Waraka wa kuichafua Chadema wanaswa

kulopoka ovyo huku ndo kunapomshushia hadhi kila kitu anataka azungumze yeye afsa habari hana kazi kabisa pale cdm
 
Unategemea nini kutoka kwenye Mtanzania zaidi ya uzushi na Majungu!!
 
- Interesting!, vipi kwenda kwenye mahakama kama Dr. Slaa alivyomshauri Ridhiwani? ha! ha! ha! haya ndio matatizo ya siasa za kulipuana, maendeleo hakuna!

Willie @ NYC, USA.

Huna haja ya kushangaa, ilibidi ujishangae wewe, maendeleo yamedidimizwa na unachokitetea na unao wakumbatia. Hata mitume walikataliwa na waliokumbatia dhambi. Mahakama ni za serikali ya CCM, Dr Slaa aliwaita wote mafisadi mkuu wa nchi akiwa mmoja wapo, kama kweli ni wasafi si wangejisafisha au wangetumia dege la jeshi kumpeleka maweni? Tinga tinga mwenyewe aliitwa fisadi akaogopa hata waandishi wa habari.

Umpende uumchukie Dr. Slaa ni kiboko yenu, anawakera sana. Na kazi ndio inaanza. Tupo nyuma yake wenye nchi. Dr. hamlipui mtu anasema ukweli. Anafundisha jamii, anatahadharisha jamii, na jamii inamwelewa. Huwezi kumwelewa Dr wewe kwanza huijui Tanzania, unaisoma kwenye magazeti. Njoo manyoni, uyole, tunduma, isaka, mbarali, MMbwe, msata, ikwizu, meru, longodo, Mwanga, Manzese nk utajua kazi ya Dr. wa ukweli.

Serikali ilioongozwa na wazee wenu ndio imedumaza maendeleo mpaka ya elimu ya watanzania halafu leo mnawakashifu. Ngoja waamshwe.
 
Tatizo la CCM si ufisadi tu bali ni mambo mengi, watueleze kwa nini ktk kipindi zaidi ya miaka 40 ya uhuru hatuna umeme, maji, watoto wetu hawana elimu bora? sasa hivi chochote wanachofanya dhudi ya kuichafua chadema wanapoteza muda wao tu. Chamsingi wajiulize hizi kero kama mfumuko wa bei wanazitatua vipi?

To be specific: Ni miaka 50 au nusu Karne!!! Kwa zamani, kabla hawajachakachua kanuni za utumishi; huu ulikuwa ni umri wa kustaafu. Ndio maana naamini bila tashwishwi yoyote kuwa CCM inapaswa kustaafishwa.
 
Kijana tulia usiwe na papara ya evidence humu ndimo nyumbani mwake
hata ukitaka evidence ya nini utakula kesho watu watakupa.

ha! ha! ha! ha! nimeipenda hii. ila mwenzenu asipoandika km hivyo buku 2 atazikosa kutoka kwa napei.
 
Inaashiria fika kuwa kuna dalili ya vita baridi kati ya CCM na CDM. Msingi mkuu wa vitabaridi ni propaganda. Kwa hivo sote tunaoshuhudia vita hivi ni lazima tuwe makini kwanza tutafakari msingi wa hoja na tuhuma zinzotewa kisha tunaweza kuamua kuzipuuza au kuzijibu critically
 
Inaashiria fika kuwa kuna dalili ya vita baridi kati ya CCM na CDM. Msingi mkuu wa vitabaridi ni propaganda. Kwa hivo sote tunaoshuhudia vita hivi ni lazima tuwe makini kwanza tutafakari msingi wa hoja na tuhuma zinzotewa kisha tunaweza kuamua kuzipuuza au kuzijibu critically

kuna vita ya ukweli kabisa na wala sio baridi, ni vita ya ukweli kati ya ufisadi na chadema,
mafisadi + CCM Vs CDM + wananchi.
 
Waraka haukuandikwa na Nape; ila unaonekana umeandikwa kwenda kwa Nape..

"Waraka wenyewe umeandaliwa na Nape (Nnauye, ambaye ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM), baada ya kuona chama chao kimeshindwa kuwafukuza mafisadi. Sasa wanadai eti CHADEMA imepewa pesa zaidi ya sh bilioni tatu na mapacha watatu." Tanzania Daima
 
Habari ya kubuni wakati mtoa mada ameweka reference toka gazeti la Tanzania Daima? Tusiwe wepesi wa kuwa hasi bila kufanya jitihada kutafuta ukweli wa habari. Mimi nimeitafuta na nimeiweka hapo juu

Naomba kumfahamu mmiliki wa gazeti la Tanzania Daima.
 
HTML:
Tanzania Daima lilipowasiliana na Nape kuhusu tuhuma hizo za Dk. Slaa, alisema maneno hayo si mageni masikioni mwa Watanzania, kwani kiongozi huyo amekuwa akiyazusha kila mara.Alisema hajawahi kuandika waraka wala kumtuhumu Dk. Slaa, kwa kuwa ni mtu wa kawaida, hivyo hana muda wa kupoteza kwa ajili ya kiongozi huyo.Nape aliongeza kama Dk. Slaa ameshindwa siasa ni bora arudi kijijini kwake akalime vitunguu kuliko kuendelea na jambo asiloliweza. Kuhusu mapacha watatu, Nape alisema kuwa CCM haijashindwa kuwatimua mafisadi bali kinachosubiriwa ni kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), ambacho ndicho kitatoa hitimisho juu ya suala hilo.

KILIMO KWANZA HAKINA MAANA, KAMA INAONEKANA NI KAZI YA WATU AMBAO HAWANA AKILI KAMA KWELI NEPI NAUYE UMEYASEMA HAYA IMENIKATISHA TAMAA KABISA MIMI MKULIMA WA VITUNGUU

Siku zote Nape anatumia tumbo kufikiri.
CCM imeacha kuwa ya wakulima na wafanyakazi, sasa ni ya wafanyabiashara, mafisadi na magamba.
 
• Adai imeandaa waraka mzito wa kuichafua CHADEMA

na Betty Kangonga

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimedai kubaini mchezo mchafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) unaolenga kukihusisha chama hicho cha upinzani na utetezi wa mafisadi ili kudhoofisha mapambano ya CHADEMA dhidi ya mafisadi.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, mchezo huo umetungwa na maofisa waandamizi wa CCM, wanaolenga kukigawa chama hicho kikuu cha upinzani ili kukisambaratisha.

Akizungumza na waandishi wa habari juzi katika ofisi za makao makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam, Dk. Slaa alisema wamekamata waraka wa CCM unaodai wapinzani hao wamehongwa pesa na mafisadi ili kutibua njama za CCM kuwatimua.

"Waraka wenyewe umeandaliwa na Nape (Nnauye, ambaye ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM), baada ya kuona chama chao kimeshindwa kuwafukuza mafisadi. Sasa wanadai eti CHADEMA imepewa pesa zaidi ya sh bilioni tatu na mapacha watatu.

"Kwa mujibu wa waraka huo, inasemekana mapacha hao watatu walitupatia pesa hizo mwaka jana kabla ya uchaguzi ili kusaidia wabunge wa CCM ambao wangehamia CHADEMA, kwamba kama wangeshindwa uchaguzi pesa hizo zitumike kufidia gharama zao baada ya uchaguzi.


"Wanadai kwamba katika uchaguzi wa mwaka jana tulitumia sehemu ndogo ya pesa hizo, na sasa zilizobaki zinajulikana na Mbowe na mimi (Slaa). Hiki ni kichekesho kweli. Wanadhani wanaweza kuleta mgogoro na kutugombanisha kirahisi hivyo; wanapoteza muda wao."


Dk. Slaa alidai kwamba mbinu hiyo chafu ya CCM inalenga kuhamishia CHADEMA mgogoro wa chama tawala baada ya kuona dhana yao ya kujivua gamba imewashinda kutekeleza.

Alisema watungaji wa waraka huo wanamshutumu yeye (Slaa) kwa kumnasua Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, katika orodha ya vigogo mafisadi.

Hata hivyo, yeye alisema hajatetea ufisadi wa Sumaye, na akasisitiza kwamba ni yeye aliyemtuhumu Sumaye bungeni kuhusu shamba la Kibaigwa alilokuwa analima huku likilalamikiwa na Magereza.


"Lakini Sumaye hayuko katika ufisadi mkubwa huu tunaouzungumzia unaolitafuna taifa. Kama mtu ana vielelezo vya ufisadi wake, ambavyo sijui, atuletee. Sisi tunapozungumzia ufisadi mkubwa hatumwoni Sumaye miongoni mwao, lakini haina maana kwamba tunalinda mafisadi.

"CHADEMA haitaacha vita ya ufisadi hadi hapo watuhumiwa watakapojisafisha. Wao kama wameshindwa kuvuana magamba, washindwe tu, lakini sisi tutaendelea kuwang'ang'ania hadi watakapoacha ufisadi," alisema.

Alisema CHADEMA imeshtushwa na jitihada za serikali kuanza kuwasafisha mafisadi, hasa aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Andrew Chenge, huku CCM ikimtaja kuwa mchafu na anayepaswa kuvuliwa nyadhifa za uongozi ndani ya chama hicho.


Akisisitiza kwamba CCM wanajikanganya wenyewe, hawana sababu ya kusukumia lawama CHADEMA, kwani chama hicho cha upinzani kimejipambanua kwa muda mrefu kuwa kinara wa vita ya ufisadi.


Kwa mujibu wa Dk. Slaa CCM wamekuwa na tabia ya kuiandama CHADEMA kwa kashfa mfululizo za ukabila, udini na "ujinga" mwingine ambao chama hicho kimeupangua na kujihalalisha mbele ya umma.


Alisema hizi ni dalili za CCM kutapatapa baada ya kuishiwa hoja za kisiasa na kukosa mvuto kwa umma. Alisisitiza kwamba mbinu chafu hizi za CCM haziwezi kuinusuru wala kuisafisha mbele ya umma, na kwamba CHADEMA haitakatishwa tamaa na mbinu hizo chafu.


Tanzania Daima lilipowasiliana na Nape kuhusu tuhuma hizo za Dk. Slaa, alisema maneno hayo si mageni masikioni mwa Watanzania, kwani kiongozi huyo amekuwa akiyazusha kila mara.


Alisema hajawahi kuandika waraka wala kumtuhumu Dk. Slaa, kwa kuwa ni mtu wa kawaida, hivyo hana muda wa kupoteza kwa ajili ya kiongozi huyo.


Nape aliongeza kama Dk. Slaa ameshindwa siasa ni bora arudi kijijini kwake akalime vitunguu kuliko kuendelea na jambo asiloliweza.


Kuhusu mapacha watatu, Nape alisema kuwa CCM haijashindwa kuwatimua mafisadi bali kinachosubiriwa ni kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), ambacho ndicho kitatoa hitimisho juu ya suala hilo.


"Hayo maneno ya kusema tumeshindwa kuwatimua mafisadi tumeshayazoea…sisi tunachojua NEC itakapokutana ndiyo itawawajibisha, sasa wanaharaka ya nini?" alihoji Nape.

Alisema Dk. Slaa amekuwa akiwazushia hadi wanachama wenzake ndani ya CHADEMA hata anapohitajika kutoa ushahidi anashindwa kufanya hivyo.

"Hiyo ni tabia yake Dk. Slaa, amekuwa akiwazushia hadi wenzake katika chama na pindi akibanwa aonyeshe ushahidi anashindwa kuonyesha nyaraka, hivyo tumeshamzoea katika hilo," alisema.


 
Mwaka huu tunao, mwaka kesho tunao, 2013 tunaanza kuwapunguza, 2014 wanawehuka kwani mtoto wa miaka 16 leo atakuwa anasubiri kumtoa nyani ikulu. 2015 Nape anahamia msumbiji kutibiwa kwani kichwa itakuwa haifanyi kazi hata amini uvuvuzela wote umekataliwa. Sheria za nchi zitaanza kutekelezwa. Mapacha watakwenda keko, mkuu wa kaya atakwea kisutu, Ben Mkapa atatueleza. jasho la mtu litakuwa kipimo cha utu.

CCM RIP, Nape Nnauye umefulia tunga tu mashairi ya Uongo mwisho utajitungia wewe uongo
 
Hakika wakati wa kuwabana vizuri magambas tunauona!!

Kuna makosa makubwa walipowatosa watu wenye uelewa na weledi wa kisiasa, wakaweka mavuvuzela kama Makamba.... Kakidhoofisha chama chao mpaka ikiko kwenye "beyond repair state"

Well done Dr (PHD)
 
Back
Top Bottom