Waraka wa wazi juu ya Mahusiano ya Wakristo na Waislam kujenga amani ...

HorsePower

JF-Expert Member
Aug 22, 2008
3,612
2,566
Habari za leo Wana JF?

Binafsi si mpenzi wa kuandika nyaraka lakini nimejikuta nalazimika kuandika waraka huu kwa uchungu mkubwa kutokana na mambo ambayo nimeyasikia na kuyashuhudia kupitia vyomba vya habari juu ya mpasuko mkubwa wa kimahusiano ambao umeanza kujitokeza kati ya baadhi ya waumini wa dini za Kiislam na Kikristo.

Kwa siku za hivi karibuni tumesikia vurugu nyingi kati ya waumini wa dini fulani na polisi, waumini fulani na kuchomeana majengo ya ibada, waumini fulani na udhalilishaji wa vitabu vya dini nyingine nk. Hili si jambo la kuchekewa hata kidogo maana halina mwisho mzuri. Inawezekana likawa limepandikizwa na baadhi ya watu kwa manufaa yao binafsi na ndiyo maana nimeamua kurudi hapa kuomba viongozi wa dini zetu wafanye jambo mapema kutunusuru na kutupa amani ya kudumu.

Kudumisha amani napendekeza wapenda amani wote na viongozi wetu wa dini kutufundisha sisi waumini wao mambo yafuatayo

  1. Kuheshimu dini na imani za watu wengine
  2. Kila muumini na afundishwe namna ya kuvumilia wafuasi wa imani nyingine na kutumia vyombo vya sheria kuchukua hatua kwa matukio ambayo yanaonekana yana lengo la kudhalilisha imani nyingine
  3. Kufundisha mafundisho ya namna ya kumsaidia muumini kuishi maisha ya kumpendeza muumba wake badala ya mafundisho ya chuki dhidi ya watu wa imani tofauti
  4. Waumini tufundishwe kuwa vurugu, chuki, mapigano, vita, hasira na mengineyo mengi yanayofanana na hayo kwa namna yeyote ile hayataweza kutusaidia kuondokana na tatizo tulilonalo sasa na badala yake hujenga chuki zaidi na mbaya zaidi kwa watoto wetu ambao ndio taifa la kesho. Hapa kuna hatari ya kujenga taifa lenye chuki, lisilo na amani na kukosa upendo.
  5. Kwa namna yeyote ile, hakuna dini inayoweza kuiondoa dini nyingine ndani ya nchi hata kama kutatokea vita ya miaka hamsini na zaidi, hivyo kupigana vita, kuchomeana nyumba za ibada na pengine hata kuuana ni kudhulumu uhai na nafsi za watu zisizo na hatia na kujiweka kwenye umasikini ambao hauna tija ya namna yeyote.
  6. Migogoro ya kidini huishia kwenye kuitia nchi kwenye umaskini badala ya kupata suluhu ya dini maana mwisho wa siku suala la imani halihitaji nguvu, linahitaji convincing power.
  7. Tujifunze kutoka kwenye nchi zenye migogoro ya kivita tuone kama kuna imani moja imefanikiwa kuiondoa imani nyingine au ni faida gani waliyoipata katika hivyo vita kama siyo kupoteza ndugu zao na kujitupia kwenye shimo la umaskini!!! Tujifunze toka Nigeria na nchi nyingine jamani!
  8. Kupiga marufuku mikutano ya wazi inayofanywa na wafuasi wa dini nyingine kuchambua vitabu vya dini nyingine na pia malumbano yeyote yale baini ya dini mbili tofauti.

Nawashukuru baadhi ya viongozi wa dini hasa wa Kiislam ambao wamediriki kutoa matamko ya wazi ya kudumisha amani na kuvumilia, nawatakia kheri kwa msimamo wao wa kujali na kuheshimu imani na amani ndani ya nchi.

Pia nawapongeza baadhi ya viongozi wa dini ya Kikristo kwa kuhubiri amani wazi wazi na kuwafundisha waumini wao kuwa wavumilivu na kutokushambulia wengine.

Watanzania, tuwe makini na watu wanaotaka kutugawa, tukumbuke kuwa hakuna nchi hata moja iliyowahi kuendelea au kufaidika kwa chuki na ugomvi wa kidini, na pia hakuna nchi iliyofanikiwa kuifuta dini nyingine ndani ya nchi na kupata amani.

Mwisho ningependa watu wote wausome waraka huu wakiwa na mtazamo wa kuisaidia nchi ikae kwa amani na siyo kuleta malumbano ya kidini yasiyo na tija ndani ya uzi huu, SIPENDI!

Nawapenda Watanzania wote na napenda tuishi kwa amani na upendo,

Nawakilisha,

HorsePower Kufakunoga.
October, 2012

******** Naomba usichangie, soma kwa faida yako *****
 
ni hatua tu ya dini kukua
baadae watajifunza kutokana na makosa yao.

Hata RC iliua kipindi fulani huko rome, kila mtu alikuwa analazimishwa kuwa mkiristu.

Faida waliyonayo ni kuwa wangeweza kujifunza kwa makosa ya wengine, hawakuwa na haja na wao kurudia makosa hayo hayo.

NB: kuhusu kutochangia nisingeweza, ni sawa na kusema nile, nitafune afu nisimeze.

Afu siku zote mie ni mvunja sheria, huwa siwezi fuata sheria.
 
Bwana Mmoja kwanini tupigane wakati sote twamuabudu Mungu Mmoja. Kama wapo wengi basi kila mmoja aache mungu wake ajipiganie.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
ni hatua tu ya dini kukuabaadae watajifunza kutokana na makosa yao.Hata RC iliua kipindi fulani huko rome, kila mtu alikuwa analazimishwa kuwa mkiristu.
nakumbuka kwenye history channel/NatGeo, RC wa zamani walikuwa maradufu ya ukatili tunaouona kwa sasa . yaani mpaka mwili unasisimka
 
kumbe walishawahi kuonesha.

Mie nilifundishwa kanisani, jinsi ya kuwachukulia, kuna historia ya kanisa la RC ukiisoma unaona makosa fulani hasa haya na kuua.

Je kanisa lilijifunza, labda, je wana nafasi ya kujifunza na wao, labda, je waache warudie makosa hayo, definetly hapana.

nakumbuka kwenye history channel/NatGeo, RC wa zamani walikuwa maradufu ya ukatili tunaouona kwa sasa . yaani mpaka mwili unasisimka
 
mimi nimejifunza jambo moja tu katika maisha

kuna makundi makuu mawili ya watu

1.walalahoi...kundi hili huwa linakusanya matatizo ya kila aina

itatumika dini,kabila na mengineyo but mostly ni umasikini tu

2. Matajiri kundi hili hutaona wakigombana kwa dini wala kabila wala chochote
mostly watashirikiana hata kuoleana bila kujali dini wala kabila mradi tu wabaki matajiri..

mengine yooote ni drama tu
 
Mie niliyajua hayo na ndio maana niliachana na hizi dini za mapokeo na kurudi kwenye dini za jadi za mababu zetu za kuamini matambiko na mizimu........
Hivi mshasikia wapagani wanagombana na mtu hata siku moja kwa sababu ya imani zao...?
 
Nimeipend hii mkuu nakuunga mkono na miguu
Mie niliyajua hayo na ndio maana niliachana na hizi dini za mapokeo na kurudi kwenye dini za jadi za mababu zetu za kuamini matambiko na mizimu........
Hivi mshasikia wapagani wanagombana na mtu hata siku moja kwa sababu ya imani zao...?
 
Mimi nawashauri wakristo wote waingie dini ya ki islam ili tuepukane na balaa, sababu uislam ndo dini ya haki.

Sababu waislamu wote wanamini Mungu ni mmoja tu, na ndugu zetu wakristo wanamini Kuna miungu mitatu.

1- God the Father

2- God the Son

3-God the Holy Spirit

Afu ukitazama sana kila siku wanakuja na story nyingi, Mara Yesu ndo Mungu mara sijui Yesu kumbe alikuwa na mke yani upuzi mtupu.

Vitabu vyao vinakanyagana karibu wa kristo wote wana amini Jesus alikuwa Mungu, na vingine vinasema alikuwa sio mungu ukweli hakuna hata single verse in the bible Yesu anasema alikuwa Mungu.

Afu tazama siku zote kwenye ukweli lazima kunakera wengi, ndo mana siku zote unaona wanao anzisha fujo ni wakristo sio waislamu.

Tazama huwezi kukuta muislamu ana msema Jesus, lakini tazama wakristo wanavyo msema Muhammad kwa kumzulia mambo ya uwongo.

Wailsmau tunamheshimu Jesus kama Muhammad sababu ni Prophet , Jesus ni kama Muhammad na kina Ibrahim walikuwa manabii walio tumwa na Mungu :poa
 
ni hatua tu ya dini kukua
baadae watajifunza kutokana na makosa yao.

Hata RC iliua kipindi fulani huko rome, kila mtu alikuwa analazimishwa kuwa mkiristu.

Faida waliyonayo ni kuwa wangeweza kujifunza kwa makosa ya wengine, hawakuwa na haja na wao kurudia makosa hayo hayo.

NB: kuhusu kutochangia nisingeweza, ni sawa na kusema nile, nitafune afu nisimeze.

Afu siku zote mie ni mvunja sheria, huwa siwezi fuata sheria
.

Kongosho hapo kwenye bold sijui niseme nini, maana unavunja sheria ukiwa unafahamu kuwa unavunja sheria, niliomba msichangie mada sasa amani ninayoizungumzia tutaipata kweli kama ndo mnafanya makusudi hivi?!
 
Last edited by a moderator:
Mimi nawashauri wakristo wote waingie dini ya ki islam ili tuepukane na balaa, sababu uislam ndo dini ya haki.

Sababu waislamu wote wanamini Mungu ni mmoja tu, na ndugu zetu wakristo wanamini Kuna miungu mitatu.

1- God the Father

2- God the Son

3-God the Holy Spirit

Afu ukitazama sana kila siku wanakuja na story nyingi, Mara Yesu ndo Mungu mara sijui Yesu kumbe alikuwa na mke yani upuzi mtupu.

Vitabu vyao vinakanyagana karibu wa kristo wote wana amini Jesus alikuwa Mungu, na vingine vinasema alikuwa sio mungu ukweli hakuna hata single verse in the bible Yesu anasema alikuwa Mungu.

Afu tazama siku zote kwenye ukweli lazima kunakera wengi, ndo mana siku zote unaona wanao anzisha fujo ni wakristo sio waislamu.

Tazama huwezi kukuta muislamu ana msema Jesus, lakini tazama wakristo wanavyo msema Muhammad kwa kumzulia mambo ya uwongo.

Wailsmau tunamheshimu Jesus kama Muhammad sababu ni Prophet , Jesus ni kama Muhammad na kina Ibrahim walikuwa manabii walio tumwa na Mungu :poa

fazaa haya ndiyo yale malumbano ya kidini ninayoyakataa, ni vyema kuheshimu imani ya mtu mwingine badala ya kuweka hoja ambazo hazijawahi kufanikiwa tangu kuwepo kwa hii dunia! Umewahi kusikia kokote kule dunia kuwa kuna dini moja imefanikiwa kuitoa dini nyingine au kuibadilisha?

Naomba tuwe na mitazamo itakayotuletea amani, kuheshimiana, kupendana na kuvumiliana badala ya kung'ang'ania kuandika makala zinazobomoa umoja na amani tuliyonayo. Tuwe na mapenzi ya kweli na nchi yetu na jamii iliyotuzunguka.

Kaka wewe ni Muislam ni ngumu kuelewa Ukristo vizuri unless utoke kwenye Uislam uingie kwenye Ukristo hivyo kwa Mkristo hawezi kuuelewa Uislam mpaka na yeye ahamie huko na kufundishwa imani za huko.

Kama Wakristo wana imani ya Kuamini katika utatu na kama wewe hauamini ni bora kubakia sehemu uliyopo badala ya kufikiria kutumia hoja za kubadili imani au nguvu kuumiza watu na kuharibu mali za wapita njia wasio na hatia.
 
Mie niliyajua hayo na ndio maana niliachana na hizi dini za mapokeo na kurudi kwenye dini za jadi za mababu zetu za kuamini matambiko na mizimu........
Hivi mshasikia wapagani wanagombana na mtu hata siku moja kwa sababu ya imani zao...?

Mtambuzi nakuunga mkono ingawa nilizuia kuchangia mada! Kama watu wote wangekuwa wapagani kama sisi, nafikiri tusingefika huku tunakoelekea hata kidogo!
 
Last edited by a moderator:
Mimi nawashauri wakristo wote waingie dini ya ki islam ili tuepukane na balaa, sababu uislam ndo dini ya haki.

Sababu waislamu wote wanamini Mungu ni mmoja tu, na ndugu zetu wakristo wanamini Kuna miungu mitatu.

1- God the Father

2- God the Son

3-God the Holy Spirit

Afu ukitazama sana kila siku wanakuja na story nyingi, Mara Yesu ndo Mungu mara sijui Yesu kumbe alikuwa na mke yani upuzi mtupu.

Vitabu vyao vinakanyagana karibu wa kristo wote wana amini Jesus alikuwa Mungu, na vingine vinasema alikuwa sio mungu ukweli hakuna hata single verse in the bible Yesu anasema alikuwa Mungu.

Afu tazama siku zote kwenye ukweli lazima kunakera wengi, ndo mana siku zote unaona wanao anzisha fujo ni wakristo sio waislamu.

Tazama huwezi kukuta muislamu ana msema Jesus, lakini tazama wakristo wanavyo msema Muhammad kwa kumzulia mambo ya uwongo.

Wailsmau tunamheshimu Jesus kama Muhammad sababu ni Prophet , Jesus ni kama Muhammad na kina Ibrahim walikuwa manabii walio tumwa na Mungu :poa
jamani sa mbona unaenda kulle kule tunakosema si kuzuri!kila mmoja aheshimu imani ya mwenzie!
 
fazaa haya ndiyo yale malumbano ya kidini ninayoyakataa, ni vyema kuheshimu imani ya mtu mwingine badala ya kuweka hoja ambazo hazijawahi kufanikiwa tangu kuwepo kwa hii dunia! Umewahi kusikia kokote kule dunia kuwa kuna dini moja imefanikiwa kuitoa dini nyingine au kuibadilisha?

Naomba tuwe na mitazamo itakayotuletea amani, kuheshimiana, kuopendana na kuvumiliana badala ya kung'ang'ania kuandika makala zinazobomoa umoja na amani tuliyonayo. Tuwe na mapenzi ya kweli na nchi yetu na jamii iliyotuz
Sawa kwanza lazima wakristo wanza kujifunza kuheshimu waislam, wawache tabia za kumsingizia mtume Muhammad uwongo na waheshimu kitabu chetu kitakatifu, uliona wapi muislamu akaikojolea bible?

Any way una point nzuri inabidi kila mtu aweke heshima mbele.
 
Back
Top Bottom