dini walipoona kuwa jukwaa la dini linatumika kwa maslahi binafsi ya wanasiasa na viongozi wa serikali, nao pia wakaingia kwenye “game” la siasa [jukwaa la siasa] .

Hapo ndipo utata ulipoanza, siasa na dini kuingiliana. Madai/kauli za viongozi wa dini mbali mbali zikaanza kuwa na nguvu katika kushinikiza maamuzi ya serikali kwa maslahi ya dini husika. Dini zikaingia “vitani”, kila dini ikitaka isikilizwe na serikali na madai yao yatimizwe.

Kutokana na hali hiyo, viongozi wa siasa na serikali wamekuwa wakipata ugumu katika kuwaongoza watanzania; wawasikilize watanzania kwa ujumla wao, au wawe wawakilishi wa dini zinazowaunga mkono na kutumia nafasi zao za uongozi kwa maslahi ya dini fulani? Watanzania tuepuke hili kwa maslahi yetu sote kama taifa moja, kwa faida ya kizazi cha sasa na cha baadae.

Baba wa Taifa aliliona hili: “Serikali haina dini”. Watanzania tu wamoja!!!!!!!!!!

Unapokuwa kiongozi wa kisiasa [chama] au wa serikali unapaswa kutambua kuwa watu unaowaongoza ni watu wa imani tofauti. Jambo la dini linabidi uliweke kando, halina nafasi katika nafasi yako ya uongozi. Dini hizi tunazozifuata watanzania ni dini za mapokeo, ziliwakuta mababu zetu wakiwa wamoja, kwa hiyo zisije kutugawa watanzania!!!!!!

Swali
: Mbona tunaimba wimbo wa Taifa: "Mungu ibariki Tanzania……"? jibu la haraka lisiloumiza kichwa: Mungu siyo dini. Pagani anaamini Mungu yupo, lakini ibada ya kumuabudu Mungu anayemwamini ni tofauti na ya Mkristo, Muislamu, Muhindu, n.k. Mwanasayansi pia anaweza kumzungumzia Mungu kwa namna tofauti, siyo kiislamu wala kikristo. Tafsiri ya Mungu isitugawe watanzania!!!!!! Mungu kwenye wimbo wa Taifa ni yule unayemwamini wewe mtanzania mmoja mmoja kwenye nafsi yako. Unapoimba wimbo wa Taifa kwa kumtaja Mungu ni yule unayemwamini nafsini mwako!!!!!!

Hitimisho: Watanzania tuunganishwe na utanzania wetu, tusitenganishwe na imani au dini zetu. Viongozi wa kisiasa na serikali wanaokwenda wakizunguka kwenye nyumba za ibada kutoa michango mikubwa kwenye nyumba za ibada huku wakihubiri siasa kwenye nyumba hizo, ni sawa na kutoa rushwa ili nyumba hizo za ibada zitumike na ziwasaidie katika kutimiza maslahi yao binafsi kisiasa.

Serikali haina dini. Watanzania wa kweli hawatakubali dini ikatumika katika uvunjifu wa amani ya watanzania. Mtanzania, unayo haki ya kumwabudu Mungu umwaminiye kwa kupitia dini uyaminiye. Haki yako hiyo istumike kuwagawa watanzania na kuchochea chuki miongoni mwao.

Haya shime: Ipende tanzania, wapende watanzania wenzako!!!!!!!
 
Assalaam a'laikum ,Jamani waislaam wenzangu wote tutulie hatakamaa tunachokozwa tuwaachie Allah {SWT}hakika yeye ndomwenyekuhukum kwani hawa makafiri chokochoko nauchokozi hawajauanza leo kwani hata enzi za nabiiMuhammad {S.A.W}Mpaka kumfukuza Makka na kwenda Madina na pia tujaribu kuwavumilia kwani hata mtume Muhammad (S.A.W) wakati ikijibizana nao hawa hawa makafiri Mwenyezi Mungu{S.W.T}alimteremshia aya na kumwambia:wambie enyi makafiri siabudu mnachokiabudu,walanyinyi hamuabudu ninayemuabudu,wala sitaabudu mnachoabudu,wala nyinyi hamtaabudu ninaye muabudu,ninyi MNADINI YENU na mimi NINIDINI YANGU. Hivyo nawaasa tu waislaam wenzangu kuawenye subira na nyinyi WACRISTO acheni uchokozi na kudharau dini za wenzenu pia unapomfundisha mwanao mazuri ya dini yako, usimfundishe ubaya wa UISLAAM kwani utamfanya awe nimwenye kuchukia UISLAAM,vitabu vya kiISLAAM na WAISLAAM wenyewe kitu kinachoweza kuhutarisha amani yetu adim tuliyonayo Tanzania ~KAGOMA BIHUSI.
 
The solution is to stop brainwashing your kids, the argument btn the kids proved you wrong. you always lies to your kids regarding the power of quran, just tell them the truth.
 
Assalaam a'laikum ,Jamani waislaam wenzangu wote tutulie hatakamaa tunachokozwa tuwaachie Allah {SWT}hakika yeye ndomwenyekuhukum kwani hawa makafiri chokochoko nauchokozi hawajauanza leo kwani hata enzi za nabiiMuhammad {S.A.W}Mpaka kumfukuza Makka na kwenda Madina na pia tujaribu kuwavumilia kwani hata mtume Muhammad (S.A.W) wakati ikijibizana nao hawa hawa makafiri Mwenyezi Mungu{S.W.T}alimteremshia aya na kumwambia:wambie enyi makafiri siabudu mnachokiabudu,walanyinyi hamuabudu ninayemuabudu,wala sitaabudu mnachoabudu,wala nyinyi hamtaabudu ninaye muabudu,ninyi MNADINI YENU na mimi NINIDINI YANGU. Hivyo nawaasa tu waislaam wenzangu kuawenye subira na nyinyi WACRISTO acheni uchokozi na kudharau dini za wenzenu pia unapomfundisha mwanao mazuri ya dini yako, usimfundishe ubaya wa UISLAAM kwani utamfanya awe nimwenye kuchukia UISLAAM,vitabu vya kiISLAAM na WAISLAAM wenyewe kitu kinachoweza kuhutarisha amani yetu adim tuliyonayo Tanzania ~KAGOMA BIHUSI.
Mchokozi ni uislamu baada ya kuuchokonoa Ukristo! Yaani wamelazimisha hata Yesu wakati hayupo na kumuita eti isa! Ona basi Yesu anasema yeye ni Mwana wa Mungu! Uislamu unasema unakufuru! anaekufuru anaitwaje? Acheni uchokozi, kukosa subra ya Wakristo pangechimbika na uislamu ungebakia stori!
 
Back
Top Bottom